Nilifurahi sana hii siku kukaribishwa kwa mtindo huu...
Nsio mimi tu niliyefurahia..
.
Saturday, July 27, 2019
Sunday, July 21, 2019
Sunday, July 14, 2019
NIMEPITA SOKONI SONGEA NIKAKUTANA NA VYAKULA NIVIPENDAVYO SAMAKI MBELELE NA LIKUNGU NILI
Hapa ni samaki aina ya mbelele watamu sana sana ila wana miba ndogo ndogo ulapo yabudi uwe mwangalifu sana...
Wednesday, July 10, 2019
Saturday, July 6, 2019
Saturday, June 29, 2019
NAWAKARIBISHA HAPA KWETU RUHUWI/SONGEA TULE VYA ASILI
Matunda ni kutoka nje na kuchuma, kama muonavyo ni papai, passion, tunda damu, machungwa na ndizi. Raha tupu-:)
Chai kwa vitumbua...nimekumbuka enzi hizo ili kupata pesa ya kalamu basi tulikuwa tukipika vitumbua.
Chai kwa vitumbua...nimekumbuka enzi hizo ili kupata pesa ya kalamu basi tulikuwa tukipika vitumbua.
Monday, June 24, 2019
TUANZE HII WIKI NA PICHA HII KUWA IWE PICHA YA YA WIKI ...
Pamoja na kuwa amebeba mtoto na mzigo kichwani lakini sura yake ni ya furaha ...nimeipenda hii picha...
Monday, June 17, 2019
HODI HODI NYUMBANI ....RUVUMA YITU YABWINA
Kwetu ruvuma ni kuzuri nje kuona na mahindi mje kula vyakula vya asili . KARIBUNI SANA MAANA MIE NISHA KARIBIA:-)
Wednesday, June 12, 2019
NIMEAMKA NA WAZO HILI LEO
Nawaza kwa sauti kwa nini mifuko ya plastiki inakatazwa lakini sio viti vya plastiki. Maana ukiangalia hiki kiti kina ubora zaidi kuliko cha plastiki...nimewaza tu kwa sauti
Sunday, June 9, 2019
TUFANYE NYUMBA ZETU KUWA "KIJIWE" CHA MARAFIKI WA WATOTO WETU
nimekumbuka enzi zilee
Siku zote fungua milango kwa watoto kufurahi nyumbani kwako na watoto wenzao na utawasaidia kuepuka mengi kwa dunia ya sasa yenye changamoto za kila namna. Ni vyema mtoto akawa huru kuchagua rafiki, ila kama mzazi / mlezi unaweza kumsaidia ushauri tu juu ya marafiki wema wenye maadili mema kama wewe ulivyojitahidi kumfundisha. Sikiliza mazungumzo yao, michezo na tabia za marafiki aliowachagua mwanao kisha umshauri kuhusu marafiki hao endapo utaona sio marafiki wazuri na mpe pongezi unapoona marafiki zake ni binadamu wema. Ni vyema pia ukayafanya makazi yako kuwa sehemu rafiki kwa marafiki wa watoto wako kujumuika na kufurahi pamoja. Hii itakusaidia kujua tabia za marafiki hao na pia itasaidia kuwaweka salama watoto wako kwa sababu watacheza na kufurahi nyumbani kwako na sio sehemu zingine usizofahamu
Wednesday, May 29, 2019
VYAKULA/MILO AIPENDAYO KAPULYA
Chakula cha asubuhi mayai, soseji na vinginevyo na bila kusahau matunda kama papai, nanasi na zabibu. Bila kusahau chai(chingambwe) yaani chai isiyo na sukari
Hapa ni viazi kwa samaki wa kuchoma/banika yaani hapa ndo walinikumbusha kwetu LUNDO/NYASA.
PAMOJA DAIMA.
Monday, May 20, 2019
HUU NI UJUMBE WA JUMATATU YA LEO.......
Wakati mwingine unaweza kupata msaada kwa mtu ambaye hukuwahi ku/mtegemea au ulimdharau, hivyo ni kheri kuishi vizuri na kila mtu kwa kuwa hujui kesho yako.....
