
DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa. Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.
Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).
Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.
Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.
Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi watoe taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.
Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.
Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.
Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.
Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.
Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.
Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.
Habari hii inatoka Jamii Forum imeandikwa na Joyce Joliga, Songea
10 comments:
Hatari kubwa diwani mzima anafanya vitendo hivyo haya yetu macho na masikio.
Jamani jamani. Mbona tunafananisha KIFO NA USINGIZI???
Yaani mtu aliyezini anatoza faini ya pesa? Ili akaendeleze uzinifu?
Mie sijui NJAA itatufikisha wapi. Amegharamia vipimo vya magonjwa ya zinaa na UKIMWI? Ama mume anaenda kununua shuka jipya kwa hizo laki tatu na kisha "kubanjukia" na mzinifu wake?
Mie naacha
DUH!
Kwa hiyo Mke wa shekhe ni shilingi laki tatu kufumaniwa mara moja hata kama nyama ya bata ililiwa angalau kwa miaka mitatu mara mbili kwa wiki?
Mmmmh!:-(
Mengine Mzee wa Taratibu na Mzee wa Changamoto Mshayasema!
Hii haijatulia kabisa,labda niulize swali,huyo shekhe ana wake wangapi? na huyo mke aliyefumaniwa ni wangapi?hapo kweli ukimwi utakwisha? hao hao madiwani ndio wanajidai kuhamasisha watu wajiepushe na ukahaba,sasa hapo anatoa mfano gani?
Ndipo hapoutagundua watu na masuala ya uaminifu katika ndoa hakuna, Sheikh wa watu kakimbilia faini. Na bado lazima amkatie mjumbe pesa ya usuluhishi. Wakuu hapo juu wamenena kiasi cha kutosha. Thup, nimetema mate kwa uozo huo.
Ndipo hapoutagundua watu na masuala ya uaminifu katika ndoa hakuna, Sheikh wa watu kakimbilia faini. Na bado lazima amkatie mjumbe pesa ya usuluhishi. Wakuu hapo juu wamenena kiasi cha kutosha. Thup, nimetema mate kwa uozo huo.
Nikweli hapo inaonekana pesa ni mali zaidi kuliko mke. Wanaume hawana maana kabisa. Samahani kama hii sentensi itawakwanza wengi.
Asanteni kwa kutochoka kutembela maisha .
Mh!
Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.
Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com
Uchawi wa mapenzi wa Dkt. Dawn hufanya maajabu kweli.
Niliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.
Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.
ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
Hirizi za mvuto
Kutatua migogoro ya ardhi na mali
Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com
Post a Comment