Thursday, March 25, 2010

MILA NA DESTURI ZA WANGONI:- Upande wa ndoa na kuchumbia

Kwanza uchumba halafu harusi/ndoa.

Katika mila za wangoni, hapo zamani kijana na msichana wakikua kufikia umri wa kuoa walioa. Kwa mila za wangoni, mtoto wa kiume hata kama akikua na kuoa halafu hajaenda vitani ilikuwa haionyeshi maana. Wakati wa kupigana vita kijana ilibidi aonyeshe nguvu zake zilivyo. Kijana ambaye bado hajaenda vitani aliitwa (walimwita) ”lijaha” ikiwa na maana ya kijana/mvulana mdogo. Kijana ambaye ametoka vitani walimwita/aliitwa ”lidoda” ikiwa na maana mkubwa . Mke wa kuoa walimtafuta ambaye ni mwenye ukamilifu, anayejua kufanya kazi za nyumbani. Anatafutwa mwanamke anayeweza kuokota kuni, kuchota maji, kutwanga, kupika chakula, kupika pombe na awe mwanamke anayecheka vizuri na watu wote katika mji.

Ndoa haifungwi katika ukoo. Kwa wangoni hawaoi mke au kuolewa na mume mwenye (kibongo) ubini mmoja. Kama watu wakioana katika ukoo, basi wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali. Kama hawa watu walioana katika ukoo wa karibu, basi watawaapizia. Watu wnaogopa kuoana ndani ya ukoo kwasababu wakifanya hivyo watoto watakaozaliwa watakufa. Na pengine watoto hao watapata kifafa au pengine mababu (mahoka) watakasirika.

Mtenga:-

Kwa kingoni cha zamani mtenga ni mtu anayenunua au kuuza kitu. Mtenga anamuuza mototo wa kike. Yeye ndiye atoaye ”Chiyagabuli” yaani mali ya mwanzo na ”Mawolowolo” ikiwa na maana mali yote kwa wenye mtoto wa kike.

Kulonda mdala=Kutafuta mke:-
Wenye mtoto wa kiume wanapotaka kumwoza kijana wao , wazazi wengine walimtafutia mke. Wazazi wengine walimwacha kijana wao atafute mwenyewe mke. amtakaye. Kama walimwona msichana mrembo watamtafuta ndugu yao ambaye watamtaka na kumwelezea habari za ndoa. Na huyu ndiye atakayekuwa MTENGA wao. Mtenga huyu ataanza kuulizia kwa siri mambo ya wazazi wa msichana yule na wanaukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa kijana. Kama wazazi wataona ya kuwa ni msichana wa hodari, watenga wale wataenda kwa wazazi wa msichana na kuuliza kama wanaruhusiwa kumwoa? Kama wenye binti watakataa, watenga wataombeleza.

Kujitokeza:- Ni lazima wawe na kiulizio , watenga ndio wataenda kuulizia kumwoa mke. Wanapoenda kule , wanachukua kitu fulani ”lukotelu au luhongelu” ni kiulizio , kitu hicho chaweza kuwa nguo, ushanga au hela nk.

Chiyagabuli= Mahari ya mwanzo

Kama wakwe wa pande zote mbili wanakubaliana watoto wao waoane, watenga watapeleka mahari kidogo kwa mama na baba wa binti ambayo ni mahari ya mwanzo. Baada ya muda yatapelekwa tena mahari ya mwanzo yaani kwa mara ya pili itakuwa jembe moja LUSUKA. Kama aina fulani ya jembe "ngwamba" ni jembe lenye tundu pale pmini unapotumbukizwa. Hii itamaanisha binti yao tayari amekwisha poteza ubikira

