Saturday, August 9, 2008

AGOSTI 9,2008 MIMI YASINTA

Leo, kuna jua kidogo nimeamka nimevaa nguo zangu za mazoezi na kuanza kukimbia baada ya kukimbia kidogo mvua hiyo lakini kwa vile nilishaamua kukimbia basi nimeendelea nimekimbia kilimeta 5. Ila sasa nimerudi na natetemeka kama kifaranga cha kuku. Nataka nifanye mazoezi ili niiwakilishe Nchi yangu Tanzania kwa jinsi ninavyoipenda. Mnajua hii hali ya hewa ya hapa inaniuzi sana kwani kila siku hali nyingine leo jua kesho mvua keshokutwa baridi na hata pengine theruji hakuna msimamo. Kwa hiyo kama hujitosi tu kukimbia au kuwa mstuni labda kutafuta uyoga au matunda basi utabaki ndani ya nyumba siku hadi siku.

Mnajua leo nimekumbuka sana nyumbani kwa hiyo nimeamua kupika ugali na mchicha pia maharage. Nimeukanyaga kweli lakini hata hivyo haitoshi kwa hiyo nimeamua kusikiliza mziki.

5 comments:

Anonymous said...

Sasa hujafafanua kwamba umeamua kuiwakilisha nchi yako kwenye mbio gani, maana hata mbio zenyewe ukimbia peke yako bila mtu wa kushindana naye, halafu hutatuambia je, hizo km 5 umekimbia kwa muda gani isije ukawa umetumia masaa 2.
Hata hivyo nakupongeza sana dadangu kwa kuwakilisha nchi kwa hizo km 5 maana najua hilo ni zoezi muhimu sana kujiweka fit na kuwa na umbo zuri, safi sana huo ni mfano wa kuigwa na akina dada wengi au akina mama wengi.
Hongera sana

Yasinta Ngonyani said...

Asante kaka Lazarus Ni kwamba nitakimbia meta 5000 kwa kutumia dakika 14 na sekunde ishirini km 5

Anonymous said...

Siamini na sikubali,
Kijiji kizima mimi ndo mkimbiaji na najua wewe nakuacha mbali kabisa ila huwa nakimbia mita 5,000 kwa dakika 14 na sekunde 30 iweje wewe unishinde,
Najiandaa nije Sweeden tuwe na olympic yetu naanza kutafuta wadhamini.
Sikubali kabisa na siamini hadi nione kwa macho.

Anonymous said...

Aisee kweli mnanichekesha sana ndiyo raha ya kijijini watu mnakuwa pamoja muda wote.Nimeiangalia picha ya dadangu halafu hizo dakika 14 na sekunde 5 nikasema hii sasa amemshinda hata Bolt yule jamaa wa Jamaika mwenye kasi kuliko binadamu wote,nikamkumbuka pia yule Powell mpinzani katika mbio za mita 100,nimecheka sana. Sasa nawaambia hamniwezi mimi natumia dakika 14 bila sekunde....msiniulize swali kazi kwenu njoooni nyasa muone...

Yasinta Ngonyani said...

Usitudanganyw kaka mpangala dakika 14 tu. sikubali basi nitazidi kufanya mazoezi iwe dakika 10. vipi uliona nimezeeka au yaani katika picha