Monday, September 8, 2008

WAKATI NASOMA SHULE YA MSINGI

mchakamchaka saa 12 asubuhi

Nadhani wote mnakumbuka wakati mlipokuwa mkisoma shule ya msingi. Asubuhi kabla ya yote mchakamchaka, Usafi wa mazingira n.k.




darasani saa mbili asubuhi


3 comments:

Anonymous said...

Unanikumbusha mbali sana,
Sasa hapo uchelewa shule ile saa moja kamili asubuhi fimbo utakazopata kwa mwalimu wa zamu.
Hata hivyo wengine tulikuwa wajanja kuliko wengine, binafsi nilikuwa natumia ubabe kwa kuwaambia wanafunzi wenzangu hata niwahi au nikichelewa mimi namba yangu ni moja so wakifika asubuhi lazima waanze na namba mbili then waendelee. Ubabe tu!
Lazarus

Yasinta Ngonyani said...

eeh! we kaka ulikuwa mjanja sana. Binafsi sikuhitaji kufanya hivyo kwani nilikuwa dada mkuu.Kazi kweli

Kibunango said...

Bahati nzuri ama mbaya nilisoma shule ya msingi ya bweni huko Longido Arusha. Ratiba ya shule ilikuwa ngumu sana kiasi ya kujiona kama upo gerezani. Kwa ufupi wanafunzi tulikuwa tuna amshwa saa kumi na moja alfajiri ili kukimbia mchakachaka. Saa kumi na mbili asubuhi ni kufagia eneo lako kabla ya kuwahi kwenda kuoga, ile mtoni(wakati wa masika) au kunawa tu uso. Saa moja kamili ni kunywa uji usio na sukari, nusu saa baaadae ni kujipanga foleni kwa ukaguzi wa usafi kabla ya kuingia madarasani. Mchana wa saa sita ni wakati wa kuhwahi ugali na maharage kabla ya kurudi tena madarasani. Saa kumi jioni ni kurudi mabwenini na nusu saa baadae ni kwenda kutafuta kuni kwenye mapori ya karibu. Na inapofika saa kumi na mbili jioni ni wakati wa kupata chakula cha usiku. Baada ya hapo ni kucheza cheza hadi saa mbili usiku ambapo wanafunzi wote utakiwa kuwa vitandani kusubiri tena kengere ya saa kumi na moja alfajiri kesho yake kuanza tena siku mpya...