Saturday, September 27, 2008

Matatizo ya uzeeni, Mila na desturi za kubagua watoto wa kike

........................................................

Wazee mara nyingi hupoteza uwezo wa kukumbuka vitu kwa hiyo huwa wasahaulifu sana. Huwa rahisi kuvurugikiwa akili zaidi hasa pale wanapopatwa na homa kali. Mara nyingi wazee wanapata shida ya kukabiliana na mazingira mapya au yanayobadilika. Kijadi mara nyingi wazee ni watu ambao walikuwa wakiheshimiwa sana na kutunzwa vizuri. Heshima hii iliwafanya wajione kuwa ni watu wanaothaminiwa na jamii, na kuwaongezea furaha ya maisha. Siku hizi vijana wengi wanashindwa kuzingatia mila za zamani za kuwaenzi na kuwaheshimu wazee na hivyo kushindwa kuwapa nafasi yao katika jamii. Wazee wa mijini na hata vijijini wanakuwa wapweke bila watu wa kuwasaidia. Sehemu nyingine wazee wanasakwa na kupigwa hadi kufa kwa kuhofia kwamba wao ni wachawi. Hali hii ya kuwatenga wazee na kuwasingizia uchawi ni mojawapo ya matatizo ambayo yanaathiri sana afya yao ya akili.Sijui mila ipi ni nzuri kwani mimi kwa sasa nina mila "mbili" wenzetu ughaibuni wazee wao wanatunzwa kwenye nyumba maalum hii mara nyingi inasumbua akili yangu na nataka nitakapokuwa mzee sitaki kutunzwa na mtu zaidi ya familia yangu je nakosea? semeni ninyi.
. .


Nilizani ubaguzi utapungua lakini, naona hadi leo kuna baadhi ya wazazi ambao wanapuuza elimu ya watoto wa kike na kutoa kipaumbele kwa watoto wa kiume. Mfumo dume huu unachangia kuathiri afya ya akili ya kina mama. Nyumbani watoto wa kike wanatakiwa wasaidie kazi za jikoni na za ndani wakati wa kiume wanasoma au kwenda kutembelea marafiki. Hata katika maamuzi ya familia mawazo ya watoto wa kiume yanapewa uzito zaidi kuliko yale ya watoto wa kike. Waalimu nao mara nyingine wanawajengea watoto wa kike imani potofu kwamba wao hawawezi masomo ya sayansi.

Wasichana na vijana wanawake daima hujikuta wapo kati ya mila za zamani na mila za kisasa, kwa mfano, anapotaka kwenda shule hupambana na mila za zamani, zikiwa za dini au za kikabila.
Hili limekuwa ni tatizo kwani wasichana wa siku hizi hupenda kusoma ili baadaye waweze kupata kazi kabla ya kuolewa. Kwa hiyo wanapolazimishwa kufuata huo utamaduni wanapata mvurugiko wa akili.

1 comment:

Anonymous said...

mmmm mimi sina uhakika kama wanabaguliwa na vipi yule jamaa anaitwa mungu kwa wale watu wa dini pale alipozaliwa Adamu? ule ubavu wa nani aliozaliwa Eva? vipi yale maneno ambayo mungu huyo alitamka baada ya kuwakuta uchi,alimwambiaje mwanamke? au mambo ya zamani sana. TUYAACHE AU? mnieleweshe sijui mwenzenu