Tuesday, October 30, 2012

MIKUMI NATIONAL PARK/MBUGA YA HIFADHI YA WANYAMA MIKUMI 2011 MWEZI WA SITA!!!

 Jamani subirini kwanza sisi tupite...Nyani/tumbili hao walivyojua kuziba njia
 Hakuna mnyama mzuri kama twiga...habari jamani!!!
Tulipata bahati ya kumwona Nyati  pia mnyama asemekanaye mwenye hasira kuliko wote..Kwa mbele ni hawa Funo hawa hukosi kuwaona ukifika /pita Mikumi

7 comments:

ray njau said...

@Yasinta;
Asante sana maelezo ya mbuga za wanyama!
==================================
Twiga hupenda kukaa na twiga wenzake, na wanaishi katika makundi yaliyo mbalimbali yenye wanyama 2 hadi 50. Twiga wa kike hubeba mimba kwa muda wa siku 420 hadi 468, kisha huzaa ndama mwenye kimo cha meta mbili. Wakati anapozaliwa, ndama huanguka kwa kichwa kwa umbali wa meta mbili hadi chini! Lakini baada ya dakika 15 mtoto, asiye na jeraha, anasimama kwa miguu isiyo imara, akiwa tayari kunyonya. Baada ya majuma mawili au matatu, ndama huyo aanza kutafuna-tafuna matawi machanga ya mkakaya na muda si muda hupata nguvu ya kutosha kwenda kwa mwendo sawa na mama yake.
Twiga mchanga afanana kabisa na wazazi wake. Ijapokuwa yeye ni mfupi akilinganishwa na twiga aliyekomaa, bado ni mrefu kuliko watu wengi. Kumwona ndama asiyeogopa na mwenye udadisi anayesimama wima kando ya mama yake mrefu aliye macho kwavutia sana.
Katika majira ya kuzaa, twiga wachanga hukusanyika pamoja katika vikundi na wanatumia wakati huo kupumzika, kucheza na kutazama mambo yanayoendelea. Ndama mchanga anakua haraka sana. Anaweza kukua kwa meta moja kwa muda wa miezi sita, na anaweza kukua kwa meta mbili katika mwaka wake wa kwanza. Katika juma moja tu ndama huenda akakua kwa sentimeta 23! Twiga wa kike humlinda sana mtoto wake, na hata ingawa anamruhusu kutembea mbali, uwezo wake mzuri wa kuona unamwezesha kumtazama.
Kwa sababu ya ukubwa, wepesi, na pia uwezo wake bora wa kuona, twiga hana adui wengine porini mbali na simba. Hata hivyo, mwanadamu amewawinda na kuwaua twiga wengi sana. Ameuawa bila huruma kwa sababu ya ngozi yake maridadi, nyama yake tamu, na nywele ndefu nyeusi za mkia wake—ambazo baadhi ya watu wanaamini zina nguvu za kimizungu—na kwa sababu hizo wanyama hao watulivu wanaelekea kutoweka. Zamani za kale twiga walikuwa wengi sehemu mbalimbali za Afrika, siku hizi wanakaa salama tu katika mbuga za pekee na katika hifadhi za wanyama.
Leo wageni wanaotalii Afrika bado waweza kusisimuka kuwaona twiga wenye shingo ndefu wakikimbia kwa uhuru katika nyanda pana sana zenye nyasi. Huko wanaweza kuwaona wakila matawi ya juu ya mkakaya ama wakitazama tu mbali kama wanavyozoea twiga. Mnyama huyo mwenye fahari, mwenye umbo maridadi la kustaajabisha na mpole, kwa kweli ameumbwa kwa njia ya ajabu sana—ni uthibitisho mwingine wa uwezo wa kubuni na utu usio na kifani wa Mungu mweza yote, Yehova.—Zaburi 104:24

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante sana kwa maelezo haya. na vile Twiga ni mmoja wa wanyama niwapenda nimefurahi kujua maelezo hayo ambayo sikuyajua. Hii ndio inaitwa kutonyimana ELIMU .Kwa kweli naweza kusema nina kila haki ya kujivunia mbuga/vivutio vyetu

Anonymous said...

Ameuzwa uarabuni na viongozi wetu bila huruma wala utu

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina hapao juu..naomba ufafanuzi nani kauzwa uarabuni?

Christian Sikapundwa said...

Na kupa hongera Dada Yasinta kwa kupata picha nzuri za wanyama wa Mbuga ya Mikumi.Nilibahatika mwaka juzi kupata picha ya Nyani mzuri,lakini nyani yule alipendeza vile alikuwa anapata vyakula kutoka kwenye magari ,akiona gari anasogelea ili atupiwe ndizi na vyakula.Juzi nilipita kutoka Dar es Salaam sikubahatika kuona mnyama.

ray njau said...

Ulimi wa Twiga na viumbe wengine.
---------------------------------
ULIMI wa twiga una urefu wa sentimita 45, unanyumbulika, na una nguvu za kutosha kung’oa majani katika matawi ya miti. Ulimi wa nyangumi mwenye rangi ya bluu-kijivu una uzito kama wa tembo. Wazia nguvu zinazohitajiwa ili kuusogeza tu ulimi huo!
Ulimi wa mwanadamu hauwezi kamwe kulinganishwa na ukubwa, uzito, na uwezo wa ndimi hizo. Hata hivyo, una nguvu zaidi. “Kifo na uzima viko katika nguvu za ulimi,” inasema Biblia kuhusu kiungo hicho kidogo cha mwili wa mwanadamu. (Methali 18:21 Kwa kweli, ni mara ngapi tumesikia nguvu za kifo za ulimi wa mwanadamu zikitumiwa kutunga uwongo na ushahidi wa uwongo ambao umesababisha uharibifu, hata kifo cha watu wasio na hatia?
Vivyo hivyo, urafiki wa muda mrefu umevunjwa na maneno yenye kuumiza. Watu wameumizwa kihisia na maneno makali. “Ninyi mtaendelea kunikasirisha nafsi yangu mpaka wakati gani na kuendelea kuniponda kwa maneno?” akalia Ayubu aliyeshutumiwa sana. (Ayubu 19:2 Mwanafunzi Yakobo alieleza kwa njia nzuri nguvu za kuharibu za ulimi usiozuiwa: “Ulimi ni kiungo kidogo na bado hujigamba kwa njia kubwa. Tazameni! Ni moto mdogo tu unaohitajika ili kuuwasha mwitu mkubwa! Basi, ulimi ni moto.”—Yakobo 3:5, 6
Kwa upande mwingine, nguvu za ulimi zinaweza pia kuleta uzima. Maneno ya huruma na yenye kufariji yamewaokoa watu fulani walioshuka moyo na kuwazuia wasijiue. Kufuata mashauri mazuri kumewaokoa watu wengi waliokuwa wakitumia dawa za kulevya na wahalifu wa mitaani kutokana na kifo cha mapema. Kwa kweli, matunda ya ulimi wa mwadilifu ni “mti wa uzima,” na “neno linalosemwa wakati unaofaa ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu kwenye chombo cha fedha kilichopambwa.”—Methali 15:4;25:11
Hata hivyo, njia nzuri zaidi ya kutumia ulimi ni katika kumsifu Yehova Mungu, kutangaza habari njema ya Ufalme wa Mungu, na kuwafundisha wengine kweli zenye thamani za Biblia. Kwa nini? Yesu alisema hivi: “Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na juu ya yule uliyemtuma, Yesu Kristo.”—Yohana 17:3; Mathayo 24:14;28:19, 20

Anonymous said...

Hongera