Friday, May 17, 2019
KWETU RUVUMA NI KUZURI VYAKULA VINGI SANA HASA VYA ASILI....KARIBUNI
Maembe sasa yanaelekea kwisha ila da ni uhondo juu ya uhondo
Hapa ni masuku, matunda pori/asili sisi wangoni huyaita pia MAPOTOPOTO
Na mwisho hapo ni matunda pori/asili nayapenda sana sijui kama yana jina la kiswahili ila sisi wangoni twayaita MADONGA.PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA NA VYAKULA VYA ASILI AU KITU KINGINE....Kapulya wenu.
Wednesday, May 8, 2019
BADO NIPO KWETU RUVUMA NAFAIDI HIVI VYAKULA VYA ASILI
Hapa ni mchanganyika wavyakula nivyopendavyo yaani mahindi ya kuchemsha pamoja na maboga/mapondo na halafu njugu....
......na hapa ni kikande yaani hiki ndo cha asili kabisa, hakina radha saa lakini ni kitamu
Na hapa ni kumbikumbi napenda sana kumbikumbi. Na nafurahi kwamba miaka kadhaa ijayo karibu dunia nzima kutakuwa na chakula kama hiki, yaani kumbikumbi, nzige, mende nk. TUKUTANA TENA WIKI IJAYO....KAPULYA WENU.
......na hapa ni kikande yaani hiki ndo cha asili kabisa, hakina radha saa lakini ni kitamu
Na hapa ni kumbikumbi napenda sana kumbikumbi. Na nafurahi kwamba miaka kadhaa ijayo karibu dunia nzima kutakuwa na chakula kama hiki, yaani kumbikumbi, nzige, mende nk. TUKUTANA TENA WIKI IJAYO....KAPULYA WENU.
Monday, April 29, 2019
Friday, April 19, 2019
Thursday, April 11, 2019
HAPA NI VAZI LA WIKI HII CHUICHUI NA NYEUSI
Mdada yupo katika pozi fulani hivi kwa kulifurahia vazi laki
...hapa kaambiwa asilale/sinzia
Nachukua nafasi hii kuwatakieni juma njema, amani na furaha na pale upatapo wasaa wakumbuke wapendwa wetu/wako. TUPO PAMOJA:-)
Friday, April 5, 2019
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA NJEMA .....
....pia mwisho wa juma kwa ujumla kwa mlo huu. UJUMBE:- Maisha sio kama mshumaa , maisha ni kama mwenge.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA NAWATAKIENI KWARESMA NJEMA. Kapulya.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA NAWATAKIENI KWARESMA NJEMA. Kapulya.
Monday, April 1, 2019
Tuesday, March 26, 2019
LEO NIMETUMIWA ZAWADI HII NA RAFIKI YANGU
Baada ya kushukuru nimemlaumu sana kwa kunitamanisha.....ahsanten kwa zawadi rafiki yangu umenikumbusha kwetu Lundo/nyasa
Saturday, March 23, 2019
ASIFIWE TUTAMKUMBUKA DAIMA!
AHSANTE KAKA JACOB MAHOLIJA KWA KUMBUKUMBU HII NZURI NIMEONA NIIWEKA HAPA KIBARAZANI KWA VILE LEO NI MIAKA 9 SASA IMETIMIA HAUPO NASI KIMWILI ILA KIROHO.
Leo ni arobaini ya Mpendwa wetu Asifiwe Ngonyani alama ya upole na upendo iliyofutika ghafla tarehe 23/3/2011 kama imefanyika ilivyopangwa.
Pamoja na kuwa mila zetu wengi zinatueleza kuwa arobaini ni kuhitimisha msiba lakini ukweli itachukua muda huzuni kufutika katika mioyo yetu, hasa kwa tuliopata bahati ya kumuona binti huyo. Tunakubali kwasababu kazi ya mungu haina makosa. Bali Asifiwe Tutamkumbuka.
ASIFIWE TUTAMKUMBUKA!
