Tuesday, June 26, 2012

JE HAPA NI ILE NJOO TULE BASI.....AU?

Hata wanyama na ndege nao wana tabia kama BINADAMU...unafikiri hapa JOGOO ANASEMA NINI KWA HUYU KUKU JIKE?

14 comments:

Interestedtips said...

hahaha hapo anasema kula ushibe ila usisahau majukumu yako ya familia na watoto wana njaa

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmmh! bahati mbaya sijui lugha za wanyama, wadudu na ndege bali za wanadamu baadhi teh teh teh!

Yasinta Ngonyani said...

Ester! kama vile ulikuwepo mawazoni mwangu..Nami nadhani anasema hivyo...
Kaka Chacha...Hapa si kujua ni kuotea au pia unaweza kugeuza yaani hapa ni mume na mke...je unafikiri ingekuwaje?

Israel Saria said...

Ajiandaa kuomba unyumba......

tunu said...

Israel acha kunichekesha mie tehe tehe tehe

Aisha said...

Israel usinichekeshe ,lakini kwa mawazo yangu nafikiria anaomba unyumba.

ray njau said...

Duh,hapa ni kitendawili tega ukishindwa nipe mji na mji nakupa Songea!

Simon Kitururu said...

Wajanja Njiwa hasa katika maswala ya nipe kidogo nichangamshe damu!
:-(

sam mbogo said...

Kwa tulio wafugaji, hapa jogoo anamwita kuku jike aje ale chakula,halafu wakati kuku jike anakula chakula hicho ambacho jogoo kakigundua , nahiyo huwa ni njia ya kimahaba kwa jogoo kumpata kirahisi kuku jike.hapo bila kuchelewa wataanza kufukuzana na hatimaye kuku jike anapata chakulayake ya mchana.pia wakati jogoo anatega mtego wa kumnasa jike huwa anatoa mlio fulani ambao kwa hakika jike lazima ataingia mkenge. jogoo anambinu nzuri sana anapo taka kuvunja amri ya 6!. kaka s.

DarSlam said...

anasema "ngoja nitifuetifue nikuchambuli wadudu wengine wanang'ata mrembo wasijekukukwama bureee..! kokoko..ko ko...kokoliiiko!
u get me?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mie naona vyote njoo ule au you know what I mean kama ulivyoliweka. Maisha ndivyo yalivyo hata hivyo. Muhimu ni kuheshimiana na kuridhishana.

emuthree said...

Hii ni mfano halisi ya misha yetu,...kuwa upendo ni muhimu, kujaliana na kuwa karibu na mwenzako.
Kuku jogoo, utamuona, akipata kitu atamuita kuku jike kama vile kuku jike anavyowaita vifaranga...mfano wa upendo.
Siku hizi upendo ni `hapendwi mtu, kinachopendwa ni pesa....tutafika kweli.

Tupo pamoja ndugu wangu

ray njau said...

Wadau naona hapa somo sasa limekolea na mada imezuka kivingine kuwa kuku wana upendo kuliko binadamu.Wakati huku wanakufa njaa kutokana na ukosefu wa chakule kule upande wa pili maghala yanafurika kwa nafaka.

ray njau said...

"Wanakufa njaa kutokana na ukosefu wa chakula".