Friday, June 10, 2011

Picha ya Ijumaa ya hii-: Huyu ndiye ombaomba Maarufu MATONYA

Picha hii imenikumbusha kila Ijumaa mjini Songea kuna kuna mtindo huu watu kuja kuomba...sijui kama wewe umewahi kuwaona? HAYA IJUMAA NJEMA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA!!!!

9 comments:

watila said...

Naona Matonya style yake babu kubwa anagaragara kwenye maji dahh
hata kama huna pesa utaende kukopa ili urudi umtilie angalau shilingi 200.

Anonymous said...

Da yasinta hawo wapo wengi sana hupita kila duka hapa jijini na kupata karibu 4000 mpaka 5000. kwa kazi hiyo hasa kwa siku ya Ijumaa kama leo.mungu ibariki tanzania na watu wake. Mungu ibariki Afrika

Simon Kitururu said...

Wikiendi njema Da Yasinta!

Tukiachana na hilo!

Nilishawahi kukumbana na mjadala kuwa Tanzania Wakarimu ni Waislamu na ndio maana Ijumaa wanyonge huitumia kuomba kwa kuwa watoaji wazuri ni Waislamu kitu kifanyacho usione ombaomba wengi Jumapili kwa kuwa WAKRISTO fulu maneno ila kiutoaji ni roho ya korosho!

Kama kuna ukweli kuwa WAKARIMU ni WAISLAMU kuliko WAKRISTO usiniulize miye-sijafanya utafiti!:-(

EDNA said...

Hawa mbona wapo wengi sana tu.Ijumaa njema kwako pia.

Mwanasosholojia said...

Hii kali..teh!teh!Kweli kuna njia nyingi za kutafuta huruma ya watu kukupa chochote..hii ya Matonya ya mpaka kwenye maji imenikosha!Lakini nasikia huyu Matonya kwao Dodoma ana rasilimali...sijui kama ni kweli :)Ahsante Da'Yasinta!

Rachel Siwa said...

hahaaha kaka Kitururu sasa tumuulize nani? Na kuna mwingine alisema Baadhi/wengi wao wa Afrika Wakristu kama Kangaroo, Mikono mifupi lakini Miguu milefu!! Kwenye kucheza na kuimba mpaka liamba! Lakini kwenye Kutoa/matoleo kazi ipo hapo!!!Matonya kiboko!
Ijumaa njema nawe pia.

Penina Simon said...

Dah nimemkumbuka!!! hv sku hzi yupo wapi, kuna tetesi kuwa alihamia Morogoro baada ya maaskari jiji kuwasumbua omba omba mjini Dar, ingawa wengine walirudi lkn yeye nadhani hajarudi tena, sjui kama bado yupo hai?, na nasikia ni tajiri mkubwa kijijini kwao anaheshimika.

Mija Shija Sayi said...

Mimi nitamkubali siku atakapojilaza kwenye moto..

@Rachel, hiyo ya Kangaroo ndo naisikia leo, kweli watu kiboko..lol!!

Rachel Siwa said...

kwikwikwikwi da Mijaaaaa! maneno hayo si yangu ati niya yule kaka yako I..... WA NAMBA 339!!!!

Nami msiniulize!!!!!!