Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…
Mahusiano kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye shughuli zake au aanguke. Kwa nini? Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe.
Mke anapomkosoa mume, anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa anayo. Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi anavyojitathmini. Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima ataanza kuwa na uhusiano mmbaya na watu wengine kutokana na hukohuko kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwengi kwa mkewe. Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.
Baadhi ya makampuni huko Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji
wala mwenye kulalamika-lalamika humpa cheo mtumshi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini. Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na
mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.
.......................................................................................................................................................
Swali langu hapa je hii ni pale tu mwanamke anapomjali mume na ndio iwe hivi? Je? mwanamke astahili kujaliwa na kukubaliwa ili kuongeza kujiamini?..au ndo kusema mwanamke anajiamini sana kuliko mwanamume?..swali kutoka kwa KAPULYA...
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengine wafaidike na ELIMU hii.
Tuesday, February 11, 2014
Sunday, February 9, 2014
MAOMBI YA JUMAPILI YA LEO NI KAMA IFUATAVYO:- SHUKRANI!!
Mungu wetu tunakushukuru kwamba unatupenda. Yesu Kristo ingia ndani ya mioyo yetu na uchukue dhambi zetu, huzuni, maumivu na hali yetu ya kutamamauka. Tupe tumaini, twaomba tupe maisha mapya. Ahsante sana Bwana tumeamini mioyoni kila mmoja anayekuja kwako ataokoka na kuanza maisha yake upya. Twasema AHSANTE kutukubali leo . Tupe moyo mpya na maisha mapya Bwana katika jina la Yesu Kristo.
AMINA.
AMINA.
Friday, February 7, 2014
UJUMBE WA IJUMAA YA LEO KUTOKA KWA KIBARAZA CHA MAISHA NA MAFANIKIO NI KAMA UFUATAVYO!!!!
Bila ubishi wala maswali mengi katika maisha ya Taifa letu tunategemea sana uwepo wa wanawake.
NAWATAKIENI WOTE MWANZA MWEMA WA JUMA HILI MAANA LEO NI IJUMAA WENGI WANAANZA MAPUMZIKO BAADA YA KAZI YA JUMA NZIMA.

Thursday, February 6, 2014
HII KWA KWELI ITAKUWA PICHA YA WIKI...UGALI KWA NYAMA PANYA !!!MMMMHHH KAZI IPO!!!
Ni muda mrefu nimekuwa nikisikia ya kwamba nyama ya panya na nyoka ni tamu kama ya kuku. Na pia nimesikia katika habari ya kwamba baaada ya miaka wadudu wote watakuwa kitowoe kizuri sana kwa binaadamu. Swali moja kutoka kwa kijana wangu linaulizwa hivi:- Iweje tule panya wakati anatuletea magonjwa? Na je nyoka si adui yetu na pia ana sumu?
Wednesday, February 5, 2014
INAHUZUNISHA LAKINI KUNA FUNDISHO KUU KWA WOTE!!
Katika mizunguko yako nimekutana na habari hii ambayo ni kusikitisha lakini pia ni kumpa mtu mafunzo mazuri sana. Ungana nami ….
---------------------------------------------------------------------------------------
Ndugu zangu wapendwa!
Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote. “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha ana umizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake. Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauté ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu Sali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu?. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa Jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali, kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwaMary. Kwa kweli nilimdharau mke wangu! Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande. Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu. Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika nakuwa jambo la hakika zaidi. Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Mary. Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali Kabila nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa
kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwatatizo kwangu,nilikubali mango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu. Nilimsimulia Mary kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana nakupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba. Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya utur aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mkewangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe!Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi. Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi. Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... Mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mkewangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono Wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia Mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka. Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu nakumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua....nikapanda ngazi. Mary alifungua mango nikamwambia, ‘Samahani, Mary, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’.Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu
sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mkewangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu nakuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kilo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu Kuba usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani. Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema. Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema….Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenu ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao Mungu awabariki na awe nanyi nyote mliosoma nakujifunza hapaNAWATAKIENI JUMATANO NJEMA SANA…

Tuesday, February 4, 2014
USIJE UKADHANI NI MJI KASORO BAHARI:- NI MOROGORO YETU YA SONGEA/PERAMIHO!!
