Wednesday, October 19, 2011

HOSPITAL YA LITEMBO YATIMIZA MIAKA 50!!!

Tarehe 10/6/2011 Litembo Hospital ilitimiza miaka 50 ya kutoa huduma ya afya . Ashukuriwe Mungu. Picha hizi nimetumiwa na Padre Raphael Ndunguru ambaye tulisoma pamoja shule ya msingi Lundo.

Hospital ya Litembo
Hapa huyu mwenye kanzu nyeupe ni mhashamu Askofu mpya wa jimbo la Mbinga John Ndimbo.
Sr. Maria Meiss avishwa taji:- Ametumikia Litembo kama muuguzi kwa muda wote wa miaka 50.
Hapa akina mama kwa furaha wameungana kusherehekea.

6 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana Hospitali yetu..

ISSACK CHE JIAH said...

hongera kwakweli je miundo mbinu ni ileile maana toka 83 nimalize shule kule sijaenda tena kulikuwa na Dr waya sijuwi yupo kweli? nilitibiwa nikapona pale kulikuwa na madokta wazuri.kwakweli naipongeza hospitali yetu mungu azidi kuipa uimara na serikali ipanue miundo mbinu yake
Che Jiah

chib said...

Huyo aliyedunda miaka 50 kwenye hospitali hiyo hiyo, Duh!

John Fisher said...

Hongera Hospitali ya Liembo. Mimi mwenyewe nilipata mattibabu madhubuti hapo miaka ya 1985 kwa Dr. Weyer ambaye aliweza kugundua shida yangu ya afya na kutoa ushauri nihamishwe toka Peramiho hadi Roma kwa masomo kwa minajili ya afya na masomo yangu.

Mbele said...

Shukrani kwa taarifa hii na picha. Hapa ndipo nilipozaliwa na kusoma shule ya msingi. Enzi hizo shule ya msingi ilikuwa kuanzia darasa la kwanza hadi la nne.

Siku alipofika Dr. Weyer na wauguzi wake kutoka Ujerumani, akiwemo huyu muuguzi anayeonekana hapa, sisi tulikuwa tarasa la tatu. Nakumbuka tulijipanga barabarani tukiwangojea, na kulikuwa na manyunyu ya mvua ya hapa na pale.

Chini ya Dr. Weyer, hospitali hii ilipanda chati sana, na watu walikuwa wanafika hapo kutoka pande mbali mbali za Tanzania, kutibiwa.

Mwezi Agosti mwanzoni, nilikuwa hapo kijijini, nikaja hadi hapo hospitalini, maana ndipo kilipo kituo cha magari ya kwenda Mbinga.

Anonymous said...

PROFESA WANGU Mbele umekatisha hayo maelezo nilikuwa na hamu ya kuenderea kusikliza.............batamwa