Monday, December 8, 2008

KUASAIDIA KAZI ZA NYUMBANI

Hapa nimekumbuka nilipokuwa mdogo kutoka tu shuleni kwenda kuwafungulia mbuzi. je? kuna mtu ambaye hajafanya kazi hii.

15 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Hii ni nguzo njema na mafunzo mema ya mtoto kuelekea utu uzima. Kujifunza kujitegemea na pia majukumu mengine ya kifamilia mbali na wale walio ndani. Ni kujifunza kujishughulisha na harakati za kimaisha na ni kati ya mambo ambayo kwa jamii ambazo zinapoteza haya, basi zihakikishe kuwa zina msingi m'badala wa kuwalea vijana wajao.
Asante Da Yasinta kwa kumnbukumbu hii ambayo wengi tumepitia

Fadhy Mtanga said...

Da Yasinta, we ni kichwa kweli kweli. Wanasema maisha anayoyaishi binadamu wakati utoto huwa na athari katika maisha ya ukubwani. Kazi hizo ambao wengi tumezipitia ndiyo zimetufanya tuwe hivi leo. Uwezo wa kufikiri, kujitawala, kujitegemea na uchapa kazi. Nakumbuka nikiwa mdogo nilikuwa hodari wa kuchunga ng'ombe, pia nyumbani ilikuwa ni lazima nioshe vyombo na kupiga deki. Nashukuru sana kwa malezi yale.
Kwa mantiki hii nakubaliana na mwandishi wa riwaya wa Kirusi, Feodor Dostoyevski, aliyepata kuandika, 'The second half of a man's life is made up of nothing but the habits he has acquired during the first half."
Bila shaka hapa tunakwenda sawa.

Eid Mubarak!

Yasinta Ngonyani said...

Mubelwa ni kweli nafurahi kama nawe umepitia kazi hizi.ni kweli hapo ndio mtu unaanza kujitegemea kwani ipo siku utakuwa peke yako au sio?

Fadhy nawe naona hauko mbali kwa hiyo nakuomba haya mambo uliyojifunza wakati u mdogo basi endelea nayo mpaka uzeeni.

MARKUS MPANGALA said...

aaaah nakumbuka 2003, nipo kidato cha tano nakwenda shambani kung'oa mihogo na mtoto wa dadangu alikuwa binti wa miaka 14 tu yaani nyumba nzima watoto wa kike hakuna walikuwa shule, mama kazini. mmmm mtoto wa kiume nangoa mihogo+kumenya+kuloweka+kuchota maji kisimani LAKINI wadogo zangu wamefika kidato cha 4 siku hizi kibesi sana. nakumbuka mengi kiasi ambacho mama yangu anawakumbusha nilivyokuwa sijali mwanaume kutulia nyumbani mmm aiseh nakumbuka mbali sana kazi utadhani mtoto wa kike. Lakini kwangu ni poa tu kwani haijaniondoa katika uhalisia wangu. wengi tunadhani kazi za nyumbani zimeumbwa kwa ajili ya wanawake LAKINI mbona wanaume wengi wanafanya kazi za upishi mahotelini au migahawani lakini wakifika nyumbani hawataki wao kibesi tu hivi inakuwaje hapo??????

Yasinta Ngonyani said...

Mimi wala sishangai, katika familia yangu hakuna hili jambo la kusema kazi ya wanawake au ya wanaume. Kwani mimi nilikuwa mtoto wa kike peke yangu muda mrefu sana. Kwa hiyo kaka zangu hawakuwa na ubaguzi wowote ule. Wanaweza kuosha sufuria ya ugali,chungu, kutwanga, kufagia, kudeki pia kuchota maji na bila kusahau kupika.

Nwashukuru sana baba na mama kwa kutulea hivi leo kila mtu anaweza kujitegemea. Hata mwaka jana walinipikia ugali. RAHA SANA!!!:-)

Fadhy Mtanga said...

Hongera sana kama kaka zako walikupikia ugali mwaka jana. Nashukuru sana nimekuwa na tabia hiyo hadi leo. Kila niendapo nyumbani kusalimia huwa napika walau mara moja. Hupenda kwenda nyumbani kwa mama wakati wa Xmas, siku yenyewe, familia nzima huenda kanisani, mi hubaki nyumbani (uvivu wa kusali huu, siyo mzuri). Naandaa msosi na kila kitu. Wao wakirudi hukuta mambo shwari. Nimejizoesha hivi tangu nikisoma, ili kuwaonesha wao kuwa nawathamini.
Tabia hii iliniponza Xmas ya mwaka jana. Mitikasi za maisha zilinipeleka mbali, nikashindwa kusafiri hadi nyumbani kwa Xmas. Nilisikitika sana mamaangu hakuweza kula siku hiyo. Alinitext akisema nilimzowesha vibaya. Namwomba Mungu anijalie Noeli hii nijumuike nao nyumbani.
Nimejaribu tu kuungana na wenzangu kuonesha namna tunavyowajibika na kujituma hata katika shughuli ambazo wengi wenye mtazamo wa kake hudhani ni za wanawake.
Ahsante da Yasinta kwa mada hii, umenifanya nikumbuke kisa hiki.
Ubarikiwe sana.

