Friday, May 29, 2015
NI IJUMAA YA MWISHO YA MWEZI HUU WA TANO MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIA MWEZI UJAO UWE MWEMA ---EBU SIKILIZA KIPANDE HIKI CHA MZIKI HATA KAMA HUELEWI..
IJUMAA YA MWISHO YA MWEZI HUU WA TANO IWE NJEMA SANA KWA WOTE:-)
Thursday, May 28, 2015
LEO NA WANGONI WETU HAPO KALE!!
pPicha ya leo /wiki ni hii hapa....ni ndugu zetu wangoni hapo kale...nimependa mavazi yao ...PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA :-) KAPULYA...
Wednesday, May 27, 2015
LEO NIMEAMKA NA HAMU YA EMBE KWELI...KWENDA DUKANI ETI EMBE MOJA BEI YAKE ...
Ni 2640, duh nikakumbuka nyumbani Ruhuwiko nina miembe na mpaka kuna wakati natupa maembe au nalisha nguruwe...Mmmmmhhh maisha haya kaziiiii kwelikweli.... JUMATANO NJEMA KWA WOTE!!
Sunday, May 24, 2015
Thursday, May 21, 2015
CHAGUA LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HIZI PICHA ZIWE ZA WIKI: JE? UNAIKUMBUKA PICHA HII? NA JE? NI UBUNIFU AU?...
Nilitumiwa picha hii na msomaji wa Maisha na Mafanikio 2012kwanza nikashikwa na butwaa, na pili nikajiuliza ni ubunifu? Na tatu nikajiuliza kukosa mtu wa kumtunza mtoto au chekechea? Nawaachia mwenzangu tusaidiana kujadili hapa...Duh! ila sidhali kama mtoto huyo anapata raha hapo.....MCHANA MWEMA MAJEMANI!!!
NA LEO NIMETUMIWA HII HAPA
Kwa mimi naona afadhali ya hapa mtoto anapata raha kidogo maana ni mto ila huu mti, Duh ...Je? Na huu ni ubunifu? KILA LA KHERI PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!
Wednesday, May 20, 2015
KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BIBI YETU VALERIANA NGONYANI -MBAWALA!!!
KUONANA NA BIBI 2005 MWEZI WA NNE
Leo ni tarehe 20/5 ni miaka kumi imepita tangu bibi yetu mpendwa Valeriana Ngonyani-Mbawala atutoke. Kwangu ni kama vile jana tu. Alifariki 20/5/2005 katika hospitali ya Liuli. Sisi wajukuu wako wote, watoto wako ndugu na marafiki wote wanakukumbuka daima. Bibi Valeriana ni huyo aliyejifunika kitenge, katikati nadhani mnajua au basi ni mimi na mwishoni ni mama yangu mdogo, mdogo wake mama. TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA NJIA YA SALA ZETU. USTAREHE KWA AMANI AMINA. Na hapa naweka na huu wimbo kwa ajuli ya akina bibi wote walio hai na waliotutangulia ..........
TUWAOMBEE BIBI ZETU!
TUWAOMBEE BIBI ZETU!
Tuesday, May 19, 2015
PICHA KUTOKA KITABU CHA DARASA 5 TUJIFUNZE LUGHA YETU! KWA DARASA LA NNE...
Na kitabu chenyewe kinaonekana hivi kwa nje....Picha ya kwanza ni hadithi ya jogoo aliyesema, ya pili ni Sadiki na Sikiri, ya tatu nimesahau sijui kuna anayekumbuka anisaidie?.ya nne ni Sizitaki mbichi hizi
Monday, May 18, 2015
JUMATATU YA LEO NIMEKUMBUKA HAPO ZAMANI NIKIWA NA UMRI KAMA HAWA WASICHANA....
Nachotaka kusema ni kwamba watoto wa siku hizi hawawezi kazi kama hizi, yaani kuchota maji, Kutwanga, kupika chakula wala hata kuwaangalia wadogo zao wazazi wawapo shambani. Yaani najiona kama ni mimi huyo mwenye ndoo ya kijani. Kizazi cha zamani/enzi hizo watoto walikuwa wakakamavu na wenye afya njema, ila watoto wa kizazi cha sasa ni walegevu mno
Saturday, May 16, 2015
SASA TUNAANZA NA ILE BUSTANI YETU....RASMI NIMEANZA LEO FUATANA NAMI KUONA MAENDELEO...
Kama unaona kijana kijana ni vitunguu saumu ambavyo nilipanda mwaka jana vimekuwa tosha kula..:-)
Ni raha ilioje kuanza tena kulima bustani..maaana mikono ilikuwa inawasha sana ..nimepatika mchicha, chainizi, figiri mboga maboga nk. Ni Kapulya wenu ------
Ni raha ilioje kuanza tena kulima bustani..maaana mikono ilikuwa inawasha sana ..nimepatika mchicha, chainizi, figiri mboga maboga nk. Ni Kapulya wenu ------
Thursday, May 14, 2015
MAPISHI:- LEO KATIKA KUSOMA SOMA NIMEKUTANA NA MAPISHI HAYA....
