Sunday, December 7, 2008

SALA YA MUME AKIMWOMBEA MKEWE

Hapa nimejaribu kubadili maneno kutoka kwenye ila sala ya kumwombea mke au niseme ni kama mfano vipi mume anaweza kumwombea mke wake.


Ee Bwana, wakati mwingine namtazama mke wangu Nami nashangazwa.
Inakuwa kama ni kwa bahati tu nilikutana naye.Siku ile ya kwanza,
Tulikutana na kila mmoja alikuwa mgeni kwa mwenzake.Sasa ninamjua sana.
Lakini bado ninashangaa na kujiuliza.Bila yeye ningekuwa mtu wa namna gani?
Ningefanya nini?

Je? Ningekuwa nimefanya mambo mengi hivyo?
Je? Ningekuwa bado nikitafuta?
Nikitafuta anasa mbaya za maisha, nikiondoa upweke na uchungu,
Kwa chupa moja ya bia baridi au kwa kumtembelea rafiki.

Ninajua kwamba nimebadilika, yeye alinibadilisha.
Upendo wake, na upole wake, kunitunza kwake, na subira yake,
Vimenifundisha na kunijenga.Amenifundisha niwe zaidi,
Niwe zaidi mtu yule uliyetaka niwe.Amenisaidia niwe hivyo
Mlifanya kazi pamoja, ulifanya kazi ndani yake
Naye katika wewe

Ninyi -wawili- Bwana,
Mlinipa moyo, mlinipa nguvu,
Mlinipa amani ya kweli, raha na furaha.
Mlinisaidia, nikajiamini.

Na nikakuamini.
Kwani, Ee Yesu mpendwa, ulikuwa mgeni.
Picha kwenye kitabu, Mtu aliye angani mbali nami.
Mpaka nilipokutana naye.

Kwani alinionyesha nafsi yangu mwenyewe. Na alinionyesha wewe.
Alinipa watoto, watoto wako Ee Bwana. Sasa ni watoto wetu

Hali hii tuliyo nayo leo hii, ni dalili ya upendo wako,
Ninakushukuru kwa ajili yake,umbariki na unlinde.
Umweke salama, na unifundishe jinsi ya kumpenda zaidi.


NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

Hapo da Yasinta umefunika mbaya. Kiukweli ni jambo bora kuliko kwa wanandoa kuwa wanaombeana badala ya kunyosheana vidole. Ndoa yenye watu wa namna hii, wanaokumbuka kuombeana ni ndoa yenye mafanikio na furaha na amani.
Mi nadhani tuachane na usasa mwingine unaotujaza umajinuni na tukumbuke kuombeana ili kutoziruhusu nyufa katika mahusiano si tu ya ndoa, hata ya kawaida. Tujifunze kuwaombea wazazi, kaka na dada zetu, wadogo zetu, ndugu, jamaa na marafiki wote. Kwa sababu hao wote wanao umuhimu katika maisha yetu kila mtu kwa nafasi yake.
Lakini, mume na mke hawana budi kulijua hili, na kuenenda katika kuombeana na kutakiana heri.
Mungu atujalie na kutuongoza sisi ambao bado tunasaka wenza ili tusipate nafasi ya kuyajutia maamuzi yetu.
Nakupongeza da Yasinta kwa ubunifu wako wa hali ya juu.
Jumapili njema.
Ahsante sana.

Rashid Mkwinda said...

Duuu bwelayi chenjelai ba bomani hapa, mmmh ubweli chi gafula, nimekuona dadangu, umetulia tulii kama maji ya mtungini, hivi hiyo ndoto yako ya utawa imeishia wapi?

Fadhy Mtanga said...

Unaona sasa da Yasinta? Kila mtu anataka kujua ndoto yako iliishiaje? Mi nadhani hapo kwenye profile ungeongeza kasentensi mtani ukielezea kwanini ndoto haikutimia.
Mzee wa Mbeya, hiyo ndo lugha gani? Umeme umewaka? Poleni sana.
Ni hayo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy asante kwa kinitembelea mara kwa mara.

Na kaka Mkinda karibu sana kijijini kwangu ni vizuri kutembeleana kubadili mawazo.Na chilawu mewawa. Huo mjadala wa utawa(usista) tutaongea siku nyingine.

Unknown said...

Nimeikopi na nitaiprinti na kuiweka ukutani kama ile ya kwanza ya sala ya mke kumuombea mume.
kazi nzuri sana dada Yasinta.