Sunday, June 29, 2008

JUNI 29,2008 THAMANI YA MSICHANA (KUTOKA KITABU UTIMILIFU WA MSICHANA)

Siku hizi kuna wataalamu wa aina na mambo mbalimbali. Hao wameendelea sana katika ufundi wa ujuzi wa mambo mengi. Tunafurahi kwani maendeleo hayo ni kwa ajili ya saida na manufaa makuu ya binadamu. Tulipewa akili ili tukautawale ulimwengu na kuufanya kuwa mahali bora pa kuishi binadamu. Kwa sababu ya utaalamu huo mwingi, mambo mengi hupimwa kwa darubibini na mbinu mbalimbali, mbinu tofauti na zile tulizozizoea katika maisha yetu ya kla siku; hasa kadiri walivyoishi wazee wetu. Mabadiliko yatokanayo na mbinu na darubini hizo mara nyingi hutufanya kujisahau na kutojua tutokako wala tuendako.

Leo hii, wataalamu hao wamefikia kiwango cha kusema kuwa mwili wa binadamu unatengenezwa tu na mchanganyiko wa madini mbalimbali. Kama vile chumvi chumvi pamoja na chembe chembe za hewa-Carboni, Oxigeni na kadhalika. Hayo yote, wanadai wataalamu hao. yanaweza kununuliwa na kuuzwa dukani. Thamani ya mwili mzima wa binadamu kwa kufuatana na vipi mo hivyo inakisiwa kuwa karibu shilingi ishirini tu. Hakika, mbinu zimetofautiana. Wengi wanashtushwa na msemo huo wa wataalamu kwani wanafahamu, japo hawana utaalamu wa kisayansi, kuwa mwili wa binadamu na zaidi ya madini na michanganyiko ya mambo hayo ya kiulimwengu. Sasa basi, wewe dadangu, hebu jipime na ufikirie juu ya thamani yako ya kweli. Tafiti kwa unyofu wako wote juu ya umaana, ubora na thamani ya kweli ya usichana wako. Ugunduzi huo mdogo utakaoufanya, nakuhakikishia, utakuwa huo mdogo utakaoufanya, nakuhakikishia, utakuwa wa mafaa makubwa kwako kuliko ugunduzi wa wataalamu wengi ambao wameingia kwenye mkondo wa kushusha hadhi ya utu wako. Pale unapojisikia ukiwa, unapojiona kuachwa, hata na marafikizako na unapokuwa na wasiwasi moyoni; jizatiti na kwa unyofu ujichunguze, utapata faraja ya kweli na kufanya ugunduzi mkubwa kwa maisha yako. Hata unapojiona si kitu mbele ya wenzuo bado una nafasi na thamani ya pekee. Mimi najaribu kukunyoshaea msitari tu wa kufikia ugunduzi huo. Hata hivyo, ni wewe tu unaweza kuukamilisha, hakuna mwingine.

Mungu Baba yako anafurahi anapokuona ukitafiti juu ya umaana na thamani yako ya kweli. Ufanyapo hayo kwa nia ya kujitambua kweli, na kujikuza kimwili na kiroho, yeye mwenyewe atakuwa tayari kukusaidia ili ufikie lengo lako. Yeyote ajisaidiaye husaidiwa. Hasa kwa vile kwa kufanya hivyo unajofunua kwake na kuangalia ni nini nafasi yako ya pekee kama msichana, nafasi ambayo hakuna mwingine awezaye kukupatia bali yeye mwenyewe.

Unapojisikia mwenyewe fungua macho yako ya ndani, jikusanye kimawazo, legeza maungo yako ili usitawanye nguvu zako ovyo na uwe na nia ya kweli ya kufahamu ukweli wa maisha juu yako mwenyewe. kwanini hasa U MSICHANA!

Wewe U msichana mwenye uhai, mzuri na mpendeka. maisha hatuna budi kuyazatiti, si kwa sababu yatuletea vituko au hata furaha, lakini hasa kwa sababu mara tu tuzaliwapo tunakuwa tumewekwa kwenye msafara ambako tutapambana tutake tusitake na milima na mabondo- yaani magumu ya maisha. Kisha kuzaliwa kwako, utakuwepo mpaka milele, hutaisha tena. hata unapokufa kama walivyodai wengine, huo hautakuwa mwisho wa safari au kuwepo kwako. Baada ya kifo cho utakuwepo kwake Yeye akupendaye kiutimilifu, yaani Baba yako wa mbinguni ndiyi aliyekuumba.

Hata hivyo, dadangu mpendwa usiogope. hutakuwa peke yako katika msafara huo. Wazazi, jamaa, marafiki na wasichana wenzio na hata yule atakaye kuwa mteule wa moyo wako atakuwepo katika msafara huo pamoja nawe. Hutasikia ukiwa ikiwa ulitumia busara wakati wa safari yako. Juu ya hao wote, yeye aliyekupa uhai yupo akikutazama na kukuchekelea kama mama mzazi anavyofurahia apapokiona kitoto chake kinajaribu kutembea kwa mara ya kwanza. Kitoto kinapokuwa hatarini mara mama yu tayari hata kama kufanya hivyo kungelikuwa hatari kwake. yeye Baba huyo wa mbinguni ndiye, kiu cha maisha yako, japo hutakuwa umekitambua dhahiri.

Hiki kitabu kimenielemisha na nakipenda sana.

Na; Yasinta Ngonyani

No comments: