Friday, March 5, 2010

Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mume,Baba na Shemeji pia Rafiki yetu

Ni siku yako leo mwl. Klayson
Tunaanza na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sala hii :- SALA YA MKE KUMWOMBEA MUMEWE

Ee Bwana , ni ajabu,
Jinsi fikra zangu zinavyomrudia kila mara
Huyu, mume wangu,
Mwenzi anayeshiriki maisha yangu kwa namna ya pekee.
Ninapofagia nyumba na mazingira yake,
Nataka kutengeneza nyumba nzuri kwa ajili yake.
Ninapopika chakula vizuri,Napenda kumfurahisha.
Ninaponunua nguo mpya na kujaribu kuonekana mrembo,
Ni kwa ajili yake tena, Ee Bwana.

Na ninaweza kukuambia kwamba
Ninamwonea fahari,
Anafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki yetu;
Ni mtu mwenye haki, mwadilifu,
Naye hujitahidi kutufurahisha.
Kwangu, yeye ni mpole na mwangalifu.
Hunijali na kuonyesha kweli kwamba anajali.
Hunifanya mimi nijiamini mwenyewe,
Anajua jinsi ya kuondoa hofu zangu,
Hunipatia usalama na upendo ambao nahitaji sana.

Ee Bwana, ninakuomba,
Umbariki na umlinde.
Katika safari zake, umfikishe salama.
Kazini mwake, umpe fanaka
Na hapa, nyumbani petu naomba apate amani na heri.

Bwana, unisaidie mimi pia
Niweze kuwa yule mke anayehitaji.
Unifanye niwe mtu anayeweza kumwamini daima,
Mwanamke ambaye anaweza kumfurahia,
Niweze kumsaidia asahau matatizo yake,
Niweze kuondolea mbali hofu zake na kupunguza uchungu wake.

Bwana, Wewe ndiwe uliyenipa mume huyu,
Na katika yeye,Umenipatia sehemu ya nafsi yako mwenyewe.
Ninakusifu kwa ajili yake, Ee Bwana.

Na leo twakumbuka siku muhimu saana maishani mwako. Siku iiliyoanzisha yote mazuri/mema tujivuniayo maishani kwa uwepo wako. Ni SIKU HII ULIYOZALIWA

Zaidi mtembelee Mwalimu Klayson http://matetereka.blogspot.com/

Tunapenda kusindikiza siku hii na mwanamziki ambaye anampenda sana kwa wimbo huu wa DR. REMMY ONGALA Uitwao NARUDI NYUMBANI ni.



23 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Nianze kwa shukrani kwa MUNGU kwa uwepo wa kila mmoja wetu.
Pili naleta salaam za heri ya siku ya kuzaliwa kwa Shemeji yangu lakini si kutoka kwangu tuu, bali kwa familia nzima hapa.
Maisha mema na yenye baraka twamuombea.
HAPPY BIRTHDATE

Faith S Hilary said...

Samaki tupo wengi tuuu!!!! Happy Birthday Baba. Mungu aendelee kukubariki na kuishi miaka 100 kidogo :-)

Koero Mkundi said...

ha ha ha haaaaaa, kumbeeeeee,
Aiseee, hata sisemi happy birthday.....LOL

Fadhy Mtanga said...

Heri ya siku ya kuzaliwa bwan'shemeji. Uwe na maisha marefu sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Duh, Heri y a kuzaliwa, uwe namaisha mafupi ya mwili, marefu ya roho!

John Mwaipopo said...

hongeya kwa kutimiza miaka kazaa Mwalimu Klayson. mungu akujaalie miaka tele kadri ya mapenzi yake.

du yasinta na wewe usita ulikukosa kidogo kama upadre ulivyomkosa mzee ngonyani nini? maana hiyo mistari!

Bennet said...

Mungu akuongezee umri mara dufu na akuope afya njema

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Mwalimu K.

Uwe na wakati mwema nawakati ukikata keki jua tuko nanyi tukisosomola pamoja!

watila said...

yasinta shemeji yetu anatimiza miaka minagapi mungu ampe umri mrefu wenye siha na afya

PASSION4FASHION.TZ said...

Happy birthday shemeji yetu,mungu azidi kukupa maisha marefu,hekima zaidi na mafanikio kwa kila unalokusudia kufanya lifanikiwe.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta hiyo mistari utasema ndo uliyopewa kwenye Unyago Duuh! Kweli wewe ni Mke mwema.

Hongera Baba Camilla, Mungu awe nawe daima.

Furahia siku yako.

chib said...

Heri katika sikukuu yako ya kuzaliwa mwalimu.
Mtunze dada yetu naye akutunze

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Happy Birthday shemeji yetu!

mumyhery said...

Happy birthday Shemeji Mungu akujalie maisha marefu afya njema na furaha tele

mwl. Klayson said...

Asante sana mke wangu. Pia sante kwa wote.

EDNA said...

Grattis på födelsedagen....Shemeji

Nampangala said...

Mlongo hongela sana na bambu kwa siku yake ya kuzaliwa, je umtelikili ugali wa mundula na chikandi?
Za magono mlongo wangu? Nawatakia weekend njema kwako na familie yako.

Nampangala said...

Mlongo hongela sana na bambu kwa siku yake ya kuzaliwa, je umtelikili ugali wa mundula na chikandi?
Za magono mlongo wangu? Nawatakia weekend njema kwako na familie yako.

Simon Kitururu said...

Happy Birthday Mwl. Klayson!

Unknown said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Shemeji,

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa kumpongeza baba watoto wangu. Na pia ahsante sana kwa maoni yenu mazuri.

MARKUS MPANGALA said...

mzee wa matetereka. hongera

Christian Bwaya said...

Kila lililojema mzee! Nakutakia maisha marefu ya mwili na roho