Friday, March 28, 2014

MMMHHH! NINGEPENDA MLO HUU UWE MLO WANGU WA MCHANA WA LEO LAKINI....

.......duh kumbe ni ndoto tu ..kwanza unga sina...nimemaliza, pila mboga nilizoweka akiba zote nimemaliza yaani kutoka kwenye bustani yangu. Ila muda si mwingi nitaanza kulima tena kwa sasa nimewatika/atika. Ila mmmhhh mate yananitoka hapa...maana huyo samaki  eeeehh bwana weee ngoja niache...NGOJA TU NIWATAKIENI MWISHO WA JUMA MWEMA.

6 comments:

Rachel Siwa said...

Pole sana KADALA, Kwani huko kwenu hakuna African/Indian shops yanayouza Unga wa Ugali?

Rachel Siwa said...

Pole sana KADALA, Kwani huko kwenu hakuna African/Indian shops yanayouza Unga wa Ugali?

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante KACHIKI..yapo alo ila ugali wake si mtamu...nitaenda kesho kutafuta..kstika mafuka ya Afrika/Arab :-D

Anonymous said...

Wallahi nimetafuna hiyo kitu (Ugali na samakimkaango rojorojo)jana, lakini si samaki nchanga! By Salumu.

Anonymous said...

Jamani jamani jamani Yasinta, ndio nini hicho? Mbona umenitamaisha sana sana! Yaani nasikia njaa kaaaaaaaali sana, baada tu ya kuona na kusoma picha. Sasa tutafanyaje? Maana sasa umechokoza tumbo langu na wakati siwezi kukipata hicho chakula. Haya ukipata unga nijulishe lini utasonga ugali nije kujichana huko kwako. Hapa nikiwa nahamu sana ya ugali nanunua wa njano tu! Ama kweli nyumbani kuna vyakula vizuri sana, halafu ile harufu ya ugali wa nyumbani unajua tofauti na wa huku! Ladha nayo. Jamani lini twaenda Tz? endelea kutuwekea vyakula alau twala kwa macho. Ubarikiwe sana na mchana mwema.

Yasinta Ngonyani said...

Kaks Salumu...nimefurshi kama umetafuna tafuna...:-D

Ndugu yangu usiye na jina....yaani wewe acha tu. Mtu kwao. Nikipata tu unga ntakutonya ili tuutwange ugali..