Ndiyo:- najua wengi mtashangaa, lakini msishangae sana. Tulio wengi tunafahamu Morogoro hii kutokana na HOSPITAL maalumu/MAARUFU ya wagonjwa wa ukoma. Si mbali kutoka Peramiho kama sikosei ni km 5-8 hivi.
Monday, February 3, 2014
MSAADA WA VITENDAWILI NA MAANA ZAKE!!
Nimetumiwa ujumbe huu lakini kwa bahati mbaya hivi vitandawili kwangu vimekuwa vigumu kidogo kwa hiyo naomba ndugu zangu tusaidiane maana palipona wengi hapaharibiki kitu..Natunguliza shukrani zangu za dhati kwenu. Na ujumbe wenyewe unasema hivi:- karibuni!!
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Dada Yasinta, habari za leo? Samahani naomba msaada wako kwa vitendawili vifuatavyo:
1) Wanastarehe darini.
2) Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa baba yangu.
3) Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa.
4) Ini la ng'ombe huliwa hata na walio mbali.
5) Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja.
6) Mvua kidogo ng'ombe kaoga kichwa.
7) Njoo hapa nije hapo.
8) Msitu ambao haulii hondohondo.
9) Aliwa, yuala, ala, aliwa.
10) Ajenga ingawa hana mikono.
JUMATATU IWE NJEMA KWA WOTE!

Saturday, February 1, 2014
HUYU NDIYE MWANAMTINDO ATAKAYEFUNGUA MWEZI HUU WA PILI/FEBRUARI
Ebu angalia hapa alivyopendeza nimependa ile mbaya. Rangi zote zimekaa safi sana.
Hapa akaona abadili mtindo amekaa na kofia nyingine hakika nimependa mno vazi hili. Na huyu binti si mwingine tena bali ni shangazi yangu Paulina Mubelwa. Binti Bandio Mubelwa /Mzee wa Changamoto.JUMAMOSI NJEMA.
Friday, January 31, 2014
MWISHO WA MWEZI JANUARI TUUMALIZE ZILIPENDWA HATA KAMA SIELEWI ILA MZIKI UNACKEZEKA...KARIBUNI!!!!!!.....
AU TU LABDA TUSIKILIZE NA HUU WIMBO WA MONICA....
Mara nyingi ukiwa sambamba sana na walezi huwa unakumbuka vitu vingi sana.....nadhani mmenielewa...haya tuendelee kuselebuka ...tuonane mwezi ujao. Oh! Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda salama wote tulioumaliza mwezi huu na pia napenda kuwaombea wote waliotutangulia na pia wagonjwa. Na pole nyingi kwa ndugu zetu wa Morogoro /Kilosa mji kasoro bahari, Mungu awape nguvu. IJUMAA NJEMA.
Thursday, January 30, 2014
KAMA KAWAIDA NI ALHAMIS LEO...TWENDE MPAKA MBUGA YETU YA RUAHA ILIYOPO KUSINI MWA TANZANIA!!!!!!!
Mbuga ya Ruaha :- Mbuga hii ni nzuri na ndogo ambayo haijulikani sana kana SERENGETI au NGORONGORO. Ipo kusini wa Tanzania, kama uonavyo kuna simba, tembo, nyati, twiga na wanyama wengine wengi wa pori ambao wanaipendezesha Mbuga hii kwa ukamilifu mazingira yetu ya Afrika/Tanzani....ALHAMIS IJIYO NA MBUGA MPYA...
Wednesday, January 29, 2014
NIMEPENDA VITU/FANICHA/SAMANI HIVI/HIZI VYA /ZA ASILI VINAVUTIA NA NI IMARA..EBU ANGALIA
Kama kuna mtu anafahamu wapi vinapatikana nitashukuru kupata taarifa. Nilisikia vinapatikana Mfaranyaki/Songea kwetu nimeulizia sijafanikiwa.....PAMOJA DAIMA.JUMATANO NJEMA PIA JIONI NIJEMA.
Tuesday, January 28, 2014
JUMANNE YA LEO TUANGALIE TANZANIA YETU...KUHUSU MIUNDOMBINU TANZANIA
http://www.bbc.co.uk/swahili/medianuai/2014/01/140122_tz_miundomsingi.shtml
Ni kweli kabisa barabara ni msingi wa maendeleo..Kwa hiyo kama wote tutafuatilia/tutajituma basi tutafanikisha JUMANNE NJEMA!!

