Friday, November 22, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAPO KALE UJAMAA, UMOJA, USHIRIKIANO NA UNDUGU !!!

 
Lakini leo /sasa kila mtu na chake. Hakuna tena ule umoja wa kunywa pamoja, kula pamoja na kusali pamoja. Je? kwa nini umoja wetu umepotea?----Nawatakieni wote Ijumaa njema ila usiwe ugimbi/ ulanzi/ pombe...mwingi/nyingi ,,Lol

5 comments:

Anonymous said...

Ni kwa sababu ya kutokuamiana maana unaweza kuwekwa sumu na kundi fulani lakini pia Magonjwa nayo kama mafua yanaweza kuambukizwa kupitia kushare vinywaji.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina! Na je kwa nini zamani hakukuwa na hayo uliyosema. Maana tulikuwa tukila sinia moja, kunywa kikombe kimoja na kila kitu kilikuwa safi tu...ilitokana na nini?

Rachel Siwa said...

Ubinadamu wa leo upo machoni tuu...Imani imepungua.

Yasinta Ngonyani said...

KACHIKI ! Umenena ndugu yangu!

Salehe Msanda said...

Umoja wetu umepotea kutokana na kuwa Ujamaa ulioasisiwa na mwalimu ulikuwa unakwenda kinyume na matarajio ya mwanaadamu na kwa maana hiyo kazi iliyokuwa inafanywa na mwalimu ikakosa washirika wa ukweli. Kinachotokea sasa hivi ni uthibitisho wa uasilia ya binaadamu ya kuwa na choyo ya kutoka kupata yeye tu na si vinginevyo.
Iko haja ya kufanya juhudi za ziada kuwarudisha watanzania katika hali hiyo ilivyokuwa hata kabla ya ujamaa wa mwalimu na kuangalia ni jinsi gani tunaweza kurudisha utu na thamani yetu kwa kuacha kuthamini sana katika umimi na kurejea katika ubinaadamu pamoja na kuwa ni kazi ngumu kweli kwa hali ilivyo sasa.
Kila la kheri