Monday, November 1, 2010

HUU NDIO WEMA!

Jirani kala nini?

Huu ndio wema! Unapotenda wema usitegemee fadhila. Unapokuwa na marafiki, ndugu, na jamaa wa karibu, watendee wema bila kudhamiria kupata fadhila kutoka kwao. Ninapoongelea wema na kutoa ninamkumbuka mama Theresa wa Calcutta ambaye kwa umri na maisha yake angelikuwa Bilionea lakini kwa kujitolea kwake alikufa masikini, lakini akiwa ni tajiri wa nafsi. Nina maana alikufa akiwa na ridhiko, kwani kazi aliyotaka kuifanya aliifanya tena kwa kufaulu. Je wewe hufurahii kuwa kama yeye?
Kumbuka amri kuu isemayo “mpende jirani yako kama unavyojipenda” Je unapokula na kusaza huwa unajiuliza kuwa jirani kala nini?

Tafakari……… hii aliandika mdogo wangu wa hiari Koero Mkundi.

4 comments:

Simon Kitururu said...

Nawasiwasi na:


``Theresa wa Calcutta ambaye kwa umri na maisha yake angelikuwa Bilionea ..... alikufa masikini,.... Nina maana alikufa akiwa na ridhiko.´´ -katika andiko.

Ukimfuatilia huyu mama kunamengi tu yanakwaza. Kwa mfano tu mmoja kuwa alikuwa anaamini kuwa masikini anaoshughulika nao wasitoke kwenye umasikini hasa kwa kuwa aliamini umasikini husaidia watu kuwa karibu na Mungu. Sasa jiulize kuwa mtu mwenye imani hiyo alikuwa anawasaidia kweli hao Masikini katika maana ya kusaidia masikini watu waitambuayo kirahisi? Na je ni kweli kibano cha umasikini hakiwezi kuchangia baadhi ya dhambi?


Pili , katika baadhi ya barua zake zilizowekwa wazi baada ya kufa kwake inaonyesha kuna wakati alikuwa anakwazika kama watu wengine tu kuhusu ni nini madhumuni ya Mungu. Je hilo ni ridhiko?

Nawaza tu kwa sauti!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mhh watakatifu watangazwao na binadamu asiyemtakatifu wanamengi ya kujiuliza kama wunafikiri na kuwaza kwa kujitegemea

emu-three said...

Tenda wema uende zako eeh, usingoje shukurani eeh, binadamu hawana wema eeh, hata....lalala , nafikiri wakale mnaujua huo mziki!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote Tupo Pamoja daima. TEANDA WEMA nenda zako usingoje shukrani duniani hapa.