Wednesday, June 27, 2012

KWELI ZILIPENDWA HASWA!!!!

NI KILE KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO YA MARUDIO NA LEO NIMEONA TUWA HAPA HAPA YAANI NDANI YA BLOG HII KWA KURUDIA NA PICHA HII NILISHAWAHI KUIWEKA  KWA KUKUMBUSHA ANGALIA HAPA KAPULYA. KARIBUNI SANA.....
Kitu kimoja nasikitika sina picha ambayo nilikuwa kabinti kadogo sana. Najiuliza sijui nilionekana vipi lakini sipati jibu. Panapo majaliwa tuonane tena JUMATANO IJAYO....Kaaaazi kweli naipenda zamani/zilipendwa kwa kweli..inaonekana niliupenda huo mpapai au sijui ndo ulikuwa mtindo kusimama kwenye miti..LOL

32 comments:

Interestedtips said...

u mrembo sana my dada, enzi zako hizoooooo, matunda kwa afya si lazima dokta aseme, jumatano njema pia

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Katika picha hiyo ya mwaka 1993 namwona Camila!!!! Ama kweliiii

EDNA said...

Daaah ulikuwa bomba sana mtani wangu.

PASSION4FASHION.TZ said...

Zilipendwa na zinaendelea kupendwa,hahahahaaaa hapo upo bombi kweli,kweli mtani wangu...lol!

ray njau said...

Kichagga wanasema:Nokuo na ucha wopfo[Unazeeka na uzuri wako].

Interestedtips said...

Ray una misemo weweeeee, ila msemo wako una ukweli ndani yake

Anonymous said...

Hongera sana dada kwa nguo zako za heshima tangia enzi hizoooooo lakini yee sketi yavii ya mpyela yeniyo mbomi rahaa mbaka mmoyo - bambu mbawala

ray njau said...

@Ester;
Asante sana kwa pongezi zilizohanikizwa na shukrani ndani ya asante kutoka katika papachi za moyo wako.Kama vile chumvi na nazi huongeza ladha katika maharage na mboga za maji bila kusahau mlo wote kwa ujumla wake na misemo huongeza ladha ya mazungumzo na utamu wa hadithi unazidi kukolea.
Picha ya Yasinta inatukumbusha kuwa mavi ya hayanuki na daima ya kale ni dhahabu.Mwanamke anayedumisha maadili na staha ya kike anapaswa kuiga kielelezo za picha hii kwa kuchagua mavazi yanayoweza kuhifadhi vema maumbile yake ya kike kwa kuwa hiyo ndiyo fahari ya mwanamke.Wanawake wanaweza au ni lazima wawezeshwe kwanza???Nashindwa kuwaza kwa sauti!!!

ray njau said...

"Mavi ya kale hayanuki"

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote kwa uwepo,pongezina upendo wenu. Ni ruksa kuendelea na mada/picha hii ya leo.

ray njau said...

@Yasinta;
Kwa upendo wako tumekupokea na jehazi moja bado tunasafiria.Omo na tezi marejeo ngamani.

Rachel Siwa said...

Yaani mwali wewe ulikuwa mrembo tangu zamani!!!!!!

ray njau said...

@Rachael;
Umeamua tucheke au????

Mija Shija Sayi said...

Yaani hapa umefanana na rafiki yangu mmoja anaitwa Twendilwe...yaani duh!

Yasinta wewe fashionista, ni basi tu!!
Kumbe makorokoro ya kiafrika shingoni umeyaanza siku nyingi?

Hongera sana Da'Mkuu..

Bennet said...

Huu mpapai umenikumbusha nika post kilimo cha mipapai leo

emuthree said...

Heri mimi sijasema, ...lakini ngoja niseme,hii picha ndiyo ile uliyompa shemeji kipindi kile...!

ray njau said...

@emu-three;
Makofi kwako tafadhaliiiiiiiiiiii!!!
Umesema na wote wamesikia na huenda huo ndiyo ukweli wenyewe au yeye mwenyewe anasemaje?

Rachel Siwa said...

Jamni kaka Ray kwanini mcheke?au kwa furaha!!!!!pamoja sana.

Simon Kitururu said...

Mtoto mzuri kweli weye! Ungekuwa hauna Mmme...........yani sijui!:-(@Kadala

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

We Kapulya we Kapyula. Acha nijiachie unyayo. Maana mengi yameishasema.

Yasinta Ngonyani said...

Ray..Ahsante!!
Rachel! unajua kuchekesha wewe!! si unaona hadi kaka Ray kacheka:-)
Mija! duniani wawili wawili.. fasheni..tumetoka mbali..
Kaka Benet! nafurahi kama umepata kumbukumbu.
Emu3!wewe kumbe muchukozi..ngoja nimuulize kama ni hii..LOL
Ray! ha ha haaa unajuaje kama kapatia?
Rachel!ni kweli umenifanya hata mie nicheke..kwa furaha:-)
Simon/Kadoda! mbona hujamalizia hapo kwenye deshi?
Mwl.Mhango Ahsante kwa kupita hapa nina hakika hata nawe ulikuwa na la kusema ambalo tayari umesema...

Samuel Kadyakale said...

Wow! you have not changed much. You have really taken good care of yourself and still look young.

ray njau said...

@Samuel;
That is good,very goooooood!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Brother Samuel! I am trying thank you so much...

ray njau said...

@Yasinta;
Thanks for thanks!!

Mija Shija Sayi said...

Kitururu Kitururu,..mbona wako wengi tu wasokuwa na waume? mi naona kakangu labda una masharti magumu mno hadi wadada wanaona isiwe taabu, kweli si kweli??

Stay blessed u all..

ray njau said...

@Simon;
Hoja ndiyo hiyo na wadau tunasubiri mchango wako kibarazani kwa kadala!!!

siglada said...

umenikumbusha mbali sana nafikiri hapo ni wilima on those days

Simon Kitururu said...

Mie Msumbufu sitaki kusumbua Mtu!:-)@Mwanamke wa Shoka Mija

@Kapulya/Kadala: Mambo mengine siri!:-)

ray njau said...

@Simon;
Uhuru wako uanaishia pale wa mwenzako unapoanzia.Mkuu umesomeka vema na hoja binafsi imekamilika.

Simon Kitururu said...

Hahahaha@Mtani wangu Mchungaji Ray

ray njau said...

@Simon;
Asante sana kwa maneno mazuri na kumbuka kuwa mimi ni mtenda kazi asiye na faida na hapa natimiza tu kile ambacho huenda kikawa ndiyo matarajio ya jamii yangu.