Tuesday, April 30, 2013

SHUKRANI KWA WOTE MLIOSHIRIKI NASI KATIKA KIPAIMARA CHA BINTI YETU..AMBAYO NI SEHEMU/HATUA YA MAISHA KATIKA MAISHA/KUISHI!!!!

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mliohudhuria siku hii ya kipaimara cha binti yetu iwapo kiukaribu au kwa umbali..Mwenyezi Mungu awazidishie Upendo. Kwa vile Mwanakipaimara anajua kiswahili amesoma maoni ameniagiza kusema AHSANTE SANA kwa kuwa naye kwa siku hii maarufu katika hatua za maisha...AHSANTENI..NA MUWE NA JUMANNE NJEMA..KAPULYA NA FAMILIA.

Sunday, April 28, 2013

JUMAPILI YA LEO NI MAARUFU BINTI YETU CAMILLA ANAPATA KIPAIMARA..HONGERA..

picha ya pamoja baada ya kupata kipaimara Da ´Camilla  hapo katikatika na nywele nyeusi
 
nipo na rafiki
watu walivyofurika

baadhi ya wageni waliokujha kumpongeza Camilla
baadhi ya msosi

 
baada ya misa , sasa hapa nu nyumbani

keki ya karoti
 
kufungua zawadi
Jumapili hii imekuwa ndefu na nyenya baraka nyingi sana katika nyumba yetu ...TUNAMSHUKURU MUNGU KWA SIKU HII...nimeona niwe pamoja nanyi katika siku hii njema, AHSANTE MUNGU....NA HONGERA SANA BINTI CAMILLA

Saturday, April 27, 2013

JUMAMOSI YA LEO TUANGALIE VITENDAWILI VYETU...KITENDAWILI.....

Kwanza nina swali moja hivi kwa nini tunasema KITENDAWILI....na wengine wanajibu...TEGA..???? HAYA KITENDWILI...
1. Huyu mwanamume, huyu mwanamke, hwakutani...
2, Mtoto wangu ninapomtuma mmoja, wanarudi wengi.
3. unga wa kuanika usiku, mchana hakuna.
4. Shamba langu kubwa, ulezi nivunao kiganja kimoja
5. mtu mwenyewe mdogo, watoto wengi.

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NASUBIRI MAJIBU:-)

Thursday, April 25, 2013

TANZANIA INA MAKABILA MENGI NA KILA KABILA LINA MTINDO WAKE WA KUENEZA UTAMADUNI WAKE .HAPA NI NGOMA YA Traditional dance, Kisesa...


Haya jamani ilikuwa zamani kidogo na hizi ngoma zetu za asili..karibuni tucheze...mimi nafikiri ni WASUKUMA HAO ..JE WEWE MWENZANGU UNASEMAJE? MUWE NA WAKATI MMOJA

Wednesday, April 24, 2013

KATIKA MAISHA KUNA KUPENDWA NA KUCHUKIWA NA WATU ....!!! UPENDO!!!

Kupenda/upendo ni kitu cha ajabu sana mara nyingi nimekuwa nimejiuliza kwa nini sisi binadamu tuna upendo tofauti kwa kila mtu. Nikisema hivi nina maana kuna wakati mtu inaweza kutokea unampenda mtu kiasi kwamba huwezi kujizuia. Na cha ajabu mara nyingine uanaweza kumpenda mtu ambaye hujawahi kumwona ana kwa ana(uso kwa uso) na upendo ukawa wa nguvu kali sana.
Halafu sasa inaweza kuwa kinyume kabisa. Yaani watu tunaweza kuwa na chuki. Unaonana na mtu siku moja tu na utasikia simpendi kabisa jamaa huyu. Au hata kuangalia tu picha yake unapatwa na chuki. Nashangaa sana kwa uwezo kama huu ambao MUNGU amatupa na pia SHETANI anaingilia na kuharibu.Swali:- Hivi hii inatokana na nini?
Leo nimeona niimbe mwenyewe ila samahani hamtaisikia sauti yangu:
Upendo, upendo, upendo ni amri ya bwana, Yesu alisema pendaneni, pendaneni kama nilivyowapenda. Nanyi pia, nanyi pia mpendane palipo na upendo Mungu yupo nasi tupendane tupendanex2.
NAWATAKIENI WOTE UPENDO NA AMANI KATIKA KILA MFANYACHO...KAPULYA

 

Tuesday, April 23, 2013

KUNA NJIA NYINGI YA KUITANGAZA BENDERA YETU YA TANZANIA...

