Mwenzenu nahisi kuchanganyikiwa. Labda kwa sababu nina tamaduni/mila na desturi mbili najua mimi ni mtanzania na najua mila na desturi pia utamaduni wangu. Lakini sasa kichwa/akili yangu imevurugika kabisa:-
Ni hivi najua nyumbani TZ ni kawaida au labda niseme safi kama mtu umenenepa/nawili. Nakumbuka mwaka wa kwanza niliporudi TZ kusalimia watu walishtuka/shangaa sana na kuzani nilikuwa na ngoma au. Na baada ya miaka kadhaa nikarudi tena na wote walifurahi na kusema ya kwamba hivi ndiyo inavyotakiwa, wao walisema ya kwamba nilipendeza yaani niliongoza kilo kidogo nilinenepa. Na niliporudi hapa watu walisema eeh? Mbona unanenepa sana si vizuri inabidi upungue. Sasa nadhani mmegundua kwa nini nimesema nimechanganyikiwa. Ngoja niendelee kidogo kiundani au niseme kiafya nakubaliana na "waswidi" wazungu, lakini hali hii inanipa hofu kidogo kwani sasa hata watoto wadogo wanafuata mwenendo wa wazazi na marafiki pia, wanajinyima kula. Na wengine wanakula kama kawaida na baadaye wanatapika makusudi. Mnajua wanasemaje, eti wanataka kuwa wembamba, ndiyo wanapendeza. Lakini ukiwaangalia wanaonekana kama mti hata matako (wowowo) hawana.
Ndiyo najua kunenepa sana sio safi kwani kuna madara yake kama vile mshtuko wa moyo(heart attack) daibetes nk.
kama nilivyosema hapo juu mara nyingi sijui mimi ni nani na nchi gani ni yangu. ndio maana nimesema nimechanganyikiwa. Watanzania (waafrika) wanaona kunenepa ni safi na wazungu wanasema ni hatari, Na najua hakuna anayesema kweli au uongo. Je wasomaji mnasemaje Nisaidieni kidogo!!!!!!!!!
2 comments:
aaaaaa acha nicheke mimi kwani wewe unaogopa wowowowowowo????/ujua kuwa na wowowo siyo vizuri utakuta mtu anauzito ambao anadharau au kujifanya hajui kama ni hatari kwa maisha yake.Ni hivi wewe angalia afya yako unataka iweje siyo hao wanataka uweje,lakini paoa dadangu si uanjua wabongo wanafagilia wowowmo lakini angali shem atakubwaga ukiwa mnene sana.
wewe unajuaje kama mimi nimeolewa? na kama nina wowowo?
Post a Comment