Maisha ni mtihani, kwa vile watu wengi hufeli kwa sababu wanajaribu/tunajaribu kukopi/kuiga maisha ya wengine. Tunasahau ya kwamba kila mmoja ana mtihani wake.
NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA MWEZI HUU WA KUMI!
Monday, October 31, 2016
Thursday, October 27, 2016
HILI NI CHAGUO LA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII IWE NI PICHA YA WIKI HIII...
Ebu angalia hii picha unafikiri utaweza tu kupita hapa bila kusimama na kununua vitunguu au tu hata kuongea na watu....Binafsi nimependa sana mwonekano wa hii picha...MNAPENDWA WOTE NA KAPULYA:-)
Wednesday, October 26, 2016
JE? UNAKUMBUKA KITABU HIKI CHENYE HADITHI YA JUMA NA ROZA?
Tia maziwa
Tia sukari
Roza ana kiu
kunywa chai Roza"
AU HII HADITHI YA MWANASESERE
Nimekikumbuka sana hiki kitabu wale wenye umri sawa nami watakuwa pia wanakumbuka ....hivi vitabu siku hizi havipi kabisa ...TUPO PAMOJA...
Tuesday, October 25, 2016
MAISHA NI KAMA KITABU...
Maisha ni kama kitabu, kuna kurasa nyingine ni za kusikitisha, nyingine za kufurahisha na nyingine kusisimua. Lakini usipofungua hizo kurasa kamwe hutaweza kujua ni nini kipo kwenye hizo kurasa zifuatazo.
SIKU NJEMA
Sunday, October 23, 2016
Thursday, October 20, 2016
ZILIPENDWA. ..UTAMU WA MAJI YA MTUNGI AUJUE NI KATA
Hakika leo nimekumbuka mbali sana...ilikuwa kila baada ya siku mbili ni lazima kuchemsha maji na kuyachuja kwa kitambaa safi cheupe na kuyaweka mtungini kwa ajili ya kunywa. Nitaikumbuka milele domestiki hii niliyofundishwa na mpendwa MAMA yangu.. .SIKU NJEMA KWA APITAYE HAPA!
Tuesday, October 18, 2016
TUSIWE WATU WA KUSAHAU MARAFIKI MAANA SIKU MOJA UTAWAHITAJI
RAFIKI NI BORA KULIKO MWANASESERE
Nimekaa hapa huku nikiwa na mawazo mengi katika kichwa changu...najiuliza:- Hivi ni lini nitapata fursa ya kukutana na baadhi ya marafiki zangu? Hii ingekuwa fursa murwa kwangu kukutana tena baada ya muda mrefu kupoteana na kusikia maisha yao, familia na kuhusu kazi zao. Muhimu zaidi kwangu ingekuwa kupata fursa ya kuonana na wao pia kuongea mawili matatu kwa nia ya kubadilishana mawazo. Kwani ni vyema sana kuwa na marafiki wanaokujali na unaowajali katika shughuli za kila siku za kimaisha. Tukumbuke, baadhi yetu marafiki ni kama funguo ya maisha. Inawezekana kazi uliyo nayo , mke/mume uliyo nayo nk umepata kwa kupitia rafiki. Kwa hiyo, tusiwe watu wasio wajali marafiki hasa wale wa muda. Binafsi nimepoteza marafiki wengi sana wale wa kitambo...jambo ambalo natamani siku moja tuonane tena katika utu uzima huu. Ndugu zanguni kama mna marafiki ambao hakuona umuhimu wao jaribu kuwatafuta . Katika maisha ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukutana na watu mbalimbali na mwisho mkawa marafiki wa kupendana zaidi ya ndugu uliyezaliwa naye tumbo moja. Pia tuwe na tabia kuchukua fursa kukutana na marafiki ili kujenga na kudumisha urafiki wetu maana mwisho wa siku utakuwa faida. Ila isiwe tu pale kwenye shida ndiyo urafiki, hapana...ni vyema kujuliana hali kila wakati huku tukitakiana maisha mema hasa pale tukosapo muda wa kukutana. Maana katika maisha hakuna asiyependa kukumbukwa. Nadhani wengi wengi wetu tumekwisha wahi jiuliza:- kama ungependa kusahaulika na marafiki/watu wa karibu wako? nadhani jibu unalo....
