Thursday, April 21, 2011

HESHIMA KWA WANAWAKE

Kweli huu uungwana?


Acheni niwape heshima iliyotukuka wanawake woote;
IMAGINE:

ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa
anakusamehe halafu anasahau!!!

UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye
anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni
kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia
chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila
manung'uniko.

UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma
kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala
halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna
maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena
inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruwale
imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo
ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana
kashasahau na kukusamehe!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto
anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina
atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi
kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE,
WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!

HIVI INGEKUWA WANAUME TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Nimeipenda habari hii na nimeona niwahabarisha na wenzangu kwani elimu ni kuelimishana. habari hii imetoka Jamii Forum.

10 comments:

Simon Kitururu said...

Nanukuu :`` HIVI INGEKUWA WANAUME TUNAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?´´´-mwisho wa nukuu.


Mengi yatajwayo hapo wapo Wanaume wanafanyiwa tukiachia kuzaa kwa uchungu ambako siku hizi wako wanawake ambao hawazai kwa uchungu kwa kuwa sayansi inaruhusu uwezekano huo ukiachilia mbali kuwa siku hizi kuna wanawake walipao wanawake wengine wawabebee mimba``surrogate mothers ´´ ili wasiharibu miili yao au tu kwa kuwa wako bize.

Tukiachana na hilo !

Hivi si kuna maswala ya kudai usawa siku hizi kitu ambacho kinahitaji ijengwe tabia ya KUHESHIMU BINADAMU WOTE wawe wanawake au wanaume?

Nimewaza tu kwa sauti!:-(

Unknown said...

Thamani ya mwanamke ni kubwa sana.Personally have been touched na hii article.

Unknown said...

Thamani ya mwanamke ni kubwa sana.Personally have been touched na hii article.

Fita Lutonja said...

Kwa watu wanaoamini humanism wanaumia sana nikiwepo na mimi mfaasi wa mwanasaikolojia Abrahim Maslow na Karl Rogers. Yaani inapain kuzidi kiasi

chib said...

Mtakatifu, nimekusoma kwa makini!

Anonymous said...

Mwanamke ni katika viumbe muhimu sana katika vilivoumbwa na Mola wetu.
unajuwa hata katika quran tukufu mwanamke amefananishwa na jua linalowaka mchana kwa manufaa ya Binadamu na mwanamume ni mwezi.

kipi unahitajia zaidi JUA au MWEZI?

malkiory said...

Sipo mbali na Kitururu!

nyahbingi worrior. said...

Haya yote yanatokea kwakuwa tunapuuzia mila la desturi zetu,kwakuwa tumeamuwa kuiga ya ugenini,basi kila siku itakuwa ngumi mpaka ile siku tutakumbuka mila na desturi zetu.

Mizimu imekasirika kwakuwa mnaabudu ya ugenini.

Na bado.

Sellasi.

Goodman Manyanya Phiri said...

Kwa wanaume wenzangu wanaopiga au kuwadhalilisha wanawake, "adhabu yako haiko mbali!"

Hamna siri duniani kote kubwa kuliko mwanamke; wala hamna hekima kubwa kuliko mwanamke.

Sina uhakika lakini ndoto ya "usawa" itatimia. Moja ya matatizo ni kwamba hatuna maana moja ya "usawa" hapa na kila mmoja anawaza lake ikiwa wengine wanawaza usawa kiasi kwamba "kidole cha mtu kiwe sawa na jicho lake naye VENUS apate uleule ukubwa waJUPITER".

Hamna kitu kama hicho ulimwengu mzima!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hivo eeh?