Monday, January 27, 2014
JUMATATU HII YA MWISHO KWA MWEZI HUU WA KWANZA TUIANZE NA KUMALIZA NA BAADHI MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!
1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi/walezi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
2. Si utu kwenda kwa uliyempa zawadi na kumwambia akarudishie zawadi yako.
3. Usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu.....Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
4. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana busi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira yake.
5. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au, maskini hachoki, akichoka ujue amepata.
7. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni.
8. Wivu huangamiza familia nyingi ulimwenguni.
KAMA NAWE UNA NYINGINE KARIBU KUUNGANA NAMI...JUMATATU IWE NJEMA SANA!!!

Saturday, January 25, 2014
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA KWA KIPANDE HILI:- NASONGA MBELE....
JUMAMOSI NJEMA SANA....NA TUKUMBUKE YA KWAMBA SISI SOTE NI NDUGU NA WATOTO WA BABA MMOJA!!!!!
Thursday, January 23, 2014
LEO TWENDE KUTEMBELEA MBUGA YA NGORONGORO...KARIBU TANZANIA YETU
Kama nilivyosema ALHAMIS ya wiki iliyopita nimeanzisha kipindi kipya kila Alhamis tutakuwa karibu na Mbuga moja kutoka nyumbani TANZANIA na leo tupo NGORONGORO .....TUONANE TENA ALHAMIS IJAYO KATIKA MBUGA NYINGINE.
Wednesday, January 22, 2014
JUMATANO YA LEO TUANGALIE:- JAMII YA KI-SUKUMA!!!
Nimefanya utafiti kidogo kuhusu ndugu zetu wasukuma..nimefanya hivi kwa vile nilipokuwa mdogo nilisimuliwa mambo mengi sana kuhusu wasukuma na babu yangu mzaa mama pia bibi ..ni Kwamba babu yangu alikuwa fundi mwashi miaka ya hiyooooo......Na hivi ndivyo nilivyopata kuhusu Wasukuma/wanyamwezi...Karibu.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
KWANZA TUANGALIE MAANA YA NENO WASUKUMA:-
Wasukuma ni mkusanyiko wa makundi madodomadogo kutoka maeneo jirani, na kwamba kundi kubwa zaidi limetoka kusini wa eneo hilo la mkoa wa Mwanza. Jina hili limetokana na neno SUKUMA maana yake kwa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi KASKAZINI, yaani moja wapo wa pande nne za dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma huwaita walio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa KASKAZINI. Na wasukuma huwaita "Bhadakama" yaani watu wa KUSINI. Siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaitwa WABANTU. Kundi hili mara zote limetambulika kwa lugha wanayozungumza ya KIBANTU. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatilia lugha wanazozungumza.
Karibu kujadili nami kama kuna kitu nimekikosa au sahau......JUMATANO IWE NJEMA...

Tuesday, January 21, 2014
MAISHA:- USAFIRI/USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BAISKELI...HUPUNGUZA GHARAMA NA PIA MTUMIAJI HUWA NA AFYA NJEMA PIA NI SAFI KWA MAZINGIRA!!!
Katika maisha usikaa tu na kungoja ..lazima kujishughulisha. Hapa kijana yupo safirini kuelekea soko la kuuza ulazi ila kujipatia kitoweo/chakula. Baiskel zinasaidia sana miaka hii tafauti na miaka tuliokulia wengine kila kitu ilikuwa na kichwani....
Na hapa anasafirisha chakula, Ndizi hizo..
Naye huyu anaelekea sokonoi kuuza mananasi yake
Na hapa ni baiskel yangu. Kwa kweli usafiri wa baiskel ni mzuri sana na wa haraka huhitaji kusubiri foleni. SWALI:- Umegendua nini kati ya baiskel hizi nne?....Nawatakia JUMANNE NJEMA SANA WOTE
Sunday, January 19, 2014
MAOMBI YANGU YA JUMAPILI YA LEO NI KAMA YAFUATAYO.....