Yasinta Ngonyani said...

Safi sana Fadhy nazidi kukupa moyo na hata utakapooa fanya hivyo hivyo utaoana utamu wa maisha. Ni uzoefu wangu tu

MARKUS MPANGALA said...

haya wanandoa mnafundana kazi kweli kweli, haya kazaneni mtusaidie nasi. lakini UTAMU WA MAISHA NI NINI dada Yasinta?

Yasinta Ngonyani said...

Mrkus UTAMU wa Ndoa ni kusaidiana/kushirikiana. kila kitu kufanya/kupanga pamoja.

Anonymous said...

si mchezo, haya mambo ya kazi za nyumbani yamenikumbusha mbali sana. Mimi ni mwanaumelakini nilikuwa nafanya kazi zote za nyumbani isipokuwa kupika, na kunyoosha nguo zangu mwenyewe. Nilikuwa natwanga, nachota maji kisimani, naosha vyombo, napika sufuria ya ugali (chaliku) lakini kusonga ugali ni marufuku (hilo hata kwa viboko sikuwa tayari kufanya sijui kwanini, nakumbuka kuna wakati mama alikuwa ananituma wakati anasonga ugali, then nikirudi nakuta wamemaliza kula ugali na amepika chaliku ili nisonge mwenyewe ugali, lakini sikuwahi kufanya hivyo, nilikuwa tayari kushinda na njaa, alijaribu mbinu nyingi za kunifanya nipike ugali, lakini sikuwahi kufanya hivyo, wenzangu wote wanapika pamoja na kaka, baba nae ndio alikuwa mpishi mzuri kuliko hata mama), nilikuwa nafua nguo za watu wote nyumbani, zangu, wadogo wangu, za baba, za mama, nanyoosha nguo za wenzangu wote isipokuwa zangu mwenyewe, sijui ni kwanini sijui kunyoosha nguo zangu mwenyewe. kunyosha nguo zangu ilikuwa ni kazi ya baba, maana bila hivyo haikuwa hatari kwangu kuvaa nguo iliyojikunja kunja. na sasa hivi nimeoa na kakilema ka kutopenda kupika kanaendelea na pia kunyoosha nguo zangu hapo kuna kasheshe, nitanyoosha zangu, za wanangu na mke wangu, lakini zangu mwenyewe naona uvivu mpaka mke wangu anisaidie. Hivyo nawashauri wengine kama wanaweza kujifunza haya mambo tangu utotoni.

Bambu Tengeneza

Yasinta Ngonyani said...

Bambu Tengeneza uvivu huo. au vipi uyogopeye moto. Ila hata hivyo unajitahidi. Ila ningekuwa mimi mkeo ungeipata. ha ha ha ha!

Anonymous said...

lakini sidhani kama ni uvivu, kwani kama ni uvivu mbona kama kunyoosha nguo za wengine nanyosha, kuchota maji nachota, mashine naenda kusaga, na kadhalika, ila kupika ndio noma. kuna kipindi mama alikuwa ananiacha nyumbani na wadogo zangu na kuniagiza nihakikishe wanakula, sio mchezo, nilikuwa napika chaliku, halafu naenda nje kuvizia nikiona mwanamke anapita namuomba aje kutusongea ugali, na haikuwa kazi kubwa kwangu kupata mpishi wa muda kwani tunaishi jirani na kituo cha magari (kituo cha bus), na hapo kuna watu wanakuja kufanya biashara ndogo ndogo, hivyo nilikuwa naenda tu navuta mwanamke mmoja kuja kunisaidia kupika ugali, mshahara wake ni kula ugali (ugali tu na sio ugali wa wakubwa kwani wakati huo nilikuwa mdogo jamani, tehetehe).

Yasinta unasema ungekuwa mke wangu ningeipata, unasema tu wewe, mwenyewe ungenywea, kwa mfano mimi nimeoa mwanasheria, lakini uanasheria unaanzia mlangoni, akiwa ndani ni mke kama mwanamke mwingine, kizuri ni kwamba tunaelewana na kuendana, na mie ni hivyo hivyo, ualimu wa wangu wa watu wazima huko huko, nikifika home ni mwalimu wa watoto wadogo (baba, hapo ni kufundisha kwa mfano, lakini hawajui kama baba yao kunyoosha nguo zangu ni kasheshe), wananiona tu nanyosha zao na za mama yao, na mama yao ananyoosha zangu hawajui kama kwangu ni kilema kunyosha zangu, kazi ipo (hapo nimefanikiwa kuwapiga changa la macho wanangu, hawajui hata robo)

Bambu Tengeneza

Yasinta Ngonyani said...

Ningependa sana kujua jina la lako la kweli kwani nina ujumbe wako.

Anonymous said...

Yaani Yasinta umekuwa Tomaso wa kweli, hilo ni jina langu la kweli, sema unataka jina lingine nililobatizwa kanisani ambalo nipo katika mchakato wa kuliacha, nitakupatia jina langu kwa email kama inawezekana.

Bambu Tengeneza

Anonymous said...

nimejaribu kuitafuta email address yako sijafanikiwa kuiona, hivyo kama una ujumbe naomba nitumie kwa address hii
remmygama@yahoo.com