Watu wengi huwa wanafikiri au wanasena huyu/wewe ni adui yangu na hapo huanza vituko. Kuna wengine wanawaona hata wazazi pia ndugu zao ni maadui. Ndugu zanguni tuache chuki. Mwenzio akipata basi usimwone ni adui yako, kwa kufanya hivyo hakutakuwa na maendeleo. NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA USISAHAU KUMWOMBEA ADUI YAKO KAMA UNAYE..UKIZINGATIA PIA MWAKA NDIO UNAKATIKA HIVYO.
8 comments:
Umenena da'Yasinta, tuombe na kusamehe!Asante nawe Ijumaa njema!neno kutoka WARAKA WA KWANZA WA YOHANA 4:7-21 Baraka kwa wote!
@Swahili na Waswahili
Unadai eti " da'Yasinta amenena"?
Amenena ukweli gani?
Mimi nampinga hapo kabisa!
Kwanza wacha tumnukuu:
"Kuna wengine wanawaona hata wazazi pia ndugu zao ni maadui."
KWANINI NDUGU YAKO ASIWE ADUI?
Kwani adui ana alama gani au anazaliwa na nani?
Na huyo mtu wa kwanza kabisa kutolewa roho na adui yake duniani si alifanyiwa huo unyama na KAKA yake kabisa?
Mnataka kuniambiaje nyie Wanadada Yasinta na "Swahili" tena wapendwa na rafiki zangu?
Rachel! ni kweli kusamehe na kuomba ni muhimu katika maisha. Pamoja daima..naona kaka mkubwa hapo amepinga ...ngoja nijaribu kumjibu...
Kaka Mkubwa Phiri! ni hivi watu kuwaona ndugu na wazazi wao kama maadui ni pale wanapokuwa na chuki kwa jambo ambalo halina maana kabisa na hawataki kusamehe na uamuzi wa mwisho ni kukata mahusiano. Je hii ni busara kweli? na pia kuna wengine hawataki kuona ndugu yake anafanikiwa je huu ni uungwana? Rachel nsaidie kama kaka mkubwa hataridhika......
Ahsante kaka Manyanya,naona da'Yasinta amekujibu vyema au vipi? Ngoja nami niongezee kidogo tuu hapo. Hata kama mama,baba,dada,kaka,na ndugu yeyote au rafiki unahisi amekukwaza dawa ni kuyamaliza na kusamehe na kuanza upya,lakini ukikaa nacho na kunung'unika tuu haisaidii sana sana utajiletea magonjwa na unajinyanyasa mwenyewe tuu,na kuona una watu wenye chuki nao,basi chuki unaweza kuitengeneza wewe mwenyewe au kuimaliza wewe mwenyewe.
Natumaini kaka Manyanya atakuwa ameelewa sasa DADA YASINTA!
MUNGU NI PENDO APENDA WATU.
:-)
Na shukuru sana!
Kama tukikubaliana na nyie Wanadada, kwamba uadui si kitu chako....
.... wala si kitu cha mwingine,
...bali ni maumbile ya binadamu (au kiumbe chochote kile kingine), BASI TUNAKUBALIANA KABISA!!!
Kusema ukweli maisha bila adui (tena wengi) si kitu chema hata kidogo! Kama hujui, wanakujanjarusha waleee!
Kwa upande wenu Wanadada: MSAMAHA NA UPENDO NI LAZIMA TENA NI AMRI YA MUNGU. Yote ni kwa manufaa ya adui zetu pamoja nasi wenyewe.
Kwetu wenyewe kama siyo leo hapo baadaye ni lazima tu nasi wenye kutoa upendo na msamaha tutafaidi tu!
Chuki na wivu kwa wale ndugu zetu wenye mafanikio ni ujinga usiokuwa na kipimo.
Vilevile maringo ya wale ndugu wenye mapesa au mamlaka ni ushamba...mapesa na nyadhifa vitataisha tu au kifo kitayakomesha maringo ukiwa huku bado unaendelea kujidaidai wewe ni mtu kuliko ndugu zako maskini au wale wasiosoma kama wewe!
Hivyo, nawawashukuru kwa majibu yenu, Dada Yasinta na Rachel, tena mumenipa jawabu kabisa jinsi mawazo yenu yalivyolenga hapo awali.
Nilichowania kukifanya mimi kwa uchokozi na mchango wangu nikuhimiza kwamba neno "adui" halina kabila, halina rangi, wala halina damu.
Yaani mumeo anaweza akageuka adui yako sawasawa na jambazi yoyote yule mwingine mitaani!
Mkeo na mwanao pia ; na si lazima iwe ni wewe uliyeanzisha mifarakano, lahasha!
Mradi tu huyo mwenzio kaanzisha uhasama, hamuna budi WOTE WAWILI KUITANA "MAADUI".
