Wednesday, September 16, 2009

WANAFUNZI WA KIKE WAPATAO MIMBA KABLA YA KUMALIZA SHULE WARUHUSIWA KUFANYA MTIHANI

Nimezoea sana kusikiliza habari za BBC, kwa hiyo wakati nasikiliza habari hii, nikaona sio mbaya kama nikiiweka hapa kibarazani kwangu ili wengi msome na tuweze kujadiliana.

Idadi ya wanafunzi wa kike wanaoacha shule kwa sababu ya mimba isiotarajiwa inazidi kupanda

IDADI ya wasichana wanaokatisha masomo yao na kuacha shule wilayani Kericho, kwa sababu ya kupachikwa mimba wasiotarajia imewashangaza maafisa wa Elimu na wadau wengine.

Katika kisa ambacho kimezua mjadala mkubwa juu ya Elimu na mimba miongoni mwa wanafunzi wa kike, imeibuka kuwa toka kwa idadi ya wasichana 25 waliojiunga katika kidato cha kwanza katika shule moja katika eneo hilo, 24 waliacha shule baada ya kutwikwa mimba.

Katika makala ya wiki hii tunahoji nini kinachopelekea hali kama hii ya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi???? Mwalimu mkuu alizungumzia umbali wa shule kuoka kwa makao ya wanafunzi ambao wanalazimika kupitia katika misitu ya chai jambo amabalo linawaweka katika hatari ya mahusiano ya kimapenzi na hata ubakaji.

Mwalimu huyo mkuu alisema ni jambo la kushangaza sana. Aliongezea kuwa idadi ya waichana katika shule hio sasa ni ishirini pekee. Wengi wa wasichana waliokuwa wakifanya vyema katika masomo wameacha shule baada ya wanafunzi wenzao na baadhi ya wafanyakazi katika mashamba ya chai kuwatwika mimba.

Elimu ya watoto wa kike inaendelea kuwa ndoto isioweza kutimika katika eneo hili la Afrika. Wasichana wengi wanadanganywa na wanaume na kujitosa katika tabia na mahusiano ya kingono yanayopelekea mimba isiotarajiwa. Jambo ambalo huwafanya wasichana hawa kuacha shule na kuanza maisha ya uzazi wakiwa wao wenyewe bado wachanga.

Wengine wanakumbwa na vizingiti vya kitamaduni kama vile tohara ya wanawake, ndoa za mapema, kazi za nyumbani, magonjwa na umasikini. Kumekuwa na mjadala iwapo kuratibishwa kwa masomo ya afya ya uzazi katika silabasi za shule kutaksaidia kudhibiti mimba isiotarajiwa na magonjwa ya zinaa miongoni mwa wanafunzi.

Inchini Tanzania serikali, kwa mara ya kwanza, imewaruhusu wale waliopata mimba wakiwa shuleni kufanya mitihani. Hapo awali wanafunzi waja wazito walikuwa wakikatazwa kufanya hivyo.

Je, nini mchango wako kuhusu yote haya??????

Habari zaidi sikiliza hapa katika kipengele cha kimasomaso. http://www.bbc.co.uk/swahili/

12 comments:

Fadhy Mtanga said...

Duh! Hali inatisha kwelikweli. Katika watoto 25 anapona 1 tu!
Nadhani jamii inapaswa kulipa jambo hii umuhimu wa kutosha!

Simon Kitururu said...

Inasikitisha!

Mhh!
Lakini huko inaonyesha kuna vidume kwa kutongoza haviwezekani!

Dawa ni wasichana wote wafundishwe Kung Fu! na kuanzia darasa la tatu wasichana wote waanze kufunzwa jinsi ya kukataa mtongozo!

[Samahani kama nimelainisha hoja iletwayo na topiki hii muhimu na labda hilo ndio moja la tatizo lifanyalo utatuzi wa mambo magumu kama swala hili la wasichana wadogo kujazwa kidude ushindikane!:-(]

chib said...