Marehemu Asifiwe akiwa na baba
Kwa upande wangu nikiwa na siku kadhaa mbali na Jiji la Dar es Salaam katika Vijiji ambako network ya mawasiliano ni mtihani kidogo hali yangu ya kifikra ilikuwa tata kidogo, nahisi ilikuwa ishara ya taarifa ya kusikitisha.. nilipokuwa katika vijiji vyenye mtandao, niko bize, baadae nikaona Misscall ya Yasinta. Sikuwa na hela ya kutosha kwenye simu siku iliyofuata Simu iliita nikiwanayo mkononi nikapokea.
Tofauti kabisa na nilivyozoea napompigia au anaponipigia, habari niliyoipata ilininyong’onyesha!, Kwa sauti ya unyonge Yasinta alisema “Jacob nilikuwa nakutafuta ulikuwa hupatikani, nilitaka nikupe taarifa Asifiwe Hatunaye Tena” kwanza nilijipa moyo huenda sikuwa kwenye simu ni mawazo tu .. lakini kwanini niwaze hivyo?....ikabidi nimuulize “Unasemaji Yasinta?” .. “Asifiewa Amefariki” alirudia kunithibitishia … hatukuongea sana .. nilimwambia tutaongea .. bado nikiwa nahisi labda ni mawazo tu .. nikamtumia msg kumuuliza tena, alinijibu “ni kweli Jacob, Asifiwe Ametuacha” tuliendelea kuchati kwa muda kidogo lakini dakiki zilivyozidi nilizidi kuishiwa nguvu.. nikakata mawasiliano..maana taarifa zilikuwa zinazidi kuniumiza!
Nilikuwa namfahamu Asifiwe baada ya kumtembelea Nyumbani Ruhuwiko miezi michache baada ya kurudi Kutoka kwenye matibabu ya moyo Dar es Salaam mwaka jana.
Ktika picha ya pamoja na Marehemu Asifiwe
Kwa waliowahi kukutana na binti huyu kama kaka Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti aliyewahi kumtembelea pale Hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo, Shaabani Kaluse ambaye pia Jumamosi ya terehe 18/03/2011 alipata bahati ya kumuaga Asifiwe, na wengine waliowahi kumuonawataungana nami kuwa binti huyu alikuwa mpole, mtulivu mwenye sura ya heshima na upendo.
“Nilijikuta nikimwambia kuwa sasa anatakiwa kurudi Shule, akiwa na tabasamu pana usoni mwake alinijibu kuwa yuko tayari kurudi shule na ndipo baba yake akaniomba nimsaidie kumtafutia shule nzuri atakayosoma binti huyu” alisema Shaabani Kaluse, ambaye naungana naye mia kwa mia.
Asifiwe alikuwa na kiu sana ya kusoma, kama ilivyokuwa kwa Kaluse nilipomtembelea, katika mazungumzo alionyesha sana kiu ya kusoma, nilimuahidi kumsaidia atakapukuwa ametulia vizuri na nikampa kitabu kinachoitwa “Mpenzi wa Kweli” nilichokiandika kwa ajili ya vijana hasa wanafunzi kikizungumzia maadili na umuhimu wa kupenda Elimu. Alikipenda sana!.
Nasikitika nilichelewa kupata taarifa, nasikitika sikushiriki wakati wa msiba ila wanablog 53 kwa niaba ya wote walipata kushiriki vizuri msiba huu mzito online, wengine walitumia simu .. wengine wakaandika kwenye blog zao .. Yasinta hakuwa peke yake wakati huu mgumu.
“Dada Naomba uamini kuwa msiba huu sio wakwako peke yako ni msiba wetu sote, yaani familia ya Mzee Ngonyani na ya Mzee Mkundi au pengine na Wanablog wote wa ndani na nje ya nchi.
Ni msiba wetu kwa sababu wengi wetu tulikufahamu wewe kupitia maandishi yako katika Blog ya Maisha na Mafanikio ambapo pia tukaifahamu familia yako na familia ya Mzee Ngonyani” alisema Koero mkundi katika blog yake.
Baada ya kuongea mambo mbali mbali namna ya kumsadia asifiwe, nilipata picha na Mzee Ngonyani.