Nimependa magauni haya nafikiri safati ijayo nami nitashona maana duh nimepeata hamu kweli--kama tusemavyo ni rangi nzuri na kila moja ina maana yake..tukianzia na..
1. Nyeusi- Huonyesha watu wa Jamuhuri ya Tanzania.
2. Kijani - Huonyesha mimea na ardhi ya Tanzania
3. Njano - Huonyesha utajiri wa mali ya asili.
4. Bluu - Huonyesha bahari inayoziunganisha sehemu za Jamuhuri ya Muungano
Haya ni maelezo  ya Bendera yetu ya Jamuhuri ya Tanzania....Si mnakumbuka tulijifunza darasa la tatu-nne vile au?......Nawatakieni wote JUMANNE NJEMA!!!!

Monday, April 22, 2013

SIMBA WEUPE WA PORI LA LIPARAMBA WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA....!!!

Juzi nilikuwa naangalia habari ya wanyama pori ambayo ilikuwa kuhusu simba waupe huko Afrika ya kusini,,,Mara nikakumbuka ya kwamba Simba waupe wanapatikana pia katika pori la wanyama la Liparamba wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Ina semekana Wanyama katika pori hii kila mwaka wanahamia kutoka nchini Msumbiji kuingia Tanzania. JE WEWE MWENZANGU UMEWAHI KUONA SIMBA MWEUPE???

Sunday, April 21, 2013

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE WATAOPITA HAPA...MAISHA NA MAFANIKIO

IMANI YA BWANA IWE NANYI...NA UPENDO PIA BARAKA ZITAWALE NYUMBANI MWENU.

Saturday, April 20, 2013

JUMAMOSI ...UJUMBE WANGU NI HUU....

Ukiwa DUNIANI USIHUZUNIKE na usiwe MNYONGE hata kama una UMASKINI kiasi gani. Mungu yuko pamoja nawe na unatakiwa kuzingatia haya:-
1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4. 5. kumbuka Mungu ndie mpangaji wa kila linalokutokea.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. Kukikosa ulichokikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU/JUMAMOSI  NJEMA

Thursday, April 18, 2013

KWA MARA NYINGINE TUANGALIE JAMBO HILI :-MTOTO/KIJANA AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI -SONGEA!!!

Katika pitapita nimekutana na hii mimi na Tanzania ...nikakumbuka hii nikaona niweka hapa  maisha na mafanikio... haya hebu wasikilize maelezo yao pia wanajamii wengine...

Sijui hapa itakuwa laani au ni ukosefu wa akili...inasikitisha sana kwa kweli....Jioni njema kwa wote mtakaopita hapa..Bibi kaongea na kingoni bwana :-)

unaikumbuka hii???- KUAMINI KUWA WAMEKAMILIKA NI KUJIDANGANYA BURE!


unaikumbuka hii? ebu soma tena ni vizuri kukumbuka  zilipendwa....karibu

Wiki iliyopita na wiki hii nimekumbuka sana nyumbani, nadhani ni kwa sababu wiki iliyopita tarehe 17 ilikuwa ni tarehe ambao mama yangu alifariki na wiki hii 23/5 imetimia miezi miwili tangu Mdogo wangu alifariki. Kwa kweli nam-miss sana mama yangu pia mdogo wangu.

Nakumbuka ilikuwa kila nikienda likizo, nilikuwa natumia muda mwingi kuwa jikoni na mama yangu nikizungumza naye simulizi za kale za enzi ya utoto wangu.

Ni simulizi ambazo kwa kweli kila nizikumbukapo huwa natamani yale maisha yajirudie kwani kuna mengi ya kufurahisha na ya kuhuzunisha ambayo kwangu mimi nimejifunza mengi kwako.