Mwenyezi Mungu nakuomba ulisikie ombi langu. Nakubali kwamba mimi ni mtenda dhambi. Na ninaamini ulimtuma Yesu Kristo kuniokoa, ninamkubali Yesu kama Bwana na Mkombozi wangu. Nisamehe dhambi zangu unifanye safi. Nipe nguvu za kutembea katika njia zake. Naomba hivi kwa jina la Yesu Kristo. AMINA...,,,KWA MAOMBI YANGU HAYA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII IWE YA UPENDO NA FURAHA. jUMAPILI NJEMA KWA WOTE.
Saturday, January 18, 2014
HAYA NI MAPISHI YA KAPULYA JIONI HII YA LEO..KITIMOTO NDANI YA UYOGA......
Ni kitimoto, uyoga niliochuma mwezi wa kumi, cream kidogo, nyanya , chumvi na maji kidogo na viungo vingine....
Na baada ya muda chakula kilikuwa tayari kuliwa na hapa ni shani yangu, ikiwa imeshehena na wali, kitimoto,uyoga kama hapo juu na sallad tamuuuu ambayo ni:- nyanya, tango, carroti, majani ya salladi na chizi(fetaost) na kitunguu kwa mbaliiii...
Nikapandishia na glasi ya maji kama uonavyo...Ila usisite kuja kuna chakula bado karibu sana tena sana kujumuika nasi. JIONI NJEMA.

JUMAMOSI NA MAPUNZIKO MEMA KWA WOTE.
Nadhani wengi tunakumbuka ilivyokuwa enzi za mababu zetu...na pia miaka ya 1980 mpka 1990..Kanisa moja, shule moja rais mmoja Chama kimoja na pia kula na kunywa pamoja na sahani moja na kikombe/robo/kichonjo kimoja. Lakini sasa mambo haya hakuna kabisa inasikitisha sana. JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI...PIA KUMBUKENI POMBE SI MAJI....:-) TARATIBU
Thursday, January 16, 2014
SERENGETI/TANZANIA
KARIBUNI TANZANIA YETU...KILA ALHAMIS TUTAKUWA TUKITEMBELEA MBUGA MBALIMBALI TANZANIA...TUONANE TENA ALHAMIS IJAYO...
Wednesday, January 15, 2014
WANAWAKE NA HISIA ZA USALITI: ZIJUE DALILI ZAKE!!
Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………
Kutoka kwenu mara kwa mara kwenda kupata chakula cha mchana, unagundua kwamba huyu bwana ni mtu mwenye kiwango cha juu ya usikivu, katika mazungumzo yenu anaonekana sana kwamba ni mwelewa na mwenye subira. Hana papara katika kuzungumza na mara nyingi huwa ni msikilizaji. Huyu unaweza kumwita rafiki ingawa ni wa jinsia tofauti, (Sidhani kama ni dhambi kuwa na rafiki wa jinsia tofauti……!) Kuna kitu wenzetu wazungu wanakiita Emotional infidelity, kwa tafsiri yangu naweza kusema ni hisia za usaliti katika mapenzi. Maana yake ni kwamba unaruhusu mtu mwingine wa jinsi tofauti azibe pengo la hisia ambalo lingetakiwa lizibwe na mpenzi wako au mume wako. Kama inavyofahamika kwamba wanawake ni viumbe wa hisia, wanapenda sana kusikilizwa, na wanapenda kuona wapenzi wao au waume wao wanawasikiliza. Inapotokea hitaji hilo halitekelezwi na mpenzi au mume wake, basi ni rahisi sana atakapotokea mtu mwingine ambaye bila kujua akamudu kuziba pengo hilo kuvutiwa naye na kuhitaji kuwa naye karibu mara kwa mara.
