Wednesday, September 10, 2008

SHUGHULI ZA NYUMBANI


Kuchota maji, kazi hii nimeifanya sana mpaka unapata maumivu ya shingo. Siku moja niliachiwa kuchochea maharagwe nikajisahau kucheza mpira yakaungua . Eee bwana we nilipewa adhabu ya kujaza maji kwenye pipa Mhh! jamani tumetoka mbali sana.

Nakumbuka siku moja wengine wote walikwenda shambani na mimi nikaachiwa mihogo kutwanga ili wao wataporudi shamba wakute unga tayari. Niliacha kutwanga na kuanza kucheza. Kwa sababu nilikuwa sipendi kutwanga kwani mtu unatwanga mpaka unapata(mangelengela) tena afadhali hata mihogo, kukoboa mahidi wee bwana acha tu. Maisha kazi kweli.



2 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Dada yangu na mimi nimekumiss sema karatiba kidoo kamenishika shingoni.

Nipo busy kidogo ndio tunakaribisha majira mengine na kujipanga tena baada ya KIANGAZI.


pamoja nashukuru kwa kunitembelea.

Anonymous said...

Dada Hizo mbona kazi rahisi.
Mimi nilikuwa napangiwa kupiga mahindi gunia nikirudi shule darasa la sita.
Halafu nimetwanga mahindi kwenye hicho kinu hadi kidato cha sita, bahati mbaya kwetu tumezaliwa wavulana basi hapo hakuna kulinga, hapo bado sijabeba mizigo ya kuni (mdembo) ila kwa habari ya maji kijiji changu kimebarikiwe kila mtu ameingiza maji ndani ya nyumba maana yanatiririka tu kutoka milimani.

Umenikumbusha mbali sana