Lakini lipo jambo moja ambalo nimelikumbuka, ambalo kwa kweli huwa linanifikirisha sana. Jambo lenyewe ni kuhusiana na baadhi ya marafiki zangu kule nyumbani.

Kusema kweli ule ukaribu niliokuwa nao na baadhi ya marafiki zangu umepungua kiasi cha kukatisha tamaa.

Sababu kubwa ni kutokana na kile walichodai kwa nimewatupa kutokana na kutowasaidia kupata wachumba wa Kizungu. Yupo rafiki yangu mmoja mbaye yeye aliwahi kunitamkia wazi kuwa mimi ni mbinafsi kwa kuwa ni mara nyingi ameniomba nimtafutie mchumba wa Kizungu kwa kuwa ninaishi huku ughaibuni lakini nimeshindwa kumtafutia.

Nakumbuka nilimweleza ukweli kuwa siwezi kumsaidia juu ya jambo hilo kwa sababu liko nje ya uwezo wangu, lakini kutokana na labda tuite ufinyu wa kufikiri, nilimpoteza rafiki huyu kwa sababu ya kushindwa kumtafutia mchumba wa kizungu……..yaani kaaaazi kweli kweli.

Hata hivyo nilijiuliza swali moja, kuwa hivi hakuna wanaume huko nyumbani mpaka mtu aamue kutafuta mchumba wa Kizungu? Je ni mapenzi au ni Uzungu unaotafutwa hapo?

Lakini kwa upande mwingine sikumshangaa sana kwa sababu kwa huko nyumbani ipo silka ya baadhi ya watu ambao wanaamini kwamba kuoa au kuolewa na Mzungu ni jambo la kujivunia sana. Huwa nimezoea kauli za baadhi ya watu kule nymbani kila niendapo likizo wakisema, ‘siyo mwenzako yule, kaolewa na Mzungu’ .

Yaani mpaka leo hii bado kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa kuoa au kuolewa na mzungu ni jambo la kifahari na la kujivunia. Kinachotafutwa sio mapenzi tena ni huo uzungu..

Kuna baadhi ya watu wamefikia hatua ya kuamini kuwa sisi waafrika ni duni na wenzetu weupe ni bora na waliokamilika.

Lakini nadhani makosa hayo hayakuanza leo, yameanzia mbali sana. Kwani kizazi na kizazi tumekuwa tukiaminishwa kuwa wazungu ni bora zaidi yetu sisi.

Kwa mfano, mtu kufanya mambo yake kwa umakini na anayefuata muda huyo ataitwa ni mzungu, au mtu asiyependa majungu, uzinzi, uasherati na umbeya naye ataitwa kuwa ni mzungu. Nakumbuka wakati nikisoma kule nyumbani, ilikuwa kama kuna mwalimu ambaye ni mwadilifu kwa wanafunzi na anayewajali, utawasikia wanafunzi wakisema, ‘yule mwalimu ni mzungu’

Yaani kipimo cha kufanya mambo kwa uadilifu na kuwajali wengine kimekuwa kikihusishwa na uzungu, mpaka imefikia mahali kila mtu anatamani kuolewa au kuoa mzungu wakiamini kuwa hao wamekamilika.

Hata huko makazini napo watu wanaochapa kazi kwa uadilifu wanafananishwa na wazungu. Wakati mwingine huwa nacheka kwa sababu naamini hao wanaoamini kwamba mtu kuwa mzungu anakuwa amekamilika ni wazi kwamba hawawafahamu watu hao.

Kwamba kuwa mzungu ni kutokuwa na tabia mbaya, kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani, nikujidanganya bure.

Nasema kuamini hivyo ni kujidanganya, kwa sababu kwa wale wanaoishi huku ughaibuni au wale wanaofanya kazi na hawa wenzetu huko nyumbani, watakuwa ni mashahidi wangu.

Kama mlikuwa hamjui ni kwamba hawa wenzetu nakubali kuwa wapo waadilifu na wenye tabia nzuri, lakini pia wapo wenye tabia za ajabu kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, kutojiamini, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani.

Ule udhaifu tulio nao pia wenzetu hawa wanao tena wenzetu hawa wamepitiliza. Ila kutokana na kudanganywa na TV na hizo kauli za wazee wetu tumejikuta tukiamini kitu ambacho hakipo.

Mie wakati mwingine huwa nashangaa pale ninapokutana na baaadhi ya Watanzania wenzangu ambao wanaishi au wamewahi kuishi huku ughaibuni wanapozungumza kwa kubana pua kama hawa wenzetu. Wanashindwa kujua kwamba ile ni lafudhi ambayo inatokana na lugha yao. Ni kama pale unapokutana na Mmakonde, Mngoni au Msukuma au Mpare anapoongea Kiswahili kwa lafudhi ya lugha yao.

Mbona wenzetu kwa mfano Wanaijeria au Wakenya wanaongea kwa lafudhi ya lugha zao. Ni rahisi sana kumtambua Mkenya au Mnaijeria kutokana na lafudhi yake pale anapoongea Kiingereza, tofauti na sisi ambapo Tunajitahidi kubana pua mpaka tunajisahau hata pale tunapoongea Kiswahili.
Na ndio maana kuna baadhi ya wanawake huko nyumbani na hata huku ughaibuni wamefikia hatua sasa wanaukataa uafrika na kuanza kujichubua kwa mikorogo ili kuutafuta weupe.

Kuna wakati nilipokuwa huko nyumbani nilishangaa kuwaona baadhi ya wasichana ambao nawajua kabisa rangi zao kuwa ni weusi kama mimi lakini wamekuwa weupe mpaka wanatisha! Tabu yote hiyo ni ya nini?

Tumefikia hatua sasa kila jambo linalofanywa na hawa wezetu tunaiga, na ndio sababu siku hizi tabia kama za ushoga, usagaji na tabia nyingine chafu tunazozishuhudia huku zimetamalaki huko nyumbani.

Sisi kama Watanzania tunazo tabia nzuri ambazo hawa wenzetu wanazitamani sana tofauti na tunavyodhani. Kwa mfano, sisi ni kawaida mtu kuamka na kupita nyumba mbili tatu na kuwajulia majirani zake hali, au kuingia nyumba yoyote na kama akikuta chakula akala bila wasiwasi.

Kwa upande wa Misiba au harusi watu wamekuwa wakichangiana na kusaidiana kwa hali na mali, yaani tumekuwa na ushirikiano wa hali ya juu tofauti na wenzetu hawa.

Kuwa mzungu haimaanishai kuwa mwadilifu wala kuwa na tabia nzuri, bali tabia nzuri inatokana na tabia ya mtu na malezi kwa ujumla wake, hakuna mahusiano yaliyopo kati ya uadilifu, tabia nzuri na uzungu. Nasisitiza kuwa hakuna kitu kama hicho, ni kujidanganya bure.

Inashangaza kuona kwamba, badala ya kujivunia tabia hizi nzuri tulizo nazo ambazo hata hivyo wenzetu wanazitamani, tunatamani za kwao ambazo nyingi ni mbaya na zenye kuumiza.
Tubadilike………………

Wednesday, April 17, 2013

BIBI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA MAPEMA ALFAJIRI LEO..UTAKUKUMBUKWA DAIMA!!

Hapa ni Bi Kiduka katika uhai wake akipiga ngoma..
Upumzike kwa amani utakumbukwa daima.

Tuesday, April 16, 2013

KANGA YA VIKOMBE VYA CHAI...NIMEIPENDA HII KANGA!!!!!

Maandishi yanasema ISIKUHADAE RANGI TAMU YA CHAI NI SUKARI...Hivi ni kweli?

Monday, April 15, 2013

EBU LEO TUANGALIA BAADHI YA MAKUNDI MBALIMBALI YA WATU HAPA DUNIANI...