Kuchicha= kumtembela mchumba
Kuchicha ni kitendo cha msichana aliyechumbiwa kwenda rasmi kumtembelea mchumbake, kimila huyo msichana aliyechumbiwa anaenda na rafiki yake wa kike. Hivyo basi siku hiyo inakuwa ni kama anaenda kuona mazingira atakayokuja kuishi. Kimsingi katika siku ya kuchicha hairuhusiwi kulala pamoja na kufanya mapenzi ndio maana msichana alipaswa kusindikizwa na msichana mwenzake. Lakini basi mara nyingi imekuwa ngumu kujizuia wengi wamekuwa wakiishia kufanya mapenzi, mbaya zaidi unakuta mvulana anaalika na mvulana mwenzake halafu wanagawana hao wasichana waliofika hapo. Lakini pia hilo neno limekuwa likitumika isivyo rasmi kama vile kitendo cha msichana kutongozwa na mvulana wapo walioita kitendo hicho kuchicha na imezoeleka na wengi.

Au pia inakuwa kinyume:- Kijana wa kiume pamoja na vijana wenzake wanaenda rasmi kumtembea mchumba/msichana. Huko anafanya kazi nyingine nyingi. Kwa kufanya hivyo, wakwe watamwona ni kijana /mume wa uhakika, kuwa anaweza kufanya kazi za kianaume, kama anajua/weza kulima kukata matema(kukata miti shambani kwa ajili ya kuandaa shamba), kama ana kaa/ishi vizuri na watu au kama hana haraka ya kula. Muda wote huo wa aliokuwepo, kijana huyu hajionyeshi kwa wakwe zake. Anapotaka kutoka nje ya nyumba alalayo ni lazima ajifunike nguo usoni gubigubi. Kijana atafanya hivyo atakapotaka kumwona mtarajiwa mkewe, hakuna kujionyesha kwa wakwewe mpaka atakapozaa mtoto. Na mwanamke atafanya hivyo kwa wazazi wa mumewe.

Nimefanya utafiti katika kuon au kulipa mahari inaweza kuwa kama ifuatavyo
Mbuzi 1 dume
Mbuzi 5 dume 1 , majike 4
Sufuria kubwa 1
Mablanket 2
Nguo- kanga doti 2
Nguo vitenge doti 2
Nguo shuka 2
majembe 2
Simulizi/maelezo ni kutoka kwa babangu mzee Ngonyani

Ngoja tusikilize pia ngoma hii ya kitoto/lizombe ambayo ni ngoma ya wangoni karibuni!!

13 comments:

Unknown said...

Kumbe kuoa Wangoni ni rahisi namna hii....
Hebu Jaribu kwa Wamasaai, kwa akina Edo Ndaki, Wakurya, Kwa kaka Chacha Wambura, Wasukuma kwa Prof. Matondo na kwa kina Koero.....LOL

Bila Ng'ombe Kadhaa, mke utamsikia tu

MARKUS MPANGALA said...

mmmhhh umenikuna kwelikweli iiiiiiii aise yaani LIDOD/LIGOSI/LIKAMBAKU Lol.....
Nikakugwisa palaaaaa halafu lindeku kuneng'enura wamuayangu..... ha ha ha
lakini Mau ibesa kweli VAGOSI vamundela ni Vadala va mundela..... ha ha ha kamwali pekendula pekenduuuu pekenduuuuuu lya lya lya lya.

Lya Ngoku lya firigisi lya chibindi...... mmmmh jamani LIGOSI lela likugana kweli kweli, utamsea kwa baba? ha ha ha ha ha ha ha ha ha mwengaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

arrrrrrrrrriiiiiiiiiiiiiii.
umenikuna sana na hiyo picha halafu nawaza ndiyo nipo ngomani raha kwelikweli kuoa ................LAKINI..............NITAOA NITAKAPO TAKA.

Fadhy Mtanga said...

Kumbe mila ya Wangoni haijatofautiana sana na Wabena katika taratibu za uoaji. Hata kwetu ni mwiko kuoana watu wa ukoo mmoja. Hata ubini ukifanana ni kasheshe. Na kijana unapotaka kuoa ama kuoelewa, wazazi watachimba sana ili kupata ufahamu wa kutosha juu ya ukoo unaotaka kuunda nao ujamaa. Pia hupenda kuchunguza kama ukoo huo una magonjwa ya kurithi na mambo kama hayo.
Kuhusu mahari, naona hatupishani kabisa.
Ahsante sana da Yasinta kwa elimu nzuri kama hii.

mnkadebe said...

