Friday, November 8, 2013

SARESARE MAUA....IJUMAA NJEMA KWA WOTE

 Nimependa sana vazi hili
Kwa hiyo katika pita pita kwenye maduka nikaona hii blauzi(tunika) nikanunua ila  nimeipenda zaidi ya huyu dada hapo juu. Mimi nimenunu indiska, mpiga picha kaka Erik:-).NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA WIKI HII....IJUMAA IWE NJEMA KWA WOTE.

10 comments:

Emmanuel Mhagama said...

"tunika" ndiyo jina la huo mtindo au ni kitu gani?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhagama tunika ni aina ya blauzi ambayo ni ndefu nusu ya gauni..Kama lile vazi alilovaa Yesu na wanafunzi wake...Nadhani nimeeleweka...

Rachel Siwa said...

Umependeza sana dada wa mimi..nami nameipenda sana..Baba na Mama P wanazo,Mama Erik unayo,Baba Max anayo..mama Sandra ngoja nikatafute..sijui mama Manjula kama anayo!!!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Kachiki ni furaha ilipo kuona upo nasi tena...Loo wote hao, nami nipo katika orodha..;.)

sam mbogo said...

Namimi pia ninalo shati la kitambaa kama hicho,ila rangi yake ni kijani,watoto wangu wao kitambaa chake ni cha rangi bluu.umenogeka na vazi lako.kaka s

Anonymous said...

Umependeza sana Yasinta. Ila sasa mbona unatuangusha jamani, ulipoenda TZ ungepata nzuri zaidi ya Indiska, au sio? Kama ya huyo dada hapo juu! Siku ingine ukienda TZ inabidi uwasake mafundi ambao watakupa mitindo iliyopo kwenye chati wakati huo! Nakutakia siku njema.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Safi sana nitaomba picha yako na watoto mkiwa mmetinga hilo vazi:-) Ahsante...
Usiye na jina ! Ahsante sana ...Kuangusha mmmmhhh nilipokuwa Tz nyumbani sikuwaza kabisa hiki kitenge kama ulivyonishauri nitashona we acha tu . Nawe uwe na siku njema.

Unknown said...

xafi

ray njau said...

Binadamu mmoja na vipaji lukuki.Hongera sana!!

Yasinta Ngonyani said...

Eric,,,Karibu katika kibaraza hiki,,,,,na ahsante.

Kaka Ray! Nimeipokea Hongera yako kwa mikono miwili.