Katika hii dunia kuna watu wa aina mbalimbali...
kundi la kwanza: Kuna watu wanajua lakini hawajui kwamba wanajua. Hawa wanaitwa wasahaulifu na sisi tunatakiwa tuwakumbushe.

kundi la pili:- Kundi hili ni kwamba wengine ni maskini wa Mungu hawajui lakini Mungu amewabariki wanajua kwamba hawajui . Hao ni wajinga na sisi inabidi tuwaelimishe.

kundi la tatu:- Hawa wengine wao wanajua na wanajua kwamba wanajua. hawa waelevu nasi tunahitaji kujifunza toka kwao kwa vile wao ni waelevu.

Na kundi la nne: Wengine hawajui na wao hawajui kwamba hawajui wabishi. Hawa ni wapumbavu ..hawa inabidi tuachane nao kabisa. Mhhhh..najiuliza sijui ni kundi gani nipo???
JUMATATU NJEMA KWA WOTE...

Sunday, April 14, 2013

JUMAPILI NJEMA KWA NA AMANI ITAWALE NDANI YA NYUMBA ZENU....

Wote mnapendwa sana ...na tuzidi kupendana..JUMAPILI NJEMA SANA....

Friday, April 12, 2013

LEO TULIKUWA TUKIMSINDIKIZA DADA YETU MPENDWA MARIANA KATIKA SAFARI YAKE/MAKAO YAKE YA MILELE....

Kama nilivyowataarifu hapa basi leo imekuwa siku ya mwisho kumsindikiza dada yetu, Mama yetu na rafiki yet mpendwa Mariana katika makao yake ya milele..................................................................


HAPA NDIPO ATAKAPOLALA DADA MARIANA
 PAMOJA NA MWANAE MANUELA
Siku ya leo imekuwa siku ndefu na ya masikitiko kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na imekuwa siku ya kujifunza mengi kwangu, kutoka kwa da´mkubwa Mariana kwa kweli. Ama kweli wote watendao mema huwa wanatutangulia kwanza. Katika maisha yangu hapa nimewahi kwenda  kwenya misiba/mazishi mingi/mengi sana lakini huu leo hapana. Watu walifurika kuliko kawaida kiasi kwamba nikajiona nipo kwangu Afrika. Na kanisa lilikuwa halitoshi kabisa. Kweli ukitenda mema utarudishiwa hapa hapa duniani. Watu walifumuka pande zote. Au niseme hivi kwa kifupi dada huyu hakuna neno la kutosheleza maelezo yake kwa kweli,,,,alijali sana wengine na mpaka kujisahau mwenyewe. NITAKUKUMBUKA DAIMA. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA

Wednesday, April 10, 2013

PICHA YA WIKI:- WANAWAKE WANAWEZA HATA KABLA HAWAJAWEZESHWA.....

Hapa nimejiuliza mara kumi kumi hivi anawezaje  huyu mama....maana kuendesha baiskeli unahitaji balansi na kuubeba huyo mzigo pia halafu mtoto mgongoni na mtoto nyuma ya baiskeli naye kabeba mtoto ...mmmmhhh hapa kazi  kwelikweli....Lakini kweli hii ni haki kweli/Uungwana kweli??? KILA LA KHERI !!!

KUNA ANAYEJUA HABARI ZA MWALIMU MATONDO MASANGU NZULILIMA????

Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza mwalimu Matondo yupo wapi na halafu juzi tu nimeulöizwa na mkereketwa mwingiau niseme mwal. Mhango  kama najua habari na ndugu yetu huyu. Kwa kweli sijui kabisa na sasa naona kichwa kimetawala mno..Je? kuna anayejua habari/kitu chochote kuhusu ndugu yetu huyo? Maana ukiangalia hapa  inaoshesha ni muda sana aliweka kitu...

Tuesday, April 9, 2013

PALE WATU WANAPOJIULIZA KWA NINI WANGONI WANA VIBONGO/MAJINA YA UKOO KAMA WANYAMA????