Asante sana dada Yasinta,aiseh hapa umenisaidia kweli,kweli.Nitaisevu makali hii kama kumbukumbu na simulizi nzuri sana kwenye upande wa ndoa na kuchumbia.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Kama huko kwenyu hamuoani wa ukoo basi katika mila za baadhi ya jamii za kikurya BINAMU (mtoto wa Shangazi/Mjomba) ni ruksa kuonja na kuoa kwa kuwa BINAMU ni NYAMA ya HAMU....lol!

In fact wanakwambia kuwa ni kutopeleka rasilimali za familia nje ya ukoo na mkihitilafiana kama kubwengana mangumi mke anakwenda kwa MJOMBA ama SHANGAZI na si UKWENI :-(

Huko kama mume ama mke ndo mwenye makosa yaani inakuwa ni shughuli kwa kuwa atasomewa risala hiyoooo na shangazi ama mjomba...lol

Patamu hapo eti eh!

Kwa mahari ukioa ukuryani na jamii zake lazima ujiandae japo hawana categories kama za wasukuma. Ni mang'ombe mengii!!! Nakumbuka mama yangu aliolewa kwa ng'ombe 35 na ma Mkubwa zaidi ya hapo.

Nasema si kama usukumani kwa kuwa binti mweupe ana thamani sana kwa wasukuma hasa wa NTUZU (samahani Matondo....lol).
Akiwa mweupe mang'ombe kadhaa, akiwa na wowowo mang'ombe kadha! akienda kidato mang'ombe kadhaa nk!

john said...

ok dadangu nangonyani mm naitwa john ni mzawa wa ruhuwiko kwa maana hiyo ni wa kunyumba na hivi sasa nipo india kwa taaluma pia ni mdau sana wa blog yako na hii mada imegusa vilivyo.nimelazimika kuyanakili haya kwa ajili ya baadae. ila natatizwa na jambo moja naomba mrudie huyo mtoa mada anisaidie,yaani mgawanyo wa hayo mahali nani anastahili katika ukoo husika,na maanisha wajomba mashangazi,bibi,mama na baba.pse help.

Unknown said...

nifuneye kumanya ngiti vikemela mawolowolo au malowolo?

Mfundishi said...

Umenena vyema dada, endelea kutuonesha njia. Je tunaweza kusemaje juu ya mila ya wangoni:zimepitwa na wakati, Unyanyasaji kijinsia, au Ubaguzi? Tunapaswa kutafakari kama ni busara kuachana na utajiri huu wa kimila na kudandia ya wenzetu.
Regards

Yasinta Ngonyani said...

mila na desturi za kingoni kusema kweli zinatofautiana sehemu na sehamu na ukoo na ukoo. Kuna wenginene wanatosa mali nyingi sana na wengine ni kama asante na wapokeaji ni pia tofauti ukoo mwingine anaweza kuwa baba na mama tu na ukoo mwingine wanaweza kugawana wote yaani bibi, babu, shangazi, mjomba, mama, na baba.

Kaka chalres nikosili ni kweli linaandikwa malowolo. Ahsante!

Mfundishi! unyanyasaji kijinsia haupo kwa wangoni tu ni kila sehemu kwa hiyo ningeona mila za koingoni zisitupwe kabisa. Kwani ni asili yetu tukizitupa basi tutakuwa tumejitupa pia.

Unknown said...

Nawapenda wanguni saanaaa

MUSA SADATALE said...

naanza chuo.Mnitafutie mngoni mmoja wa kuoa. 0754650875

Ni kwa pich,video pamoja na audio mbali mbali said...

Au sio

Unknown said...

Wa kunyumba