Wednesday, October 3, 2018
TANGU WAKIWA WADOGO HUPENDA KUJITUMA, LAKINI JAMII HAIWAAMINI
Wiki hii tuanze na picha hii..yaani kama ujumbe usemavyo hapo juu....NAPENDA KUWATAKIENI WIKI NJEMA NA PIA JUMATANO NJEMA....KAPULYA WENU!!
Thursday, September 27, 2018
LIJUI TUNDA LA PAPAI NA FAIDA ZAKE KWA AFYA......
Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha.
Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.
Wiki mbili zilizopita tumeona vyakula kama karanga, korosho vinavyoweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, wiki hii pia tunaona papai nalo limo kwenye orodha ya vyakula vinavyotoa kinga ya ugonjwa huo.
Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.
HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonyesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.
KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.
KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya âbeta-caroteneâ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k
NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.
TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.
CHANZO JAMIIFORUMS:- AHSANTE SANA KWA ELIMU NAMI NIMEONA NISIELIMIKE PEKE YANGU NIKAONA NIWEKE HAPA KINARAZANI.

Friday, September 21, 2018
NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...HAYA TUFURAHI PAMOJA NA KIPANDE HIKI CHA NGOMA...
Tuwukeee tuwukeee kamwimbo katamu sana. Natamani kuungana nao na kucheza ila nabaki kucheza peke yaangu....NAWATAKIENI MWISHO WA WIKI HII UWE WENYE FURAHA NA AMANI! KAPULYA WENU
Thursday, September 20, 2018
PALE UNAPOLIMA UNATUMAINA KUVUNA NA SASA MATOKEO TUNAYAONA
Hapo mwaona baadhi ya mazao niliyovuna nyanya, tikiti maji ambalo ndani ni njano tamu sana, zabibu na pia mwaona kwa pembeni ni pilipili ni raha sana kula vyakula ulivyolima mwenyewe kwa mikono yako. KARIBUNI TULE NDUGU ZANGU.
Monday, September 17, 2018
Thursday, September 13, 2018
FAHARI YA MKULIMA NI KULIMA NA KULA ALICHOVUNA....KAZI YA MIKONO YAMGU...
kula vyakula unavyopanda mwenyewe ni kwamba ule utamu unazidi...nilipanda hili tunda aina ya tikiti maji lakini lenyewe ni la njano ndani ha picha hapo chini yaonyesha vizuri zaidi. Nilianza kulifuatilia hili tunda kwa ukuaji wake kama uonavyo ua
Na sasa lishakuwa kubwa yaani ni kama boga ila bado kukomaa ni kwamba ukomaaji wake ni mpaka hili ganda liwe njano njano....Na leo siku rasmi ya kuvuna na kula. Utakula ulichopanda, hakika najisikia fahari sana ....
Tuesday, September 11, 2018
UJUMBE WA JUMANNE YA LEO KUTOKA KWANGU KUJA KWENU...
Hata siku moja usijaribu kukata TAMAA. Dharau, matusi na kebehi: havimzuii mtu kungára.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA...KAPULYA WENU.
Monday, September 3, 2018
TUANZE MWEZI HUU WA TISA NA WIKI YAKE YA KWANZA KIHIVI .....
Nikiangalia hawa watoto warukapo kamba natamani siku, miaka irudi nyumba ili nami niweze kuruka tena ...UJUMBE:- WAACHENI WATOTO WAWE WATOTO.
Wednesday, August 29, 2018
PENDEZA KWA UBUNIFU WA KITANZANIA
Umuhimu wa kupendeza uko wazi kwa kila mtu,mara nyingi mavazi yamekuwa kama kipimo cha utanashati,basi ili kuongeza mvuto yafaa kuongezea vitu vya pekee vilivyotengenezwa kwa ujuzi wa kimasai ili tu kuonyesha utofauti kimitindo na utanashati..
Monday, August 27, 2018
MIMI NDIO NILIMUA BATA MZINGA KWA BAHATI MBAYA
KATIKA PITAPITA ZANGU NIMEKUTANA NA HILI FUNZO NIKAONA NIWEKA HAPA ILI NA WENZANGU MUWEZE KUSOMA NA KUJIFUNZA KARIBUNI:-
Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lakini ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama. Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama msafiri amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya.
Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama. Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena msafiri amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama.
Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia..
"Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mimi ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe.
Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena.
FUNZO,
Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe.
