Friday, June 29, 2012

MAISHA:- NIMEGUSWA SANA NA HABARI HII NA NIMEKUMBUKA MENGI, AMA KWELI MAISHA NI CHANGAMOTO KUBWA YA MAISHA!!!


MAMA MJAMZITO AKIPELEKWA HOSPITALI
Ni juzi tu nilikuwa nasikiliza/angalia habari. Mama mmoja mjamzito alipatwa ghafla na maumivu ya tumbo. Na alipotoa taarifa kwa gari la kubeba/kuchukua wagonjwa lilichelewa kuja . Lilikuja baada ya kama nusu saa. mama mjamzito huyo maumivu ya tumbo yakazidi na akawa anatoka damu. Alikuwa na ujauzito wa miezi saba. Kiumbe kilizaliwa kimekufa.....
Na ndiyo nimekuja kukumbuka jinsi wanawake wengi wanavyo poteza maisha kutokana na umbali wa hospitali na usafiri. Nakumbuka wakati tunaishi kijiji cha Kingoli kulikuwa  na gari moja la kijiji, duka moja kanisa moja, shule moja. Sasa hapo mtu uwe mjamzito hakuna nafasi ya kupona kama kunakuwa na shida kama ya huyu mama. Maana kutoka hapo kijijini hospitali ni Peramiho na kufika huko ni siku mbili kweli kuna kupona hapa? Ndo nikawa najiuliza sasa kama unapiga simu na watu wanachelewa kuna kuna maana gani sasa si sawa na kule kwetu Kingoli tu baiskeli au machela.... Ebu tumalizie   kijana Side boy na wimbo huu JIFUNGUE SALAMA...

IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA.!!!

7 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Yaani kwenye hiyo baiskeli ni vurugu tupu...hebufikiria kitoto kikianza ku-hindukahinduka tumboni kazi inakuwa kwa wasindikizaji... :-(

emuthree said...

Usishangaye hayo ya kijijini, hapa Dar je,....

Maana kuna maeneo ukifika, sehemu ya kupita ni upenyo, barabara ipo mbali, fikiria mama ndio kazidiwa, na tarehe zimepishana,.

Hata mgonjwa wa kawaida tu, kazidiwa, mtamtoaje hapo hadi barabarani,...
Mipango miji haija kaa sawa, ....

ray njau said...

Hizi ndizo changamoto zetu katika maisha na mafanikio!

Yasinta Ngonyani said...

Kila nikikumbuka na kila nikiendelea kusikiliza ujumbe huu napatwa na uchungu sana inauma inauma mno...

sam mbogo said...

unajuwa ,wakati mwingine haya mambo tunayakuza tu.tumekimbilia sana mambo ya hositali kuwa ndo kilakitu na mama anaweza kujifungua kwa usalam,nikweli lakini siyo wakati wote mama akiwa hosipitali atajifungua salama.tuna sahau mazingira yaliyo tuzunguka, kuna wakunga wa jadi ambao tangu enzi naenzi wapo na walikuwa na utaalamu wao mzuri tu na watu tulizaliwa nakukua.lamuhimu hapa,hosipitali sawa nimuhimu lakini waliowengi kijijini usafiri ni taabu,kwanini tusi boreshe huduma hii ya wakunga wa jadi wanao tambulika katika vijiji na kuwapa au kuwaongezea utaalamu zaidi kutokana namaisha yalivyo badirika na tuonekama hawa tatoa huduma nzuri,kwani watakuwa karibu na wananchi na inakuwa rahihisi kutoa huduma badala ya kuanza kufikiria safari ya kumkimbiza mama mjamzito hosipitali.najuwa serikali inalijuwa hili ila basi tu uwajibikaji ni mdogo. wakatimwingine husahau tuliko toka na kukurupuka bila kujifunza nini tulikifanya kablaya haya mahosipitali kufunguliwa/kuanzishwa,kuna mahali bado hatujapapatia katika kutoa huduma za kija mii tanzania,tuna safari ndefu,ila nina uhakika kwa wataalamu tulio nao kama wataacha ubinafsi na kujali masilahi ya taifa na wana nchi kwa ujmla hakuna mama atakaye kufa labada kwa bahati mbaya. kaka s.

Mija Shija Sayi said...

Hilo nalo neno @ Kaka S.

chib said...

Labda baada ya miaka 100 ya uhuru tutakuwa tumesonga mbele sana.