Dhumuni la leo ni kutaka kumjibibu dada msaidizi katika mada hii swali lake lilikuwa kama lifuatavya hapa chini
Mija Shija Sayi said...Yasinta umependezaje?
Hebu naomba utusaidie wadau wako kwamba, ni kwanini wangoni majina yao mengi wamechukua kwa wanyama?
Ngonyani, Mapunda.. n.k, Je kuna historia yoyote? Kaka S mtaalamu wa mambo ya Tamaduni,swali hili unaweza tusaidia pia..
Asanteni..
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
nami nitajaribu kujibu kama ifuatavyo....
Wangoni wanajulikana sana kwa kuwa na mvibongo/majina ya wanyama wa pori, na hata wanyama wa nyumbani ama majina ya miti au hata ya nyasi. hii ilianzia pale ukoo wa mwanzo ulitoka wapi, wangoni wana majina ambayo yanaelezea kile wanachokifanya, jinsi walivyokuwa hapo kale nk- Walipoanza kutembea na kupiga vita na watu wengine ndo hapo wakaongezea  na majina ya wanyama, ndege na ya miti. kwa mfano:- Cawe, Gama, Kapungu, Komba, Kunguru, Mbawala, Nyati, Nguruwe, Ngonyani, Soko, Nyoka na Tembo.....na mengine mengi sitaweza kuyataja yote maana ni mengi mno..

Saturday, April 6, 2013

JUMAMOSI YA LEO NINGEPENDA MLO WANGU UNGEKUWA HIVI...NAOTA NDOTO...

 
 

Nimeamka na kuanza kufikiri huu ungekuwa mlo wangu wa siku ya leo chai kwa maandazi au vitumbua...
 ....chai ya rangi bila sukari
 ...au labda chai kwa Vitumbua na chapati...
Na hapa ungekuwa mlo wangu wa mchana huu sambusa....Sambusa tamu sana ila inabidi uwe na muda haswaaa..
na kumalizia siku kwa ugali kwa samaki na kachumbali kidogo---
kumalizia na glasi ya maji...mmmhhh hivi ndivyo ningependa siku yangu ya leo ningekula lakini sasa sitaweza ....nakula kwa macho. baadhi ya picha nimezipata hapa. JUMAMOSI NJEMA.

Friday, April 5, 2013

NIMEKUMBUKA KWELI NYUMBANI LEO NIKAANZA KUSIKILIZA NGOMA ZETU ZA ASILI..HII NI NGOMA BETA YA WANGONI

NAWATAKIENI WOTE JIONI HII YA IJUMAA YA TAREHE 5/4 IWE NJEMA NA YENYE UPENDO,,,,

IJUMAA NJEMA...NA UJUMBE HUU!!!

Napenda kuwatakieni wote IJUMAA njema sana..kama una nafasi hata dakika tano chukua hizo na msalimu rafiki yako umpendaye na hata tu kumtumia ujumbe. WOTE MNAPENDWA SANA...

Thursday, April 4, 2013

TUSISAHAU METHALI ZETU....!!!!!

1. Watu tunawadhania ni marafiki, mara nyingine ni maadui.. Mpelelezi si rafiki.
2. Mtu akitaka kupata cheo, awe na heshima kwa wakubwa.
3. Kama ukipata mali kwa kazi yako, weka akiba kwa siku za uzee.
4. Ufuate mashauri na maneno ya watu wenye akili.
5. Mtu ana maneno mazuri na matamu, lakini nia yake ni mbaya.
6. Ukiwa mgeni katika nchi, uelekee kadiri watu walivyo.
7. Wakiwa wakubwa wawili, watapata ugomvi, hawawezi kukaa pamoja.
8. Mtu akitangaza habari ya uongo, ni vigumu kusahihisha maneno yake.
9. mtu anaweza kukuchekelea kwa mdomo, lakini katika moyo ana mawazo mengine.
10. Ujitahidi mwenyewe na Mungu atakusaidia.
TUTAENDELEA KUKUMBUSHANA KILA WIKI ILI TUSISAHAU..NA KAMA KUNA MMOJA ANA NYINGINE ANAWEZA KUONGEZEE TU...SIKU NJEMA SANA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA...KAPULYA

Tuesday, April 2, 2013

WANAMITINDO NA WAREMBO WA WIKI ..JE? UNAWAJUA HAWA WADADA??

Hawa ni kati warembo,wanamrindo waliokuweka katika  COVENTRY WOMEN  Kwa picha na mambo mengine zaidi bonyeza KACHIKI. Ahsanteni wote...