Ni kuku mzima ambaye nimempaka viungo na halafu nimemweka juu ya kopo la bia na na halafu nimemchuma. Nyama yako ilikuwa tamu sana. Jaribu na wewe nakwambia utajiuma...unaweza kula na wali, viazi au ugali, mimi nilikuta na kachumbali/saladi. Siku na Jioni njema. Kapulya:-)
HIVI NDIVYO WALIVYOKUWA WAKIJIKINGA MABABU ZETU HAPO KALE KWA HATARI
Tusisahau vyetu vya asili. Tuwasimulie na vizazi vyetu ilikuwaje. Huwa najiuliza je hizi picha zimehifadhiwa sehemu nzuri kama makumbusho vile ili tuweze kuwapeleka watoto/vizazi vyetu kuangalia? au Je tunavyo nyumbani? binafsi nina ngao na mkuki:-) ...Lol
Wednesday, May 13, 2015
HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO :- PICHA YA WIKI
Mbuzi wameamua kupanda mpaka juu kabisa maana huko ndiko chakula kipo...Sijui ningeweza kufanya hivyo?
Sunday, May 10, 2015
NACHUKUA FURSA HII KWA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA.:- UHAI WA BINADAMU- UWEZO WA KUFIKIRI...
Kutokea kwa binadamu ulimwenguni ilikuwa hatua kubwa mpya ya kwenda mbele, badiliko kubwa ajabu. Sasa siyo nguvu na uhai tu vilivyokuweko bali kulikuwa na uwezo wa kufikiri pia. Binadamu alikuwa na akili. Katika binadamu uhai uliweza kujitambua wenyewe kuwa unaishi.
Katika hatua hii Mungu alikamilisha kazi yake ya kuumba. Kwa milioni nyingi za miaka Mungu alikuwa akiugawia ulimwengu nguvu yake, akiushirikisha katika uhai wake. Sasa kumbe, ameushirikisha katika uwezo wa akili yake, uwezo wa kujitambua yeye mwenyewe. Na binadamu pia amefanywa kuweza kujitambua yeye mwenyewe, na kumjua Mungu.
Chanzo, kitabu:- Njia yetu kwa mapendo na ndoa.
Katika hatua hii Mungu alikamilisha kazi yake ya kuumba. Kwa milioni nyingi za miaka Mungu alikuwa akiugawia ulimwengu nguvu yake, akiushirikisha katika uhai wake. Sasa kumbe, ameushirikisha katika uwezo wa akili yake, uwezo wa kujitambua yeye mwenyewe. Na binadamu pia amefanywa kuweza kujitambua yeye mwenyewe, na kumjua Mungu.
Chanzo, kitabu:- Njia yetu kwa mapendo na ndoa.
Friday, May 8, 2015
Thursday, May 7, 2015
CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII NI HILI HAPA......
Nimependa usemi huu MAISHA POPOTE, MUHIMU FURAHA. Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza hivi ninyi watu mtokao AFRIKA kwanini kila wakati mnaonekana watu wa furaha tu? Na pia ni wakarimu hata ukiwa na kidogo au unaishi hali ya chini lakini mnaonekana ni wacheshi tu Je? kuna siku huwa mnanuna? Nakumbuka, nilimjibu hata kama nikinuna, Je ndiyo nitafanikiwa? Akanijibu ni kweli...sasa ninyi wenzangu katika hilo swali mngejibu vipi? KARIBUNI TUJADILI.......
Wednesday, May 6, 2015
SWALI LANGU LA LEO: AMANI DUNIANI IPO WAPI?
Hivi AMANI duniani imekwenda wapi? Maana sasa watu wanauana, wanachinjana na vita ndiyo kila kukicha. Je ndiyo mwisho wa dunia au Upendo na Amani vimetutoka? Ukikumbumba hasa kwa Afrika jinsi wote tilivyokuwa wamoja, wote tulivyokuwa kitu kimoja....Hivi vyote vimekwenda wapi...Naomba tujadili pamoja maana palipo na wengi pana mengi. Kapulya.
Tuesday, May 5, 2015
ENZI HIZO WATU WOTE WALIKUWA SAWA....
Ni kweli, zamani kulikuwa na Kanisa moja, hospital moja, chama kimoja, shule moja kila kijiji, watu walikuwa wakitembeleana na walikuwa wajamaa...pia hata chakula tulikuwa tunakula sahani moja ...
Monday, May 4, 2015
NI JUMATATU YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TANO ...NA MAISHA NA MAFANIKIO INAANZA HIVI....
Hakuna kisichowezekana ... si unaona hapa . Ila mmhhh sijui huu ni ubunifu au? Nawatakieni wote jumatatu hii ya kwanza ya mwezi huu iwe njema:-) Kapulya.
Friday, May 1, 2015
NA TUUKARIBISHE MWEZI HUU WA TANO NA SIKUKUU HII YA WAFANYAKAZI KWA KUANZA NA MLO HUU AUPENDAO KAPULYA
Leo ni mwezi mpya wa tano na sio hivyo pia ni sikukuu ya WAFANYAKAZI (MEI MOSI) Kwa hiyo napenda kuwatakieni wafanyakazi wote siku njema sana kwa siku hii. Binafsi sina mapumziko mzigoni kama kawaida:-) TUPO PAMOJA NDUGU ZANGU NA NAWAPENDENI WOTE.
Subscribe to:
Posts (Atom)