Wednesday, December 3, 2008

KWA NINI WANAUME/AKINA BABA WENGI WANAFIKIRI WAO NDIO WAAMUZI/WAFALME WA NYUMBA?

Suala hili limekuwa likinikera sana akilini mwangu kwa miaka mingi. Ya kwamba akina baba/wanaume wao wanafikiri kazi yao kubwa katika nyumba ni kuwa MUME/BABA basi. Mara nyingi utasikia wanasema mimi ndio mkubwa wa nyumba. Na kama wanafanya kazi za ofisini basi ndo itakuwa kero mno. Kwani hapa atataka anaporudi toka kazini akute chakula mezani, maji ya kuoga bafuni tena ya moto, nguo zmepigwa pasi n.k. Na kinyume kama hana kazi basi atakuwa anashinda kilabuni(UGIMBI) na akirudi toka huko basi ni kelele tu, hakuna amani wala maelewano

Bado naendelea, kuna wengine wanaona kupika, kulea watoto, kutafuta chakula ni kazi ya wanawake. Yaani hawawezi hata kujipikia chai kwa vile wao ni wanaume au hata kumbadili mtoto nepi, Mtoto amabaye ni wake. Kikubwa wanachofanya ni kukaa kitini/sofani na kuletewa kile wanachotaka. Wanasahau kabisha jambo la USAWA.

Bado wanaishi dunia ya mababu, mababu na mababuzi. Tuache UBINAFSI tuishi kwa kushirikiana/kusaidiana kwani wote ni SAWA. Nasema tena tuishi kwa kusaidiana hapo wote tutafurahia maisha. Tuache mambo ya UTUMWA.

10 comments:

Simon Kitururu said...

Smahani Yasinta natoka nje ya topiki. Katika utambulisho kuhusu wewe kwenye blogu hii , umesema uliwahi kutaka kuwa sista. Nini kilikugeuza mawazo?


Kuhusu kwa nini wanaume wanaleta kibezi nyumbani , nitarudi baadaye kujaribu kuelezea mtazamo wangu!
Siku njema!

Yasinta Ngonyani said...

Ndio Simon Yaani nilitaka kuwa sista hii ilikuwa ndoto ila sijawahi au sikupelekwa utwani nilikuwa napenda. je nimejibu vizuri.

Nitafurahi ukirudi na kuelezea mtazamo wako wa kwa nini waume wanaleta kibezi nyumbani.

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta, kwanza mambo vp?
Pili naomba ujibu swali la bwana mkubwa Kitururu hapo juu. Unajua ungeifuata ile ndoto yako mtani wala leo hii usingejiuliza maswali kama haya. Nakosea mtani?
Narudi kwenye hoja yako. Kwa kuwa we ni mkristo tena safi, kasome Mwanzo 3:16. Naomba ukisoma ulete hapa kijijini nukuu ya maneno hayo ili wanakijiji wote tuone kwa nini inakuwa hivi.
Lakini pia ni vema tukakubali kuwa katika kuishi lazima kuwepo na kiongozi wa familia. Hayo ya ukandamizaji wa wanawake nadhani, kwa mtazamo wangu yameathiriwa na mfumo wetu wa kihistoria wa uongozi wa kifamilia tangu karne na karne wanadamu walipoanza kuishi pamoja.
Haya mambo ya ugimbi (unaujulia wapi mtani?) na mienendo mingine isiyofaa katika ulezi wa familia, nadhani ni mapungufu binafsi ya watu. Kuna wanawake ni vimeo full pampula kiasi kwamba hajui watoto wamekula nini. Nimewahi shuhudia mke wa rafiki yangu akimtandika makonde jamaa hadharani. Hadi naogopa kujiunga kwenye klabu ya wasio maseja.
Najua sijajibu ukamilifu hoja yako, sijafanya hivyo ili utuletee nukuu hiyo ya Biblia kisha twende sawa.
Ahsante kwa hoja iliyosimama dadaangu.
Ni hayo tu!

Christian Bwaya said...

Mimi nadhani wanaume wanafikiri kuwa waamuzi wa nyumba kwa sababu wanawake wenyewe wanaamini mambo ndivyo yanavyotakiwa kuwa. Yaani ufalme wa nyumba hautokani na mwanaume mwenyewe, bali mwanamke mwenyewe.

Ni suala la kisaikolojia zaidi.

Yasinta Ngonyani said...