Hapa chini nitazitaja dalili ambazo zitakuonyesha kwamba ukaribu wako na huyo rafiki utakupelekea kuisaliti ndoa yako:
1. Unatamani sana kumuona ukiwa na shauku kubwa ya kuwa naye karibuna kutumia muda mwingi kuwa naye
2. Unajikuta ukichagua mavazi na kujikagua sana ukijiuliza jinsiatakavyo vutiwa na mavazi yako pale atakapokuona
3. Unapokuwa naye unajikuta ukimweleza matatizo ya mahusiano yako na mpenzi wako au mumeo
4. Unajikuta ukimgusa gusa wakati mkiongea au kufanya naye utani unaoweza kupeleka ujumbe tofauti kwake kwamba labda umevutiwa naye kimapenzi
5. Unawsiliana naye kwanza kabla ya kuwasiliana na mpenzi wako au mumeo pale unapokabiliwa na jambo lolote lenye kutatiza na linalohitaji msaada wa haraka au ushauri
6. Unajikuta ukiwaza jinsi gani ungekuwa na amani iwapo ungekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi au ndoa
7. Inawezekana ukawa unamzuingumzia sana kwa mwenzi wako au kwa marafiki zako, au inawezekana ukawa humzungumzii kabisaaa na kuficha urafiki wenu.
8. Unajitahidi sana kuficha urafiki wenu na kutomzunguimzia rafiki huyo kwa mwenzi wako kwa sababu unajua kwamba jambo hilo linaweza kukuletea balaa.
Kwa ujumla unapojikuta umempata rafiki wa jinsia tofauti na yako halafu ukahisi kulipukwa na moyo juu yake zikiwemo dalili nilizozitaja hapo juu, basi ujue uhusiano wako na mume au mpenzi wako uko mashakani. Usipokuwa makini utamsaliti.
Habari/mada hii nimetumiwa na mkereketwa/msomaji wa Maisha na Mafanikio kwa kutaka tu mimi nisome lakini mimi nimeona ina mafundisho ndani yake nikaona ni bora niiweke hapa ili wengi wafaidike na ELIMU hii.

Tuesday, January 14, 2014
NIMEOTA NDOTO KUWA NIPO LUNDO NA KINGOLI KWENYE SHAMBA LA MPUNGA NALINDA ILI NDEGE WASILE NA PIA NAVUNA MPUNGA...
Hapa ni mwezi wa nne mpunga huwa unakuwa umekomaa kiasi hiki kwa hiyo walaji ni wengi kama vile ndege...Kwa hiyo kwa kuokoa mpunga ni lazima kila siku kwenda shambani kulinda/kufukuzia ndege..Duh nimefanya kazi hii ...mpaka sasa naota ndoto--Maisha ya zamani kweli ni dhahabu.
Hapa mpunga umeshakauka ni mwezi wa sita na ni wakati wa kuvuna sasa kula ubwabwa/wali...Sijui kati ya hawa nipo wapi?..Mnaniona au?...Kuvuna ni raha zaidi kuliko kulinda ndege:-)KILA LA KHERI NA LOLOTE UFANYALO:-)

Sunday, January 12, 2014
JUMAPILI YA LEO HALI YA HEWA ILIKUWA HIVI, KWANGU MIMI NAWEZA NIKASEMA HALI YA HEWA IMECHAFUKA.....BARIDI -10C...HAPA BAADHI YA PICHA NILINASA LEO
Kuanzia jana asubuhi mpaka leo bado theluji inaanguka tu ebu angalia hapa ukiangalia kwa makini sana kushoto kwako ni lile enoa ambalo tumezoea kuiona bustani ya Kapulya lakini sasa mmmhhh! haiwezekani kabisa ....hata hivyo ni lazima kutoka nje ingawa ni -10C huko nje....angalia hapa ....
...hapa tupo nje ni siku ya wazazi na watoto wao kuwa nje kwa vile ni siku maalumu kwa darasa la binti yetu. Ni kwamba wamepata na wageni kutoka Colombia kutokana na darasa lake kusoma lugha ya spanish wao walikuwa kule Colombia mwaka jana na sasa waColombia wamefika hapa juzi. Kwa hiyo wazazi na watoto ni jambo la muhimu kuwapokea wageni na kuwaonyesha nini kufanya...ila duh! wameshangaa kwani ni baradi mno ...hata hivyo wanafurahia hali hii.
Mama maisha na Mafanikio alivovalia tayari kwa kupambana na baridi ya leo lakini, wee bwana haikuwa joto vidole vilikufa ganzi kabisa hata kama ningeenda kwa daktari na kuchomwa sindano nisingesikia maumivu...Si ajabu kuonekana kama tembo maana mtu unajitahidi kuvaa nguo nzito ila kuepukana na baridi.....Hiii ndio JUMAPILI YANGU YA LEO..PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE.
