Sunday, September 5, 2010

Mtu, Kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake!-TAFAKARI

Mathayo 7:15-20
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.

Luka 6:43-45
Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo Wave
Habari hii nimeipata nimeipata hapa http://strictlygospel.wordpress.com/ na nikaona si mbaya kama nikiweka katika kibaraba cha Maisha na Mafanikio. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE

2 comments:

EDNA said...

Ubarikiwe dada kwa kutushirikisha kwa neno la Mungu.

emu-three said...

...HAKUNA MTI MZURI UZAAO MATUNDA MABAYA, NA MABAYA KUZAA MAZURI...'
Haya maneno waliyajua mababu zetu ambao wakati huo walikuwa wakitumia dini za asili.
Ukitaka kuoa, au kuolewa lazima uchimbe undani wa hiyo koo unayotaka kuoa au kuolewa.
Huu ni mfano tu mdogo, kuwa chanzo cha matatizo mengine huanzia mbali, na kwa kutokuwa makini tunajikuta `tunarithi' yale mabaya yaliyoanzishwa na wengine.
Hako ni ka mchango kangu tu, najua wenzangu mnayaelewa zaidi maneno hayoo kuliko mimi.
Ahsante dada Yasinta