*MUNGU ATUSAMEHE DHAMBI ZETU NA ATUWEKE HURU...*
Sunday, August 26, 2018
JUMAPILI YA LEO TUWE PAMOJA KWA MAOMBI NA HII NI SALA YANGU
Ee Mungu wajua sababu ya mimi kuendelea kuwepo kwenye uwepo wako, naomba uendelee kunijalia hekima na busara katika kukabiliana na majaribu mbalimbali maana wewe ndiye wajua leo yangu na kesho yangu itakavyokuwa.
AMINA
AMINA
Friday, August 24, 2018
Wednesday, August 22, 2018
TUFANYE HII IWE PICHA YA SIKU
Leo ni Jumatano iliyochaguliwa nami Kapulya kuweka picha hii iwe picha ya siku. NAWATAKIA SIKU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA.
Sunday, August 19, 2018
Monday, August 13, 2018
NAWATAKIENI JIONI NJEMA YA JUMATATU HII KWA KUANGALIA NGOMA YA ASILI YA KINGONI
UJUMBE WA LEO:- Tusisahau utamaduni wetu ndugu zanguni, binafsi napenda sana uasili.JIONI NJEMA WANDUGU. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA.
Tuesday, August 7, 2018
NI WIKI NYINGINE TENA NDANI YA MWEZI HUU WA NANE... NA HII NI PICHA YA WIKI
Napenda kuwatakieni mwanzo mwema wa hili juma na furaha itawale mioyoni mwenu. Tutaonana tena panapo majaliwa.
Wednesday, August 1, 2018
TUANZE WIKI HII MPYA YA MWEZI HUU MPYA WA NANE KWA KUANZA NA KUSHIRIKIANA KULA CHAKULA HIKI
Tuesday, July 31, 2018
LEO TUANGALIA /SIKILIZE NYIMBO/NGOMA ZETU ZA ASILI
Huwa napenda sana kuangalia au kusikiliza ngoma/nyimbi wa asili . Kwa hiyo nimeona niwashirikishe na wenzangu
Monday, July 23, 2018
JUMATATU YA LEO TUANGALIA BAADHI YA VYAKULA NILIMAVYO/KAZI YA MIKONO YANGU
Hapa ni kama itakuwa vizuri basi litakuwa tango....
.....na ni matembele ...kama huna ardhi kutosha basi hii ni njia nzuri kupata chakula
Thursday, July 19, 2018
EBU LEO TUANGALIE UTENGENEZAJI WA TOGWA....
UTENGENEZAJI WA TONGWA
UNYWAJI WA TOGWA KUTUMIA KIKOMBE AU KATA. JE? WEWE UNAPENDA KUTUMIA KIKOMBE AU KATA?
Wednesday, July 18, 2018
Tuesday, July 17, 2018
WIKI HII TUANZE NA KWETU NYASA ...KUMBUKUMBU
Kiukweli leo nimekumbuka sana NYASA/LUNDO kwetu nilikozaliwa kwenda tu ziwani unapata samaki, dagaa na hata likungu. Naona fahari sana kuzaliwa Kando ya ziwa nyasa, Unajua samaki wanaotoka tu kuvuliwa wanavyokuwa watamu wewe acha tu... Niwatakieni JUMANNE NJEMA. WOTE MNAPENDWA. Kapulya!
Tuesday, July 10, 2018
LEO TUTEMBEE KANISA KONGWE LA MKOA WA RUVUMA-PERAMIHO
Hilo hapo juu ni kanisa lililo jengwa Peramiho na Wamisionari wa kikatolic miaka mia moja iliyo pita lakini mpaka leo halijanyiwa ukarabati wowote ,pamoja na kanisa hilo ipo saa ambayo nayo ina chukua miaka 100 bila kutengenzwa wala kurekebishwa
Monday, July 9, 2018
WIKI HII TUANZE NA KUANGALIA BUSTANI YA KAPULYA.... JUMATATU NJEMA WANDUGU TUPO PAMOJA
mchicha
Mboga ya maboga
Vitunguu, Mahindi na Viazi
Nyanya. Kutokana na uhaba wa sehemu basi nimetumia makopo
Wednesday, July 4, 2018
2/7 NI KUMBUKUMBU YA NDOA YETU IMETIMIZA MIAKA 25
2/7/ ilikuwa siku ya furaha kwetu ni miaka 25 ya ndoa yetu
Ni chakula cha jioni ile nyama ya ngòmbe na viazi pia kinywaji. Twamshukuru Mungu kwa safari hii ndefu.
Subscribe to:
Posts (Atom)