Monday, November 29, 2010

Nyumbani ni nyumbani...


Nadhani wote tumeianza Jumatatu vizuri, binafsi nipo salama na siku yangu imeanza vizuri na ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na nimeiona siku ya leo.

9 comments:

emu-three said...

Kweli nyumbani ni nyumbani, na kumbukumbu zetu zinatuama katika taswira za umasikini...nembo , alama, na ...lakini wanasema nyumbani ni nyumabani hata kama ni pangoni!

John Mwaipopo said...

ndani ya nyumba ya paa la nyasi si joto la kutisha wa baridi ya kutisha vipenyavyo. kuna raha yake hasa ikiwa woote katika kijiji mmeezeka kwa namna hiyo hivyo hamna wa kumuonea wivu ama gere mtu mwingine.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kweli tupu Dada Yasinta. Kama haivuji hata mvua ikinyesha kimyaaaa!!!

Baraka Chibiriti said...

Hata kuweje, kwenu ni kwenu tuuu...hakuna kuona aibu!

Rachel Siwa said...

kweli Nyumbani ni nyumbani,pawe baya au pazuri ni kwetu tuu na vyema tukapatunza.

Unknown said...

Nyumbani hapo hukoo Namatutwe, Masasi Ntwala!!! Karibuni tule samaki nchanga!!!

Simon Kitururu said...

NYUMBANI ni NYUMBANI lakini hiyo nyumba kwenye picha siipendi ....

:-(

Penina Simon said...

Napenda sana hzi nyumba zinaleta utamaduni wetu halisi, lkn na wasi wasi ipo sku zitapotea kabisa yaani

Jacob Malihoja said...

Umenikumbusha Mbali Sana Yasinta.. nitakupa stori kamili kwenye blog yangu hivi karibuni.. tulia!