Friday, April 15, 2011
IJUMAA YA LEO: HEBU FIKIRIA MILO YETU HII YA ASILI, WANAODHARAU VYAKULA KAMA HIVI HAO WANA HASARA HASWA!!!
Najaribu kufikiria naamka asubuhi. Naingia shambani kuchuma boga, nalichemsha na halafu tayari kwa Chakula cha asubuhi. Yaani boga kwa chai ya rangi. Kwa mimi chai yangu kama kawaida bila sukari hapo nitafaidi na kulamba mikono. Na mchana ni ugali, samaki, mboga majani kidogo, mchuzi, maharagwe kinywaji maji. Mmmm!! yam yam yam!!utamu jamani ...karibuni tujumuike basi.... Jioni naona tubadili mboga, tutakula KISAMVU ..yaani hapa mimate hadi inanidondoka si mchezo ..karibuni sana jamani tufaidi uhondo huu... Picha hizi kutoka kwa kaka Mjengwa . IJUMAA NJEMA WANDUGU!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
14 comments:
nawe pia ijumaa njema kipenzi ubarikiwe,,nimependa sana vyakula hivyo vya asili.
Ijumaa njema Da Yasinta!
Ila utawarusha roho watu wengi kwa mamisosi kedekede!
dah mlo uko kamili kabisaaaa.
eat only the living food, will give u life. but dead food will give u death!!!!
Nipo job lakini umenikumbusha kitu, jana nimepokea zawadi kutoka kwa mama. Kanutumia mahindi mabichi, viazi mviringo,maharage na boga. Yani nikirudi tu nalichemsha halafu nalila kwa kijiko tartiib, nna kama miaka minne hivi sijakula hii kitu.
Na wewe pia,njaa inaniuma naingia humu nakutana na vitu kama hivi...we mchokozi sana.
xx
Ijumaa njema kwako pia Mrembo!
weweeeee dada Yasinta usifunge malango wangu,mimi leo mgeni wako!!!!!mambo iko huko!
Ijumaa njema nawe na familiya!.
weekend njema kwako
Hiyo picha ya chini imenikumbusha makumbusho ya taifa DSM.
hivi kwanini watu wngi hawaupendi ugali?kwanini watuwengi hawyapendi maharage/we.? kwa nini siku ukipikwa wali katika familia zetu nikama sikukuu? kwanini ukikosa sukari nyumbani unasononeka je asali siyo tamu ?.dagaa nazo je niza watu wa hali ya chini.?mchicha nao unatatizo gani? kaka s
Yaani dada hapo umenikumbusha kijijini kwa chai ya asubuhi mpaka mate yananitoka natamani ningeipata sasa hivi ningefurahi sana.
Haya watu wa diet semeni sasa..
@Mwanamke wa SHOKA:Ki-diet HASA ,...
....labda umezidisha kula kama ndani ya siku umekula vyote hivyo pichani!:-(
Post a Comment