Sunday, September 21, 2008

VIJIJI/MITAA YA SONGEA

Nimeona labda niingia kidogo vijiji/mitaa ya Songea na umaarufu wake pia

Naanza na:-

  • Peramiho inajulikana sana kwa hospitali yake nzuri, seminari na pia kanisa nzuri.
  • Maposeni kuna sekondari
  • Lundusi anaishi babangu mkubwa
  • Mkurumo ni kijiji alichozaliwa mamangu pia amezikwa pale
  • Morogoro ni mashuhuri kwa hospitali yake ya kutibu wagonjwa wa ukoma
  • Ndirima/mdunduwalo kuna mashine moja ya kusaga
  • Likingo ni sehemu moja ambayo hutengeneza umeme wa nguvu za maji hydro-electric power station)
  • Matogoro maalufu kwa milima mizuri pia chuo cha Ualimu
  • Lizaboni hapa bwana ni maalufu kwa kitimoto mara nyingi tulinunua hapa
  • Mfaranyaki hapa tulikuwa tunatengeneza gari
  • Majengo nilijifunza kuchapa mashine yaani kuna chuo cha uchapaji
  • Mahenge niliishi wakati nasoma typist
  • Bombambili ni stendi ndogo kwenda Njombe - Dar
  • Litapwasi ni maalufu kwa uchomaji mkaa

kama nimesahau mitaa au vijji vingine basi samahani au nitaandika siku nyingine. Jumapili njema

7 comments:

Unknown said...

Hongera kwa kujuza wengine ambao tulikuwa hatujui,
hebu nicheki kwenye
www.gshayo.blogspot.com
or my email
godlistensilvan@hotmail.com.
Muwe na wakat mzuri.

Fita Lutonja said...

Nimeona profile yako kumbe uko kuleeeee!!! ongera sana. Pia asante kwa kututabayabarisha na cc ambao 2likuwa ha2jui sehemu kama hizo pamonja na kwamba rafiki yangu Markus huwa ananiambia mambo mengi sana ya huko huwa ninapata hamasa sana kupaona sehemu kama hizo, asante dada Yasinta

Kibunango said...

Shukrani kwa useful post, hivi mtaa ambao Songea girls ipo unaitwaje? Na Songea Boys ipo mtaa gani?..... Shule ya msingi Majimaji nayo ipo sehemu gani?

Yasinta Ngonyani said...

kaka kibunango inaonekana unajua sana Songea. Kusema kweli nimesahau wapi boys,girls na pia majimaji shule ya msingi ipo mitaa gani. unatoka songea pia au?

Kibunango said...

Hapana, sitoki Songea ila nimewahi kupita Songea zamani kidogo kama miaka ishirini sasa, hivyo nahitaji kusafisha kumbukumbu yangu ya mji huo... Bado nakumbuka maeneo machache tu ya Songea Mjini na Mbinga..

chemshabongo said...

amani iwe kwako! tupo pamoja

Anonymous said...

Waaaaaaaaaaaaaaaoooooooooooooooooo kwanza nimekubali mabadiliko ya blogu yako nimefurahi sana leo kwani nina siku tano sikupenda kufurahi wala kuhuzunika niliamua kula wakati mzuri mitaa ya upanga west beach pale jirani na aghakhan kuelekea sea view kuna miamba/makorongo mazuri sana huwa yananikuna sana. kuhusu mitaa nadhani umesahau makunganya ambao upo maeneo ya uwanja wa majimaji,halafu kuna mji mwema,matarawe,mateka ambako upande wa pili kuna songea girls. suala la songea girls linanipa homa kwani nikiangalia ramani naona mtaa wa majengo kwani barabara yake inakwenda hadi shuleni pale kisha kuvuka ng;ambo ya pili ambako kuna mtaa wa mateka. Songea boys nafikiri kwa haraka kama sikosei nadhani ni mtaa ulioanzai na jina la songea boys au kifupi unaitwa boys, umesahau mtaa wa zanzibar ambao ndio upo katika maeneo makuu ya mjini labda tatizo hautajwi sana ila ukiangalia katika ramani za manispaa unatajwa hivyo,mtaa wa mashujaa,ruvuma mmm iko mingi yaani ni maeneo ya pale wengine nikosoeni basi au ongezeni