Mama mjasiriamali tayari hapa kumekucha na kuwajibika ndiyo kama kawaida...na kama kawaida mara nyingi watoto wa kike hujifunza karibu kila kitu kupitia mama. Basi hapa tunaona binti huyu hayupo nyuma naye yupo mbele katika kujifunza maisha...hapa unadhani wanatoka kuuza au wanakwenda?
9 comments:
Kweli ni muhimu kuwajibika, lkn je hiyo siku ni ya shule, maana hapo kuna maswali mengi,...hawa yaonyesha wanakwenda
em-three! umenena haswa bila kuwajibika hakuna kitoweo..Nategemea si siku ya shule au keshaenda shule au ataenda baadaye..kama wanakwenda basi akishamaliza kuuza ataenda shule..
au ni jumamosi au jumapili, ndo wanaenda gengeni kuuza, wanawake tunajituma mnooooooo kwakweli
Thamani Ya “Chombo Dhaifu Zaidi”
================================
‘ENYI waume, endeleeni kukaa na [wake zenu] kulingana na ujuzi,’ akaandika mtume Petro, “mkiwapa heshima kama chombo dhaifu zaidi, yaani, mwanamke.”(1Petro 3:7) Je, Andiko hili linalomtaja mwanamke kuwa “chombo dhaifu zaidi” linawadharau wanawake kwa njia yoyote ile? Hebu tuone mwandishi huyo aliyeongozwa kwa roho ya Mungu alimaanisha nini.
Neno la Kigiriki linalotafsiriwa “heshima” humaanisha “bei, thamani, . . . staha.” Kwa hiyo, mume Mkristo anapaswa kumtendea mke wake kwa wororo, na kumjali sana kama chombo dhaifu chenye thamani. Kwa hiyo, wanawake hawadharauliwi kwa njia yoyote.
Kwa mfano, fikiria taa yenye umbo la yungiyungi iliyotengenezwa na msanii aitwaye Tiffany. Taa hiyo maridadi sana inaweza kuonwa kuwa chombo dhaifu. Je, thamani ya taa hiyo inapungua kwa sababu ya hali yake? Sivyo hata kidogo! Mnamo mwaka wa 1997, taa ya kale zaidi ya Tiffany ilipigwa bei mnadani kwa dola milioni 2.8 za Marekani! Umbo lake tata halikupunguza thamani yake, badala yake liliongeza thamani yake.
Vivyo hivyo, kumpa mwanamke heshima kama chombo dhaifu zaidi hakupunguzi thamani yake wala kumdharau. Mume anayeishi na mke wake “kulingana na ujuzi” anazingatia uwezo wake na udhaifu wake, mambo anayopenda na yale asiyopenda, maoni na hisia zake. Mume mwenye kujali hutambua na kuheshimu tofauti za utu kati yake na mke wake. Humjali mke wake ‘kusudi sala zake zisizuiwe.’(1Petro 3:7)
Mume anayeshindwa kuheshimu sifa nzuri za kike za mke wake anahatarisha uhusiano wake na Mungu. Ni wazi kwamba Neno la Mungu haliwadharau wanawake. Badala yake, linawastahi na kuwaheshimu.
Wanawake na Maendeleo.......Asante da'Kadala.
Kaka Asante kwa maoni yako. Nabarikiwa sana na maoni yako yanayoozwa na Neno la Mungu.
Bado napata shida na huku kujifunza kwa kwa huyu dogo, ile style aliyovaa nashindwa kujua kama ni Kadoda au Kadala. Shida yangu ni hii, katika umri huo ukichanganya Hisabati, Sayansi, Maarifa ya Jamii, n.k pamoja na mkao wa gengeni wa kuuza vitumbua na maandazi, mwisho wa siku kuna elimu kweli ni kuishia tu kuhudhuria darasani? Kwa mtindo huo hata homework hakuna. Atafanya saa ngapi. Kweli ni muhimu kuwafundisha maisha yanavyoenda, lakini namna ya kufundisha nalo ni jambo muhimu la kuzingatia.
Da´Ester ! inawezekana labda ni jumamosi au jumapili..
Kaka Ray! Ahsante sana kwa darasa mara zote ni raha kusoma neno.
Kachiki!Haswa wanawake na maendelea hakuna kusubiri kupewa ..
Kaka Mhagama! mimi nionavyo ni Kadala huyo. Na ulichosema ni kweli maana hapo akili itakuwa kuuza mabumunda, vimbama nk...ila mweeh matu tumetoka mbali.
Asante Sana Kaka Ray Umenifungua sana kuhusina na Chombo dhahifu mimi nilikuwa natafsiri tofauti kabisa.
Na kila kiumbe kilicho mbinguni na juu ya dunia na chini ya dunia na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani ya hivyo, nikasikia vikisema: “Kwake Yule anayeketi juu ya kile kiti cha ufalme na kwa Mwana-Kondoo kuwe na baraka na heshima na utukufu na nguvu milele na milele.”Na wale viumbe hai wanne wakasema: “Amina!” na wale wazee wakaanguka chini na kuabudu._Ufunuo 5;13,14.
Post a Comment