Au tu kwa vile ni jumatano ya marudio basi ngoje turudie na hii. nimeipata hapa
Tusalimiane japo kwa maneno
machache wakati wowote bila kujali majukumu yetu ndani mikikimikiki ya maisha
kwa kuwa kila mmoja anamhitaji mwenzake kwa nyakati tofauti ijapokuwa nyakati
nyingine waweza kuhisi kuwa mtu fulani siyo muhimu sana kwako lakini wakati wa
uhitaji ndiyo unatambua bila fulani mchakato wa maisha na mafanikio hauwezi
kufikia tamati.
Kama wingi wa viungo
mwilini kwa kutazama lakini wakati wa mahitaji kila kimoja kwa nafasi yake
humtimizia binadamu haja yake.
"Salamu ni daraja la
urafiki"
Wasalamu na
shukrani;
JUMATANO NJEMA!!!
4 comments:
Hakika salamu ni ufunguo maisha na mafanikio kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.Je wewe umewasalimia watu wangapi leo?
labda Ishirini au zaidi!!
Ujumbe huu umenikumbusha salamu za redio Tz, nani anakumbuka majina ya wanasalamu mashuhuri? ghafla majina yamenitoka...
Ubarikiwe Yasinta na wote watakaopitia hapa..
Kila kimoja kwa nafasi yake... mawaidha mazuri sana Da Yasinta
Post a Comment