Thursday, January 9, 2014
UNAKUMBUKA HABARI/HADITH HII KITABU CHA DARASA LA SITA:- MVUMILIVU HULA MBIVU? KUMBUKUMBU!!
Hapo zamani za kale Sungura na Mbwa Mwitu walioa mabinti wa jamaa mmoja. Mbwa Mwitu alimwoa kifungua mimba na Sungura kitinda mimba. Mbwa Mwitu alikuwa mvivu sana tena mlafi. Sungura alikuwa hodari wa kutega ndege. Kila siku nyumbani kwa Sungura kulikuwa hakukosekani kitoweo kizuri. Mbwa Mwitu akaanza kumwonea wivu Sungua kwa sababu alipendwa na watu wote wote kijijini.
Mwaka fulani njaa ilitokea katika kijiji chao. Mbwa Mwitu na Sungura wakamwendea mkwe wao kuomba ardhi ya kulima. Akawaonyesha mwitu mzuri wenye rutuba nyingi. Sungura hakupenda kufyeka msitu pamoja na Mbwa mwitu. Alikataa kwa sababu aliuelewa sana uvivu wa Mbwa Mwitu.
Kila siku asubuhi Mbwa Mwitu alipokwisha pata kifungua kinywa alikwenda shambani. Alipofika huko alikata mti mmoja, miwili au mitatu, kisha akakaa chini ya mti. Kwenye mti kulikuwa na mtambazi uliotambaa juu na kushikilia matawi imara kabisa. Mbwa Mwitu alitengeza pembea nzuri sana juu ya mtambazi huo. Ikawa kila afikapo shambani kukata miti miwili, mitatu, kisha hurukia pembea yake akijiningíniza.
Kila siku Mbwa Mwitu alirejea nyumbani mapema na kufanya fitina kubwa nyumbani kwa Sungura. Alimwambia shemeji yake kwamba Sungura hafanyi kazi yo yote ya kutayarisha shamba. Kazi anayoifanya ni kutege ndege tu. Kwa kuwa Sungura alikuwa hodari, kila siku alileta ndege aliowanasa kwa mitego yake. Jambo hili lilimfanya mke wa Sungura aamini maneno ya Mbwa Mwitu. Mke wa Sungura alipoona hayo, ugomvi ukazuka kati yake na mumewe. Ugomvi huu ukaendelea siku baada ya siku. Mbwa Mwitu alikuwa ibilisi mbaya sana. Sungura alijua haya yote yalitokana na fitina ya Mbwa mwitu. Hakusema neno. Alivumilia kwa sababu alifahamu kuwa njia ya mwongo ni fupi.
Majira ya kupanda yalipowadia Mbwa Mwitu alimwendea tena mkwewe kuomba aina mbalimbali za mbegu akapande shambani mwake. Akapewa. Mbwa Mwitu alipokwenda shambani, alichukua kigae. Akakoka moto, kisha akakaanga zile mbegu kwenye kigae, akala akashiba , halafu akalala fofofo. Mbegu zilizobaki akaziweka akiba mpaka kesho yake. Asubuhi ya siku iliyofuata aliendelea na mambo yale yale. Kama waswahili wasemavyo, "Chovya chovya humaliza buyu la asali", hivyo Mbwa Mwitu alimaliza mbegu zote.
Sungura hakwenda kwa mkwewe kuomba mbegu. Hii ilimfanya Mbwa Mwitu azidi kutia fitina, hata Sungura akawa anachukiwa sana. Hata hivyo akaendalea kuvumilia. Baada ya kununua mbegu za kila namna kwa fedha alizojiwekea akiba, Sungura alikwenda shambani mwake akapanda. Punde si punde, mvua kubwa ikanyesha na mbegu zote zikaota vizuri sana.
Wakati wa kupalilia ulipotimia, Mbwa Mwitu akaendelea na mchezo wake ule ule wa pembea. Lakini Sungura alifanya bidii mpaka shamba lake likawa safi kabisa. Alifanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa, akayafuata mashauri ya wataalamu wa kilimo. Juhudi yako pamoja na maarifa ndivyo vilivyokuwa msingi wa kulipata shamba kubwa lenye mimea mizuri.
