Mimi ni mtu mmoja mchangamfu, anayependa kuwa na marafiki ninapenda kuongea na kucheka karibu kila wakati. Na ni rahisi kujenga urafiki na mimi. Napenda sana sehemu ambayo ni tulivu.PIa mimi ni mtu mwenye msimamo yaani nikiamua kitu basi nimeamua(mbishi) bila kusahau ni mdadisi sanaaaa.
Ila pia, mimi ni mtu mmoja mwenye hasira sana kiasi kwamba wakati mwingine huwa najihurumia na pia nawahurumia wale ambao nimewakasirikia. Inawezekana ikapita miezi. Kwa mfano sasa nimeudhika sana kwani baba yangu amenificha kitu ambacho mimi naona nilikuwa na haki kujua. Ni hivi mara ya mwisho kuongea na baba ilikuwa katikati ya mwezi wa sita. Mpaka leo hivi sijaongea naye tena.Ila si uongo natamani sana kuongea naye lakini kutokana na hasira/maudhi nashindwa kabisa. Napenda watu wawe wakweli sio kuficha mambo.
Nadhani wote mnajiuliza KWA NINI? Nadhani wengi mmesoma/ona nimeweka kumbukumbu ya mama yangu. Sasa yeye baba ameoa mke mwingine bila kunifahamisha mimi mnajua inavyouma? Nimekuwa najiuliza je? mimi sio mtoto wake? Je? nimeishi mno Ughaibuni na kusahau mila na desturi zangu? sijui ipi ni sahihi na ipi si sahihi. Kwani kwa undani kabisa najua baba naye ana hamu sana ya kuongea nami na anasubiri kwa hamu sana. Lakini, mimi najiona bado sijawa tayari maana kama mtu umekasirika sana unaweza ukasema maneno ambayo hukutaka kusema. Kwa mtazamo wenu mnaonaje? Je? Nafanya kosa. Naomba mawazo yenu.
2 comments:
Mmm jamani hasira kwanini? inakuwaje umletee hasira baba aliyeamua kujinyakulia kimwana wake? Aaah samahani naleta utani eeh. ni hivi hakika unapaswa kuwa mtulivu kwani siamini kama baba ameamua kutokukwambia kwamba tayari amemchukua mlimbwende a,naye ni mama yako mpya. Siamnini kama baba hatoweza kukwambia hilo. Ila unatakiwa kuwa mtulivu acha akwambie au jaribu kumwuliza kwa utaratibu nin hakika mtaongea kwa utulivu na kujuzana kwanini amefikia hautua hiyo. Lakini iwapo utaleta hasira hakika angelikuwa baba yangu hawezi kukwambia neno bali ananyamaza kwani hii ni tabia za akina baba wengi. Yasinta tulia hakuna sababu ya kuapaniki au kuhuznika kwamba baba hapendi ujue hilo futa. Nina hakia baba anajua kwamba kaka/ndugu zako wamekwambia kwahiyo nadhani yeye anatulia ili akwambie mwane mpendwa kwani anajua kwamba utakuja na hoja pia anajua utashtuka sana. Hongera kwa kumpata mama mpya ingawaje hatakuwa kama aliyekuzaa. Mm nikupe mfano mimi nina ndugu{dada/kaka} watatu wote hawa maa yao amefariki lakini walilelewa na mama yangu tangu chekechea hadi kusoma sekondari lakini sote twaishi kwa amani sababu tunaamini positive atitude kwetu ni muhimu kuliko lolote. Baba yako atakwambia tu kwani naamini hivyo usilie sana,usihuzunike sana kwani ombea uhai utaambiwa mwna mpendwa
Pole sana dada Yasinta,
Mimi sioni sababu kubwa ya kukufanya ukasirike kwa Baba kuondokana kuwa widower (nahisi wanaume huwa hawawi wajane ndo maana mzee Ngonyani kaamua kufanya kweli)
Mimi naona mzee hana kosa kwani kitendo cha kuoa mama mwingine ni maamuzi yake na tatizo tu naona ni mfumo wa kupashana habari kati yake na wewe kwani nahisi kwa simu hapatikani na pia huwezi kumtumie email au fax, pia aliyekwambia ndo alaumiwe. Hata hivyo naamini ukimkasirikia sana basi itabidi this time akuombe ushauri azae watoto wangapi na kisura wake mpya? Mapenzi ni kama shule hakuna mwisho. Hongera sana mzee Ngonyani na dada Yasinta fanya kila njia kumpongeza mzee kwa kukupa mama mwngine.
maoni yangu tu do not be offended!
Post a Comment