Monday, October 17, 2016
NI JUMATATU NYINGINE NA WIKI MPYA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA IANZA KWA MTINDO HUU...MAMBO MAHIMU KATIKA MAISHA AMBAYO YAPASWA TUYAZINGATIE....
Katika maisha kuna vitu/mambo saba ambayo wote tunapaswa kuyajua... nayo ni kama yafuatayo :-Furaha, karaha, misukosuko, majonzi, migogoro, mikasa na chuki.
Haya yote husababishwa na viumbe hai kama mimi na wewe, ili kiyashinda haya yatupasa tuwe na mambo nne(4) nayo ni:- Subira, uelewa, uvumilivu na msamaha. Lakini pia katika maisha yako uwe karibu sana na mambo haya manne :- msimamo, mkweli, ujasiri na Imani na halafu epuka sana mambo haya matano yafuatayo: Udanganyifu, uchoyo, ubinafsi, wizi na ufitina
WAZAO LA LEO:- Kumbuka kumjali anayekujali hata kama yupo mbali nawe. Mpende anayekupenda hata kama hana kitu jali utu kuliko kitu.
NAWATAKIENI SIKU NJEMA
Friday, October 14, 2016
ZILIPENDWA KWELI NI TAMU...VAZI LA MAUA-MAUA NA MKANDA JUU....
Nimekumbuka sana zamani...ebu angalia hii picha. Sijui ilikuwa ni mtindo kusimama kwenye miti au maua..? Maana nimejiuliza hata jibu sijapata. Je? mnamfahamu huyu mdada?
IJUMAA NJEMA KWA ATAKAYEPITA HAPA!
IJUMAA NJEMA KWA ATAKAYEPITA HAPA!
Thursday, October 13, 2016
JIPE MOYO KAMWE USIKATE TAMAA KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA
"Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa shule. Nilipokaa, nilimuuliza kijana mmoja juu ya matokeo ya mchezo. Kwa tabasamu, alijibu "Wako mbele yetu 3-0"! Nikasema, Kweli!! Mbona huonekani kukata tamaa.
"Kukata tamaa? "Yule mvulana aliuliza kwa mshangao.... Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho? Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda! Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele! Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa,mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; nilipenda alivyojiamini ; Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi.
"Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?" Maisha ni kama mchezo. Kwanini ukate tamaa wakati Mwenyezi Mungu ndiye meneja wako? Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako? Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa? Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho. Lakini madamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.
Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.
Usijipulizie kipenga chako cha mwisho wewe mwenyewe.
UJUMBE- Maisha ni changamoto ambapo pia ni kama mchezo...twapaswa kuwa jasiri na kujiamini.
Wednesday, October 12, 2016
LEO TWENDE NA ZILIPENDWA - SHAURI YAKO
JE? UNAUKUMBUKA HUU PIA KASONGO
NIWATAENI SIKU NJEMA ...KUMBUKENI TUPO PAMOJA.
Tuesday, October 11, 2016
Monday, October 10, 2016
TUANZE WIKI HII NA KUTEMBELEA KWETU UNGONINI SONGEA NA VITU VYAO VYA ASILI
Kitanda cha ngozi
Na hapa ni NGOMA
Upitapo Songea.Karibu sana katika nyumba ya makumbusho utapenda...
Friday, October 7, 2016
NIMEKUMBUKA ZILIPENDEA...JUMAA NJEMA!
Jamani tukimbie tutachelewa ....nakumbuka jinsi tulivyokuwa tukipata viboko kwa ajili ya kuchelewa shule....
Tuesday, October 4, 2016
SAMAKI WA NYASA ....CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA WENU:-)
Monday, October 3, 2016
KILIMO CHA PILIPILI NA VINGINEVYO KWA KUTUMIA MAKOPO
Hapa ni pilipili mbuzi
na hizi zinafanana ila ni kubwa kidogo
Hapa ni pilipili hoho tayari kwa kula sasa:-)
Hizi pilipili zinafanana na pilipili hoho..yaani hazina makali sana kama kichaa na mbuzi
Na hapa ni nyanya maana huwezi kula pilipili tu hasa kwa kachumbali nk
Na mwisho zileee zabibu zetu nazo zimeiva na sasa ni raha tu...kwa hiyo ndugu zanguni karibuni tule pamoja ...si mnajua ule msemo usemao kulima mmoja ila kula wengi.... JUMATATU NJEMA!
