Mnajua pale shuleni kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali kama vile mapapai, machungwa, malimao, ndizi n.k. Na mimi ilikuwa kazi yangu kila baada ya shule nilirudi tena shuleni, nilikuwa mwizi wa malimao nilikuwa nakula sana malimao kwa siku nilikuwa nakula 10. Mama alikuwa analalamika sana. Kwani nilikuwa nakula na chumvi iliyochanganywa na pilipili. Nilikuwa siibi malimao tu chumvi pia.
Halafu magauni yangu na sketi zilikuwa na matobo sana, sababu nilikuwa nabebea malimao. Mmh! jamani Lundo sitasahau, yaani kujificha kwa kweli nilikuwa mwizi maalufu kwani sikushikwa. Ila sasa siwezi kula malimao zaidi ya nusu limao nimekinai kabisa.
LUNDO BAADA YA MIAKA ISHIRINI
Mmhh furaha, hisia pia raha vilinijia siku hii yaani mwaka jana 2007. Fikiria mwenyewe sehemu uliyozaliwa, sehemu ulianza darasa la kwanza halafu umeondoka na baada ya miaka 20 unarudi/tembelea tena.
Ila nilisikitika kidogo kwani sikuweza kujua ni nyumba gani nilizaliwa/ishi kulikuwa na mabadiliko mno. Ila cha kufurahisha zaidi ni kwamba nilionana na mjomba wangu ambaye sikumwona tangu 1985. Siku hii nilikuwa kama mtoto mdogo nilikimbia na kumrukia mjomba kwa jinsi nilivyokuwa na furaha. Mpaka machozi yalinitoka. Kwa vile mjomba anajua mimi napenda nini aliniandalia samaki What a joy. pia nilifurahi zaidi kujua alikumbuka jina langu la utani ambalo hata mwenyewe nilisahau. Mnataka kujua au? Okey ni (KANYANJA) kilugha kiswahili kanyasa. Sasa mnajua .
2 comments:
kanyanja ka mwana ka palochi. kamwana ka kuiba malimao
kama unayo kwako sema nije kuiba
Post a Comment