Thursday, July 5, 2012

MAONI YALIYOTOLEWA NA KAKA RAY NJAU KUHUSU MAISHA NI ZAWADI!!!


RAY NJAU MWENYEWE
@Hakika wewe ni mwanazuoni mahiri na makini katika tansia ya habari na elimu kwa jamii. Blogu ni gazeti kama magazeti mengine tunayaona mitaani kwetu.Tofauti ni namna ujumbe unavyowasilishwa kwa wadau na jamii kwa ujumla.Blogu inawasilisha ujumbe na taarifa zake kupitia njia ya elektroniki.Hii ni changamoto kwa wamiliki wote wa blogu kuendelea kuwasilisha kwa jamii kile kitu ambacho kwa kweli ndiyo matarajio ya jamii.Nampongeza sana Yasinta kwa kuendelea kuwekeza muda wake katika kuienzi lugha ya Kiswahili akiwa huko ughaibuni.Kupitia mada hii nimejifunza umuhumu wa kuchagua picha inayofanana na mada husika ili ibebe taswira ya ujumbe uliopo ndani ya mada husika.Picha iliyotumika ni sahihi kabisa nami nahitimisha kwa pongezi na shukrani nyingi kwa Yasinta na wasaidizi wake katika blogu( mama maisha blog) ya maisha na mafanikio.
Maoni yanatoka katika mada hii MAISHA NI ZAWADI. KILA LA KHERI KWA WOTE NA AHSANTE SANA KAKA RAY.

6 comments:

Simon Kitururu said...

Amen!

ray njau said...

@Yasinta;
Asante kwa maisha ni zawadi ndani ya maisha na mafanikio.Hii zawadi kwa wadau wote wa kibaraza cha mama maisha.

emu-three said...

Twashukuru sana bwana Njau, na ndugu wangu kwa ujumla, tupo pamoja!

Yasinta Ngonyani said...

Nami ngoja nichukue nafasi hii na kusema Ahsante sana kaka Ray...na Simon pia emu3 ahsanteni sana kwa kusema mliyO nayo moyoni.PAMOJA DAIMA.

ray njau said...

@Yasinta;
ASANTE SANA!!

ray njau said...

@Yasinta;
ASANTE SANA!!