Friday, September 30, 2016
TUMALIZE MWEZI HUU WA TISA NA BURUDANI YA NGOMA YA ASILI YA MGANDA KUTOKA LUDEWA
Wiki, mwezi ndo unaisha sasa hivi utastukia mwaka pia umeisha. Nahisi wote mwezi huu unaisha mkiwa na afaya njema. Binafsi nipo salama...Haya tuendelee na hiyo ngoma stepu yako wee moja mbili tatu....usisahau mkia na kipenenga.... mwisho wa juma pia mwezi uwe mwenye amani na upendo...Kapulya
Thursday, September 29, 2016
SEHEMU FULANI AFRIKA/TANZANIA ....JE? UNAJUA NI WAPI?
Kuna sehemu katika nchi yetu ukipita huwezi kupita tu unatamani ushinde hapo angalao tu kwa masaaa kadhaa...Je? wajua hapa ni wapi ?:-)
Tuesday, September 27, 2016
UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU!!!
Sio wakati wote mtu mwenye furaha huwa mwema. Lakini kila wakati, mtu mwema mara zote huwa na furaha.
Kila la kheri. UPENDO DAIMA!
Kila la kheri. UPENDO DAIMA!
Monday, September 26, 2016
WIKI HII TUANZE NA MAPISHI AMBAYO WENGI TUMEPIKA NA KUKULIA....NIMEKUMBUKA SANA MAPISHI HAYA YA KUTUMIA MAFIGA MATATU...
Kwenye chungu ni makande, wakati ukisubiri makande yaive basi ni mtindo mmoja tu kuchoma mahindi....Na ujuavyo chakula cha kupikia kwenye chungu kinavyokuwakitamu.....
Saturday, September 24, 2016
JUMAMOSI NJEMA ....KARIBUNI CHAKULA AKIPENDACHO KAPULYA...............!!
Nimeukumbuka LUNDO -NYASA kwetu kule Mbamba bay ugali wa muhogo na dagaa na ukikosa dagaa samaki ....mmmhhhh naweza kusema ndicho chakula nikipendachona kilichonikuza....
JUMAMOSI NJEMA.
JUMAMOSI NJEMA.
Thursday, September 22, 2016
Tuesday, September 20, 2016
PALE MTU UNAPOPATA ZAWADI AMBAZO NI MAALUMU NA NI AMBAZO ZIMETENGENEZWA KWA UMAKINI
ZAWADI HII NILIPATA MWAKA JUZI TOKA KWA KAKA MASAWE...
NA JUZI TU NIMEPATA HII KWA KAKA MDOGO BATHOLOMEW TOKA UMASAINI:-) Ni furaha ilioje kupata zawadi hizi. Hii ya pili imetengenezwa na mikono ya mama yake Batholomew mwenyewe. Vitu vya kitamaduni safi sana...Ahsante mama.
Monday, September 19, 2016
TUANZE JUMATATU HII NA PICHA HII..KWELI HUU NI UUNGWANA?
Hebu angalia huyo mama, yaani sasa badala ya kubeba mtoto mgongoni amebeba kuni na mtoto tumboni. Halafu huo mzigo wa kuni ni bonge la mzigo na ukiangalia kwa pembeni kabania na mboga majani ....Ila mimi nina swali kwa nini asingebeba hizo kuni kichawani ?Na hapo nadhani akifika nyumbani ni kwenda kuteka maji au kutwanga pia. Hakika hapa ndio pale tunapotakia kuwa na usawa....tujadili pamoja
Sunday, September 18, 2016
SALA YANGU YA JUMAPILI YA LEO...TUSALI KWA PAMOJA...
Ee Mwenyezi Mungu, mikononi mwako niguse kama ulivyo waguse vipofu wakaona. Bariki familia yangu, nyumba yetu, rafiki zangu, kazi yangu. Utupe riziki, wepesi wa maisha ya hapa duniani. Ee Mungu usikie maombi yetu. AMINA. JUMAPILI NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA!!
Subscribe to:
Posts (Atom)
















