Nachotaka kusema ni kwamba watoto wa siku hizi hawawezi kazi kama hizi, yaani kuchota maji, Kutwanga, kupika chakula wala hata kuwaangalia wadogo zao wazazi wawapo shambani. Yaani najiona kama ni mimi huyo mwenye ndoo ya kijani. Kizazi cha zamani/enzi hizo watoto walikuwa wakakamavu na wenye afya njema, ila watoto wa kizazi cha sasa ni walegevu mno
2 comments:
Hiyo Dada yangu ndiyo hali halisi ya Mwafrika,na tamaduni zake,lakini hali hiyo ya watoto kubeba vitu ,kuni,maji na vitu vingine vijijini bado hali hiyo ipo hadi leo.
Kasheshe ipo Mijini,watoto watwike ndoo kichwani mbona haiwezekani. wanaona kama wanaonewa au jamii itawacheka ukiongeza na utanda wazi basi tumishiana.
Nashukuru kama utaendelea kuwaelimisha na kuwa kumbusha wajibu wao.na wapi walikotoka Baba na Babu zao. Chenjelai.
Ni kweli kabisa watoto wa mjini wataona wanaonewa sio kutwika ka ndoo ya maji tu hata kupika nk! Ama kweli chenjelai :-)
Post a Comment