Thursday, January 23, 2014

LEO TWENDE KUTEMBELEA MBUGA YA NGORONGORO...KARIBU TANZANIA YETU


Kama nilivyosema ALHAMIS ya wiki iliyopita nimeanzisha kipindi kipya kila Alhamis tutakuwa karibu na Mbuga moja kutoka nyumbani TANZANIA na leo tupo NGORONGORO .....TUONANE TENA ALHAMIS IJAYO  KATIKA MBUGA NYINGINE.

5 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wenzio tulishakwenda na kitabu cha watoto cha safari yetu kinakuja. Kinaitwa Safari ya Mbuga za Wanyama.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera mwal. He naweza kukipata hicho kitabu...nami nijinome?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kikitoka bila shaka utakuwa wa kwanza kutumiwa tena kikiwa na saini zetu. Ni kitabu kizuri hasa kwa wazazi wanaoishi nje. Tumefanya hivyo baada ya kuona watoto wetu wanapoteza kiswahili. Hawa waliozaliwa huku ndiyo usiseme. Akikwambia karibu anasema KARAIBU. Tuligundua kuwa itakuwa aibu siku moja tukirejea nyumbani hivyo tukaamua kutunga kitabu kinachoweza kuwavutia watoto. Tunangoja kusikia mchapishaji atakiingiza mitamboni lini.

Yasinta Ngonyani said...

Nitafuhi kwa kweli...natanguliza shukrani zangu kwenu. ...nitakutafuta kwa maswali zaidi...kapulya.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hamna neon. Kama nitaweza kuyajibu nitayajibu na nikichemsha nitakwambia. Tuombe uzima.