Wote tunakumbuka/tunajua kuwa:-
Wakati wa ukoloni elimu ilikuwa ni ya wachache walioteuliwa tu.
Lengo kubwa la taratibu za elimu ya wakoloni ni kuzalisha makarani na wasaidizi wa utawala wa kiingereza.
Mara tu baada ya Uhuru mwaka 1961 taratibu za elimu zilibadilishwa ili kufuata mazingira na mahitaji ya watanzania ambao karibu 90% waliishi vijijini na mikoani. Kiingereza kilikuwa ndiyo lugha iliyotumika kufundishia wakati ule wa utawala wa kikoloni.
Kiswahili kilianza kutumika katika shule za msingi mnamo mwaka 1969. Matokeo ni kwamba vitabu vya masomo kwa kiswahili vilikuwa vichache.
Kwa vile wakoloni walitawala basi Tanzania kwa muda mrefu ilikuwa bado ingali katka hali mbaya ya uchumi, haikuwezekana kufanyika mengi. Katika baadhi ya mashule, walimu walikuwa wanawaalika wazee waje kusimulia watoto hadithi na visa vya kale. Wazee walitambuliwa kama maktaba na hazina ya ujuzi uliojengeka kwa mila za masimulizi.
Tanzania ina makabila karibu 129 mbalimbali ambayo kati yao kuna lugha na mila mbalimbali tofauti sana. Kwa hiyo kukusanywa kwa hadithi toka makabila hayo yote na kufasiriwa kwa kiswahili, kumefanya hadithi ziwe ni msingi mmoja wa mila na utamaduni wa kitanzania. Tutumaini hadithi zote zilizosimuliwa na wazee wetu zimehifadhiwa la sivyo tutakuwa tumepoteza utajiri mkubwa wa mila na ujuzi kupotea.
kumbukumbu kutoka:- kitabu cha hadithi na visa kutoka Tanzania
1 comment:
mmm hapa nilipo nasoma hadithi iitwayo 'msako wa hayawani' ilitungwa na Eddie Ganzel,pia kitabu kingine cha 'makuadi wa soko huria' sijakimaliza,lakini kile cha 'mpe maneno yake'cha Fred Macha nimeshakimaliza. Yaani wabongo kusoma riwaya imekuwa adimu sana wengi wanapenda hadithi za mahaba za magazetini tu na hatutaki kusoma hata vitabu vingine kuimarisha lugha yetu na kustawisha ubongo huku tukijifunza maisha
Post a Comment