Binafsi nilitarajia kuhudhuria arobaini ya Asifiwe, lakini nasikitika nimekuwa na wakati mgumu kimajukumu. Hata hivyo leo usiku mdogo wangu anasafiri kuelekea Sweden atanifikishia Salamu zangu kwa Yasinta. Lakini pia nitakapokuwa Songea hivi karibuni nitamtembelea Mzee Ngonyani kumpa pole.
Friday, March 22, 2019
IJUMAA YA LEO TWENDENI NAMI MPAKA KWETU KUSINI TUSIKILIZE NGOMA YETU YA LIZOMBE/KITOTO - NI SISI WANGONI KUTOKA rUVUMA
KARIBUNI SANA.....
PANAPO MAJALIWA TUTASIKILIZA WIMBO MWINGINE WIKI IJAYO ..Kapulya wenu!
PANAPO MAJALIWA TUTASIKILIZA WIMBO MWINGINE WIKI IJAYO ..Kapulya wenu!
Friday, March 15, 2019
ZILIPENDWA- MOROGORO JAZZ BAND ATT RTD DAR ES SALAAM
NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA .
UJUMBE WANGU WA LEO:- AMANI, UPENDO NA FURAHA NDIYO VIVWE NGUZO YETU. Kapulya wenu.
Wednesday, March 13, 2019
PALE UNAPOSUBIRI KUSIFIWA!
Unapofanya jambo lolote, fanya tu kama nafsi yako inakubali na inafurahia jambo hilo.
Usifanye jambo kwa kutegemea kusifiwa. Kumbuka usiposifiwa itakuuma sana, lakini ukisifiwa bila kutegemea sifa hiyo, utajisikia furaha sana.
Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa Binadamu ni kiumbe anayependa kusifiwa, lakini ikitokea ukawa na kiu kubwa ya kupenda kusifiwa , basi inabidi ujiulize, ni wapi pana kasoro kwenye fikra zako.
Haiyumkini katika malezi yako hukuwahi kusifiwa kamwe na maisha yako yalitawaliwa na kulaumiwa kwingi na kukosolewa, hivyo ukajikuta ukihitaji kukamilishwa.
Haya burudika na shairi hili la Malenga wa Mvita.
UWATAPO HAKI YAKO
Namba nawe mlimwengu, pulikiza matamko
Nikweleze neno langu, uzinduwe bongo lako
Nayo nda M'ngu si yangu, na ayani haya yako
Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
Simama uitete, usivikhofu vituko
Aliyo nayo mwendee, akupe kilicho chako
Akipinga mlemee, mwandame kulla endako
Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
Amkani mulolala,na wenye sikio koko
Isiwe mato kulola,natutizame twendako
Tuwate na kuduwala,usingizi si mashiko
Uwatapo haki yako,utaingiya motoni
Teteya kwa kula hali, usiche misukosuko
Siche wingi wala mali,sabilisha roho yako
Unyonge usikubali, ukaonewa kwa chako
Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
Siche kifaru na ndovu, wangazidi nguvu zako
Wapempe kwa uwekevu, unusuru haki yako
Siandame wapumbavu,kilicho chako ni chako
Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
Cha mtu hakifitiki,kikafungiwa kiliko
Huzuka kikawa hiki,kazana utwae chako
Uwatapo yako haki,fahamu ni dhara kwako
Leo na kwa Mola wako,utaingiya motoni
Fumbuwa unyang'arize, uone duniya yako
Bure sijiangamize,kuangalia wendako
Utatupa upoteze,wende ambapo si pako
Uwatapo haki yako,utaingiya motoni
Kadhalika nako pia,huko ambako sikwako
Huwezi kujitetea,wala huwi na mashiko
Basi iwaze duniya,kwani ya kale hayako
Uwatapo haki yako ,utaingiya motoni
Kadi tamati shairi,sitii la ongezeko
Mwanati iwa tayari, utete haki yako
Unyonge usiukiri,Jifunge ufe kwa chako
Uwatapo haki yako, utaingiya motoni
Shairi hili limetungwa na Ahmad Nassir wa Malenga wa Mvita
Friday, March 8, 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)





