Mbwa Mwitu alikwenda kisirisiri kuangalia shamba la Sungura. Uzuri wake ulimshtua sana, naye akazidi kumwonea wivu. Alikata shauri kuliharibu. Akakusanya majani makavu na kueneza katika shamba ya Sungura, ili ayatie moto na kuliunguza shamba. Lakini kwa kudura za Mungu; Sungura aliwahi kugundua hila hiyo. Mbwa mwitu alipotaka kulichoma moto, Sungura aliwahi mapema shambani mwake. Mbwa Mwitu akashindwa kuliharibu shamba la Sungura.
Mbwa mwitu hakuchoka kumfanyia Sungura hila. Baada ya miezi kadhaa alipeleleza habari za shamba la Sungura akafahamu kuwa mazao yalikuwa tayari kuvunwa. Akakusudia kuyaiba mazao ya Sungura. Alijidai kwamba shamba lile lilikuwa lake. Akawaomba mkwe na jamaa wajitayarishe kwenda shambani kuvuna, lakini Sungura akazipata habari hizo.
Kesho yake asubuhi na mapema, Sungura akawahi shambani mwake akiwa na jamaa. Mbwa Mwitu alipogundua kwamba Sungura amewahi, akalazimika kuwapeleka wale aliokuwa nao shambani kwake. Walipowasili mahali Mbwa Mwitu alipopaita shamba lake, hawakuona dalili y yote ya mazao. Mkwe wake alihamaki, akamsaili kwa nini hakukuwa na mazao. Mbwa Mwitu alifedheheka akashindwa kujibu kwa aibu. Karibu na shamba chini ya mti mkubwa, wakaona mahali alipokaangia mbegu. Waligundua maganda ya karanga na mpunga yametapakaa huku na huko. Mkwe wa Mbwa Mwitu na jamaa wakarudi nyumbani wamekasirika sana.
Jioni ileile, Sungura alimwendea mkwe wake akamweleze kwamba angefurahi sana kama yeye pamoja na jamaa wangefika kuliona shamba lake. Mkwewe alikataa shauri hili. Akaeleza jinsi alivyotendewa na Mbwa Mwitu. Sungura akambembeleza sana mkwewe mwishowe akakubali.
Waliondoka asubuhi na mapema kwenda kuliona shamba la Sungura. Walipofika shambani wakaona mazao mengi yaliyostawi vizuri. Sungura akamweleza kwamba hilo ndilo shamba lake. Akawaomba waingie shambani kuvuna. Wote waliofika walifurahi sana. Zaidi ya hayo walishangaa jinsi Sungura alivyokuwa mvumilivu kwa fitina za Mbwa Mwitu. Mkwe wa Sungura akaona ni kweli kwamba matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno. Mbwa Mwitu alikuwa amesema maneno mengi kujisifu na kumfitini Sungura lakini hakuna alilokuwa ametenda.
Jioni ile mkwa wao aliwaita Sungura, Mbwa Mwitu na jamaa wote, akasema, "Leo tumepata fundisho kubwa kwa vijana hawa wawili, Sungura na Mbwa Mwitu. Kwa juhudi na uvumilivu, Sungura amejipatia chakula cha kutosha. Kwa ajili ya fitina, Mbwa Mwitu hakuambulia cho chote. Nataka wote mjifunze kuwa "Juhudi ni Shina la Maendeleo," na ya kuwa kwetu tunayo ahadi isemayo " Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko," Kwa hiyo anamwonya Mbwa Mwitu aache fitina, uchochezi na uvivu. Badala yake afanye kazi ili afaidi matunda ya jasho lake."
Tangu siku ile Mbwa Mwitu alianza kujirekebisha. Akashirikiana na wanakijiji wenzake kuendeleza kijiji chao. Kutokana na hadithi hii twakumbuka maneno ya wahenga wetu yasemayo "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu."
UJUMBE:- Hii hutokea mara nyingi sana ..Tuache uvuvi, fitina na tufanye kazi ili kuendelea..Akina Sungura wapo wengi sana katika dunia hii.

Subscribe to:
Posts (Atom)