Tuesday, August 26, 2008
AGOSTI 26,2008 Wabunge wamzomea Mugabe.
Wabunge wa chama kikuu cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe wamezomea Rais Robert Mugabe alipofungua rasmi bunge miezi mitano baada ya uchaguzi uliokuwa na utata.
Wabunge hao walihanikiza kwa kupiga makelele wakati Bwana Mugabe, alipokuwa akiorodhesha mafanikio ya serikali yake "Umeua watu, kamwe hatutakusahau"
Mwanzo wa hutuba yake, Bwana Mugabe amesema kuna matumaini makubwa mazungumzo ya kugawana madaraka yatafanikiwa.
Upande wa upinzani ulitaka bunge lisifunguliwe hadi mazungumzo yaliyokwama yatakapopatiwa ufumbuzi.
Awali chama cha MDC kilitishia kususia hutuba ya Rais Mugabe, kwa vile hawautambui utawala wa Mugabe.
Kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Machi, chama cha Mugabe cha Zanu-PF kilipoteza wingi wa viti bungeni kwa mara ya kwanza tangu Zimbabwe ilipopata uhuru mwaka 1980.
Katika hutuba yake Bwana Mugabe ameeleza kusikitishwa na vurugu za kisiasa zilizotokea wakati wa uchaguzi mwaka huu na kuvitupia lawama vyama vyote vya siasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
wanasema mwisho wa ubaya ni aibu.Ndiyo yanayomkuta huyo dikteta.
Viongozi wa afrika wajifunze kwa zimbabwe
Post a Comment