Thursday, June 21, 2012

ALHAMIS YA LEO TUANGALIE:- MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!

1. Hata kama mtu ni mwerevu, huwezi kuwadanganya watu wote kwa muda mrefu. Siku moja utagunduliwa, kwa sababu "siku za mwizi ni arobaini" au "habari za uwongo zina ncha saba.
2. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana budi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira.
3. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
4. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni
5. usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu. Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au maskini hachoki, akichoka keshapata.
7.Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
8. Si utu kwende kwa uliyempa zawadi na kumwambia akurudishi zawadi yako
9. wivu hangamiza familia nyingi ulimwenguli
Namba kumi naomba wewe uzaja. Ni kwamba kama nawe una msemo na basi karibu jumuika nami......

3 comments:

ray njau said...

Methali 1:1-33
=============================
1 Methali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, 2 ili mtu ajue hekima na nidhamu, na kutambua maneno ya uelewaji, 3 apokee nidhamu ambayo humpa mtu ufahamu, uadilifu na haki na unyoofu, 4 kuwapa werevu wale wasio na uzoefu, kumpa kijana ujuzi na uwezo wa kufikiri.

5 Mtu mwenye hekima atasikiliza na kupata mafundisho zaidi, naye mtu mwenye uelewaji ndiye anayepata mwongozo stadi, 6 ili kuelewa methali na mafumbo, maneno ya watu wenye hekima na vitendawili vyao.

7 Kumwogopa Yehova ndio mwanzo wa ujuzi. Wapumbavu wamedharau hekima na nidhamu.

8 Mwanangu, sikiliza nidhamu ya baba yako, wala usiiache sheria ya mama yako. 9 Kwa maana hizo ni shada lenye kuvutia kichwani pako na mkufu bora shingoni pako.

10 Mwanangu, watenda-dhambi wakijaribu kukushawishi, usikubali. 11 Wakizidi kusema: “Haya, njoo pamoja nasi. Na tuvizie ili kumwaga damu. Na tujifiche ili kuwashambulia, bila sababu, watu wasio na hatia. 12 Na tuwameze wakiwa hai kama Kaburi, naam, wakiwa wazima, kama wale wanaoshuka shimoni. 13 Na tupate namna zote za vitu vyenye thamani. Na tujaze nyara katika nyumba zetu. 14 Unapaswa kupiga kura yako katikati yetu. Nasi sote tuwe na mfuko mmoja tu”— 15 mwanangu, usiende njiani pamoja nao. Zuia mguu wako usiende katika barabara yao. 16 Maana miguu yao hukimbilia ubaya mtupu, nao huharakisha kwenda kumwaga damu. 17 Kwa maana wavu hutandikwa pasipo kusudi mbele ya macho ya kiumbe chochote chenye mabawa. 18 Basi wao wenyewe huwavizia ili kumwaga damu yao; hujificha ili wazishambulie nafsi zao. 19 Hayo ndiyo mapito ya kila mtu anayepata faida isiyo ya haki. Huiondoa nafsi yao walio nayo.

20 Hekima ya kweli huendelea kulia kwa sauti kubwa barabarani. Hutoa sauti yake katika viwanja vya watu wote. 21 Inaita penye mwisho wa upande wa juu wa barabara yenye kelele. Husema maneno yake katika mahali pa kuingilia malango ya jiji:

22 “Ninyi msio na uzoefu mtaendelea mpaka wakati gani kupenda kutokuwa na ujuzi? Nanyi wenye dhihaka mtaendelea mpaka wakati gani kujitakia dhihaka tupu? Nanyi wajinga mtaendelea mpaka wakati gani kuchukia ujuzi? 23 Geukeni mpate karipio langu. Ndipo mimi nitafanya roho yangu ibubujike juu yenu; nitawajulisha maneno yangu. 24 Kwa sababu nimewaita lakini mnaendelea kukataa. Nimenyoosha mkono wangu lakini hakuna yeyote anayetazama. 25 Nanyi mnazidi kupuuza mashauri yangu yote, wala hamkukubali karipio langu. 26 Mimi pia, kwa upande wangu, nitacheka taabu yenu wenyewe, na jambo mnalohofu litakapokuja nitafanya mzaha, 27 jambo mnalohofu litakapokuja kama dhoruba, na taabu yenu wenyewe itakapofika kama upepo wa dhoruba, na shida na nyakati ngumu zitakapowapata. 28 Wakati huo wataendelea kuniita, lakini sitaitika; wataendelea kunitafuta, lakini hawatanipata, 29 kwa sababu walichukia ujuzi, nao hawakuchagua kumwogopa Yehova. 30 Hawakukubali shauri langu; walipuuza makaripio yangu yote. 31 Basi watakula matunda ya njia yao, nao watashiba mashauri yao wenyewe. 32 Kwa maana uasi wa wasio na uzoefu utawaua wao, na kutojali kwa wajinga kutawaangamiza wao. 33 Kwa habari yake mtu anayenisikiliza, yeye atakaa salama wala hatasumbuliwa na hofu ya msiba.”

Yasinta Ngonyani said...

Amina kaka Ray! ubarikiwe sana kwa neno hili

ray njau said...

Methali 9:1-18

1 Hekima ya kweli imejenga nyumba yake; imechonga nguzo zake saba. 2 Imepanga kuchinja nyama zake; imechanganya divai yake; zaidi ya hayo, imepanga meza yake. 3 Imetuma watumishi wake wa kike, ili ipate kupaaza sauti juu ya vilele vya mji: 4 “Yeyote ambaye hana uzoefu, na ageuke aje hapa.” Amemwambia yeyote ambaye amepungukiwa moyoni: 5 “Njooni, mle mkate wangu na mshiriki kunywa divai ambayo nimechanganya. 6 Waacheni wasio na uzoefu mpate kuendelea kuishi, na mtembee moja kwa moja katika njia ya uelewaji.”

7 Anayemrekebisha mtu mwenye dhihaka anajipatia aibu yeye mwenyewe, naye anayemkaripia mwovu—mna kasoro ndani yake. 8 Usimkaripie mtu mwenye dhihaka, asije akakuchukia. Mpe karipio mtu mwenye hekima naye atakupenda. 9 Mpe mtu mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima. Mpe ujuzi mtu mwadilifu naye atazidi kujifunza.

10 Kumwogopa Yehova ndio mwanzo wa hekima, na kumjua aliye Mtakatifu Zaidi ni uelewaji. 11 Kwa maana nitafanya siku zako ziwe nyingi, nawe utaongezewa miaka ya uzima. 12 Ikiwa umekuwa na hekima, umekuwa na hekima kwa ajili yako mwenyewe; na ikiwa umefanya dhihaka, utaichukua, wewe peke yako.

13 Mwanamke mwenye ujinga ana msukosuko. Yeye ni mjinga kabisa wala hajapata kujua lolote. 14 Naye ameketi katika mwingilio wa nyumba yake, juu ya kiti, mahali palipoinuka pa mji, 15 apate kuwapaazia sauti wanaopita njiani, wanaoenda moja kwa moja katika mapito yao: 16 “Yeyote ambaye hana uzoefu, na ageuke aje hapa.” Naye amemwambia yeyote ambaye amepungukiwa moyoni: 17 “Maji ya kuibwa ni matamu, na mkate unaoliwa katika siri—huo ni wenye kupendeza.” 18 Lakini yeye hajapata kujua kwamba wale wasiojiweza katika kifo wamo humo, kwamba walioitwa naye wamo mahali pa chini pa Kaburi.