Fadhy, Nilidhani nimeshamjibu kaka Simon au?
Nimesoma Mwanzo 3:16, kama nimeelewa inaonekana Mungu alitoa adhabu kwa wanawake kwa kusema maneno yale. Ni kweli au ni imani tu?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta wewe ni mkristo mzuri hivyo usiulize maswali ambayo biblia inayajibu. kibiblia mwanamke ni mt...... sijui niseme nini na unapalaumu wanaume kuwa na mawazo ya kizamani na yakitumwa, wewe unajiweka wapi? mbona unaamini biblia ya zamani? you seem to be confused. ungesomea usisiter, kuna vitu vitamu ambavyo unavipata leo usingevipata au ungevipata kwa kujificha na visingekuwa vitamu tena.

nadhani wanaume wanasifa fulani. tatizo hapa tunachanganya kati ya majukumu ya mume na ya mke. wangapi wametembelea mbuga za wanyama na kuona jinsi simba dume anavyotukuzwa na simba jike? au hata kufuga na kuona jinsi mume anavyoonekana kuwa juu?

mimi nadhani wanawake wako juu kukliko wanaume na wanajishusha kwa kutaka kuwa sawa na wanaume. NI MTIZAMO

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta bora umesoma hapo na umeelewa. Mi siwezi kusema wamepewa adhabu ama lah. Ila nilitaka tu kukuchokoza baada ya wewe kuleta suala hilo.
Da Yasinta, kiukweli dunia inabadilika. Kuna mabadiliko kijamii hatuwezi kuyakataa. Suala la kibesi kama anavyoita kaka mkubwa Kitururu nadhani linapaswa kutazamwa upya kama lina ulazima katika kizazi hiki. Kizazi ambacho wanawake siyo magolikipa tena, bali wachangiaji wakubwa mno wa maendeleo ya jamii tukianzia kwenye familia.
Nimekosea? Ni hayo tu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapo ndipo lilipo tatizo la kuzaa mitoto isiyokuwa na muelekeo. mama kaenda kutafuta baba naeye hivyo hivyo, wakirudi wamechoka, wanajifungia chumbani, watoto wanalelewa na \Tv kakusaidiana na housegirl mwisho wa siku hao wanaigiza ya kwenye TV. utafiti unaonyesha watu wazuri na watulivu kama akina Nyerer, JF kennedy, mimi na wengineo tunanidhamu na utu kwa sababu ya kukaa karibu na mama muda mwingi.
inasemekana mamake kennedy aliacha kazi ili kulea wanae kwa nidhamu. vivyo hivyo mamangu

Yasinta Ngonyani said...

Sawa bwaya nimekuelewa na karibu sana tena Ruhiwiko.

Fadhy ni kweli sasa kuna madadiliko ambayo yanatokea kila siku ni kweli siku hizi akina mama wengi ni wafanya kazi maofisini.

Kamala kuwa na mama muda wote si kwamba unakuwa na nidhamu kama usemavyo kuna wengine hawana baba wala mama na wana nidhamu nzuri sana.

MARKUS MPANGALA said...

MAKSI 100 kwa kaka KALAMA!!!!!! wanawake??? huwa najiuliza kwanini wanapewa nafasi ya upendeleo wakati wote tulizaliwa huru? namkumbuka Profesa mmoja anayenifundisha somo la manendeleo, anasema ninyi wanawake mnasema mnatawaliwa, semeni mnatawaliwa na nani? na kwanini imekuwa hivyo? je nanyi mwataka kutawala? je mnatawaliwa kwa lipi? mwanaume anakibezi, ha ha ha kibezi bwana ni mawazo tu yaani vitu vya kufikirika tu lakini kibezi YALIYOANDIKWA NI LAZIMA YATIMIE ninyi si wakristo au waislamu? mnasahau? basi msiamini yale maneno ya kina Luka sijui Marko na jamaa kibao. shauri yeni wanawake ndiyo maana mnahangaika kufanya PANEL BEATING ya uso ili mlete kibezi? Nakubali kwamba tatzio wanawake wanajishusha wenyewe, utaona mimi siataki kundi la kusoma wanawake watupu tunadanyana sana bora kuwa na wanaume ebooo! lakini nakumbuka kuna dada mmoja alikuja na hitimisho tatizo la wanawake ni WIVU ndiyo maana wanaona kila jambo lazima mwanaume atawale
HABARI NDIYO HIYO NAONGEA NA NINYI akina mama, eti haki sawa nafasi za upendeleo yaani nacheka sana hata umoja wa mataifa una ajenda za kuwasiadia wanawake ili wawe na kibezi nyumbani thubutu milele hamtasimama.
najua nawafanya mwaze kitu lakini ndivyo nilivyo??? nipo hivyo? nawakilisha akina nani? siju JIKOMBOE SASA, UHURU DAIMA