Ha ha haa, kung' fu! Naona utatuzi huo unafaa sana kule wanaopenda kupiga mieleka watoto wa kike. Ila kwa wale wanaotumia umaskini wa familia ya mtoto wa kike qwanahitaji kutafutiwa ufumbuzi, njia nzuri ni kuwawezesha maskini kujimudu, na ndipo tamaa ya vishawishi mbuzi itafifia au vp!

Simon Kitururu said...

@CHIB: Kweli kabisa usemalo!

Halafu swala la kutumia umasikini wa watu halitumiwi tu na wanyemeleao wasichana. WANASIASA wanalitumia sana katika mtongozo wa wananchi kwa ujumla kila siku!:-(

Wanacheza na umasikini wa watu kwa kuahidi ahadi za uongo na chakusikitisha vishawishi hivi mbuzi vinatumiwa sasa hivi tunavyoongea na wanasiasa kama wanasukuma mlevi vile watapewa kura kama vile kidude! wakati tunaona hivhivi!:-(

MARKUS MPANGALA said...

Sijui nani adui na mwenzetu! Lakini sijui kama kuna tatizo katika kutongoza lakini mtongozwaji na mto anayetongozwa wanashirikiana katika ule mchezo wa tayari-bado, labda tujue kama serikali yetu inatongoza nayo Lol

Bennet said...

Kitu cha kwanza ni kujenga shule kabla ya hayo mashamba ili wanafunzi wa pande zote wafike shule bila kupita katika mashamba ya chai
Pili sheria zichukue mkondo wake kwa wale wote wanaowajaza mimba, kingine kinachoonekana wazi hapa ni hali ya umasikini iliyokithiri kiasi kwamba hata wazazi wa watoto wa kike wanakuwa wapole baada ya kupewa vijisenti na hao vidume baada ya kuwajaza wanafunzi mimba

viva afrika said...

kiukweli nimechoshwa na mjadala huu, miaka nenda rudi tatizo haliishi, nadhani sheria ya adhabu katika kosa hili yahitaji makali, tuanze kuact si bla bla kila uchao.

Anonymous said...

mhh, hapa hata adhabu ziongezwe mara dufu sidhani kama tatizo litapungua kwa mtindo wa kuongeza adhabu. hapo mimi naona ni elimu tu inahitajika, tuongeze nguvu kwani sidhani kama adhabu zitawafanya watu waache kufanya kale kamchezo katamu, hivi kuna mtu yupo tayari kuacha ule mchezo kweli?

Mzee wa Changamoto said...

Labda tuache kutishana tuanze kuelimishana. Tumezidi kuwaaambia watu kuwa mimba ni kitu kibaya ilhali namba ya wazipatazo inaongezeka. Kuna ubaya gani hapo??? Mitoto yetu ambayo nayo inakuwa "zee-vuma-kichwa-maji" inashindwa kuvumilia na kujaribu. Na kwa kuwa haijui namna ya kujikinga na uhondo inaoambiwa ni m'baya na hawawezi kujadili, basi wakija kugundua namna ni pale maji yanapokuwa sakafuni.
Tuelimishe tusitishe.

Faith S Hilary said...

Mimi kama mtoto wa kike niliona (ni mawazo yangu tu) kwa njia hii tatizo hili halitopungua...najua sio "aim" yake lakini mambo yatakuwa yale yale...kama msichana akitaka grades zake ziwe nzuri (au kwa sababu yoyote ile)kama nilivyosoma article hapo juu...aanzishe uhusiano na mwalimu (or vice versa)...akipata mimba anajua bado anaendelea na masomo...anyway ni mawazo yangu tu...

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni masikitiko makubwa sana wanafunzi 25 anapona mmoja tu. Kwa nini wanaume wanafuata watoto wadogowadogo wakati wanajua ni rahisi kushawishika. Inabidi msaada mkubwa ufanyike. Nikiwa kama mzazi nimeguswa na naanza kuogopa. Sijui nikagombe angalao ubunge? LOL. Asanteni wadau kwa mchongo wenu kwani kila mmoja hapa amejifunza kitu natumaini.

Anonymous said...

Hello. And Bye.