Kutokea kwa binadamu ulimwenguni ilikuwa hatua kubwa mpya ya kwenda mbele, badiliko kubwa ajabu. Sasa siyo nguvu na uhai tu vilivyokuweko bali kulikuwa na uwezo wa kufikiri pia. Binadamu alikuwa na akili. Katika binadamu uhai uliweza kujitambua wenyewe kuwa unaishi.
Katika hatua hii Mungu alikamilisha kazi yake ya kuumba. Kwa milioni nyingi za miaka Mungu alikuwa akiugawia ulimwengu nguvu yake, akiushirikisha katika uhai wake. Sasa kumbe, ameushirikisha katika uwezo wa akili yake, uwezo wa kujitambua yeye mwenyewe. Na binadamu pia amefanywa kuweza kujitambua yeye mwenyewe, na kumjua Mungu.
Chanzo, kitabu:- Njia yetu kwa mapendo na ndoa.
No comments:
Post a Comment