NA kwa upande wako mshiriki katika huo uadui, USISITE KABISA kutumia neno "ADUI" kwani hilo neno si aibu kwa matamshi yako bali ni aibu kwa vitendo vyake mshiriki-mwenzio!
Lamsingi lakini (na hapo ndipo naamini wote watatu mimi nanyi Wanamama tutakusanyika kwa bidii) ni hili hapa.
MUNGU WETU ALITUAMRI TUWAPENDE MAADUI ZETU NA TUWATAKIE MEMA ILI TUSTAHILI KUITWA WATOTO WA MUNGU.
Yaani kila asubuhi unapoaanza siku yako ombi lako ili lifanikiwe, laanza kwa maneno: "Nampenda, wewe Mungu wangu, Adui yangu Fulani bin Fulani.
"Mungu yee, NIMEKASIRIKA SANA. Kwani Fulani bin Fulani aliniibia jana kuku wangu; bila hatia akawakanyaga pia watoto wangu vidole vyao venye funza nyingi bure,...
"Lakini hata hivyo, Eh Mungu wangu, NAMPENDA TENA NAMSAMEHE adui yangu Fulani bin Fulani, .. asante tena Amina!"
Hivyo ndivyo tunavyotakiwa "kuwashughulukia" maadui zetu.
Lakini siyo kupinga kwamba yule baba yangu mzazi au mwanangu au hata tajiri wangu ni adui yangu ikiwa kila siku matendo ya mtu yakuonyesha waziwazi yamelenga kuyahujumu maslahi yako hata uhai wako!
Kupinga unachokiona kwa macho yenye kupewa na Mungu nako kupinga kwenyewe ni ujinga wa aina yake na Mungu hapendi ujinga kwa watoto wake tena hakutuamuru tuwe wajinga!
Licha ya kunukuu amri takatifu kama hapo juu: hata kiSayansi UNAWEZA UKAPATA VIDONDA VYA TUMBO AINA YA ALSA (ulcers) ukiwa unajidai utakatifu bandia kwa kukana mtu humuoni kama adui ikiwa vitendo vyake vinakukera siku hadi siku!
Asanteni!
“Kwa maana ikiwa mnawasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi pia;lakini ikiwa hamtawasamehe watu makosa yao, Baba yenu naye hatawasamehe makosa yenu.Mathayo 6:14-15.
=====================================
Ni kweli kabisa kuwa mtenda huwa hajui kama katenda bali mtendewa ndiye anayefahamu kuwa katendewa.
=====================================
“Zaidi ya hayo, ndugu yako akitenda dhambi, nenda ufunue kosa lake kati yako na yeye peke yake. Akikusikiliza, umempata ndugu yako.Lakini asiposikiliza, chukua pamoja nawe mmoja au wawili zaidi, ili kwa kinywa cha mashahidi wawili au watatu kila jambo lipate kuthibitishwa.Asipowasikiliza hao, liambie kutaniko.Ikiwa halisikilizi hata kutaniko, mwache awe kwako kama mtu wa mataifa na kama mkusanya-kodi.Mathayo 18:15-17.
=================================== Kwa ujumla hakuna kitu uadui katika mahusiano ya kibinadamu na pale panapojitokeza changamoto ni muhimu kuzimaliza na kuendelea na maisha na mafanikio.
==================================
Kwa maana hakuna mwanadamu aliye mwadilifu duniani ambaye huendelea kufanya mema na asifanye dhambi._Mhubiri 7:20
=================================
Kama tukisema: “Sisi hatuna dhambi yoyote,” tunajipotosha wenyewe na kweli haimo ndani yetu. Tukiungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na mwadilifu hata atusamehe dhambi zetu na kutusafisha ukosefu wote wa uadilifu.Kama tukisema: “Sisi hatujatenda dhambi,” tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno lake halimo ndani yetu. _1Yohana 1:8-10
===================================
"KUSAMEHE NI KUSAHAU"
==================================
Angalizo:
Hakuna mtu anayemkosea mwenzake bali sote kwa pamoja tunakoseana kwa nyakati na viwango tofauti.
===================================
“Acheni kuhukumu ili msihukumiwe; kwa maana kwa hukumu mnayohukumu, mtahukumiwa; na kwa kipimo mnachopimia, watawapimia ninyi. Basi, kwa nini unautazama unyasi ulio katika jicho la ndugu yako, lakini hulifikirii boriti lililo katika jicho lako mwenyewe?Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Niruhusu niutoe unyasi ulio katika jicho lako’; wakati, tazama! boriti limo katika jicho lako mwenyewe?Mnafiki! Kwanza toa boriti lililo katika jicho lako mwenyewe, na ndipo utakapoona waziwazi jinsi ya kuutoa unyasi ulio katika jicho la ndugu yako.-Mathayo 7:1-5
Post a Comment