RAFIKI NI BORA KULIKO MWANASESERE
Nimekaa hapa huku nikiwa na mawazo mengi katika kichwa changu...najiuliza:- Hivi ni lini nitapata fursa ya kukutana na baadhi ya marafiki zangu? Hii ingekuwa fursa murwa kwangu kukutana tena baada ya muda mrefu kupoteana na kusikia maisha yao, familia na kuhusu kazi zao. Muhimu zaidi kwangu ingekuwa kupata fursa ya kuonana na wao pia kuongea mawili matatu kwa nia ya kubadilishana mawazo. Kwani ni vyema sana kuwa na marafiki wanaokujali na unaowajali katika shughuli za kila siku za kimaisha. Tukumbuke, baadhi yetu marafiki ni kama funguo ya maisha. Inawezekana kazi uliyo nayo , mke/mume uliyo nayo nk umepata kwa kupitia rafiki. Kwa hiyo, tusiwe watu wasio wajali marafiki hasa wale wa muda. Binafsi nimepoteza marafiki wengi sana wale wa kitambo...jambo ambalo natamani siku moja tuonane tena katika utu uzima huu. Ndugu zanguni kama mna marafiki ambao hakuona umuhimu wao jaribu kuwatafuta . Katika maisha ni vizuri kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kukutana na watu mbalimbali na mwisho mkawa marafiki wa kupendana zaidi ya ndugu uliyezaliwa naye tumbo moja. Pia tuwe na tabia kuchukua fursa kukutana na marafiki ili kujenga na kudumisha urafiki wetu maana mwisho wa siku utakuwa faida. Ila isiwe tu pale kwenye shida ndiyo urafiki, hapana...ni vyema kujuliana hali kila wakati huku tukitakiana maisha mema hasa pale tukosapo muda wa kukutana. Maana katika maisha hakuna asiyependa kukumbukwa. Nadhani wengi wengi wetu tumekwisha wahi jiuliza:- kama ungependa kusahaulika na marafiki/watu wa karibu wako? nadhani jibu unalo....
No comments:
Post a Comment