Friday, September 15, 2017
Thursday, September 14, 2017
PICHA MOJA MWONEKANO TOFAUTI...SWALI JE? MWONEKANO UPI WAMFAA DADA HUYU?
Kwanza ilikuwa hivi ....
Baadaye dada yangu Mariam akaona kuna vitu vinakosekana kama uonavyo alivyoorodhesha katika picha....
Miaka imepita na jana ndipo nilipotumiwa hii picha kwa mfano huu. Hakika sikuitambua kabisa. Na bado sijitambui maana hiyo si tabia yangu...Je wewe msomaji unauonaje huu mfano wa hii picha ya Kapulya ya mwisho?
NAWATAKIENI JIONI NJEMA KWA WALE WATAKAOPITA HAPA KIBARAZANI....KAPULYA MDADISI WENU
Tuesday, September 12, 2017
VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU ...AU KUNA MWINGINE ANAPENDA KAMA MIMI??
NI WALI NA KUNDE...KWETU UNGONINI TWAITA (NGUNDI MANGI)
Baada ya chakula nilipenda sana haya matunda ...kwa mara nyingine tena kikwetu twaita MADONGA....
Nikikosa hivyo basi nakula uyoga....Je wewe kuna chakula hujala siku nyingi na sasa watamani kukila? Nawatakieni wote jioni njema!!!
Monday, September 11, 2017
NI SIKU NYINGINE PIA WIKI NYINGINE NA NI JUMATATU....
Nawatakieni siju hii ya Jumatatu na wiki hii iwe yenye furaha na amani...pia nawatakieni yote mtakayofanya yawe yenye mafanikio mazuri. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA !
Wednesday, September 6, 2017
SOKONI SONGEA... KUMBUKUMBU
Bado tuangalie Songea kwetu kama muonavyo hapa ni nje ya soko kuu la Songea.... TUONANE TENA WAKATI UJAO.
Tuesday, September 5, 2017
Monday, September 4, 2017
TUANZE WIKI HII NA NENO FURAHA: HIVI KWANINI KUN SIKU MTU HUKOSA FURAHA?
Ndiyo...Furaha inatokana na ridhiko la ndani la mtu bila kuhusisha vitu vya nje. Mtu akishajua namna sahihi ya kuipata furaha basi hataipoteza kamwe. Yoyote anaeipoteza furaha huyo anakuwa anaitafuta nje yake kwenye mazingira ya nje.....
Lazima atakuja kuikosa siku moja kwasababu mazingura ya nje sio rafiki sana na binadamu kwasababu hubadilika badilika....
Mfano kuna wakati wa jua, masika na kiangazi za kawaida...
Kama umepanga kwenda kulipwa mapato yako fulani na umewekeza furaha yako kwenye hela halafu mvua ikanyesha lazima tu furaha yako itapotea....
Kuridhika kwa ndani kuna maana ya kujikubali jinsi ulivyo bila kutegemea hali ya nje iko namna gani...
Utakapo jikubali namna ulivyo kamwe hutajutia wala kukosa furaha hata siku moja
Saturday, September 2, 2017
UJUMBE WA LEO:- KILA AITAZAMAYE KESHO YAMPASA KWANZA AIMALIZE LEO:- ACHA NIKUDOKEZE JUU YA MAISHA YA LEO...
2.Ishi na FURAHA isiyo na mipaka.
3.Ishi kwa AMANI na kila Mtu.
4.Usiweke MAMBO yako wazi kwa kila mtu kwani binadam hatufanani.
5.Jiheshimu kwani HESHIMA yako inatokana na jinsi ulivyo.
6.Kuwa MVUMILIVU katika kila jambo ili kufikia mafanikio.
7.Weka MSAMAHA mbele kwa kila anaekukosea na unaemkosea.
8.MISUKOSUKO ni sehemu ya maisha na ndio hatua ya kuvuka ili kufanikiwa katika MAISHA hivyo usikate tamaa.
9.Omba na kumshkuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo kwani yeye ndiye anayekupa UHAI.
TUMALIZIE NA WIMBO HUU ....
Thursday, August 31, 2017
NIMEONA TUBAKI KIDOGO KATIKA MKOA HUU WA RUVUMA ....HAYA KUWA SAMBAMBA NAMI....
Kama hukujua jina RUVUMA limetokana na nini sasa wajua ni kwamba:- Ruvuma ni eneo la Tanzania. Jina lake ni kutokana na Mto Ruvuma ambao mipaka yake ipo kusini mwa Msumbiji.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA...NI KAPULYA WENU.
Tuesday, August 29, 2017
HISTORIA FUPI YA WANGONI WAKIWA KATIKA ARDHI YA WASHONA WAKIJA KATIKA ARDHI YA TANZANIA
Mara baada ya kutokea vita vilivyofahamika kwa jina la mfekane kwenye miaka ya 1800, , vilivyokuwa vikihususisha makabila yalikuwa yakipatikana kusiniu mwa Afrika. Wangoni waliamua kuondoka na kusambaa Afrika mashariki na kati wakiwa na Kiongozi wao Zwangendaba. Wakati wanasambaaa Afrika mashariki na kati, Wangoni walipitia sehemu nyingi sana, zipo sehemu walizopokelewa kwa heri na zipo sehemu walizopokelewa kwa shari. Lakini ukweli ni kwamba Wangoni waliondoka Afrika kusini kutokana na vita vilivyotokea. Na sababu kubwa ya vita hivyo ni sera ya upanuzi ya mfalme wa kabila la Wazulu aliyefahamika kwa jina ka Tshaka Zullu. Kutokana na vita hivyo ambavyo pia vilihusisha hata watu wengine ambao hawakuwa Waafrika kama vile Wadachi na Waingereza. Hivyo Wangoni waliamua kuondoka kusini mwa Afrika na kuja Afrika ya mashariki na kati. Sasa wakati wanakuja Afrika ya kati na mashariki Wangoni walipita sehemu nyingi sana. Moja ya sehemu ni ardhi ya Washona . Kwa ufupi ni kwamba Washona ni moja ya jamii zinazopatiakana katika ardhi ya Zimbabwe. Na zaidi jamii ya Washona wanapatikana mashariki mwa jamii za Wakalanga ( hii ilikuwa moja ya sehmu ambayo Wangoni walipita mara baada ya kuvuka mto Limpopo). Washona waliamia maeneo hayo wakiongozwa na mtemi wao aliyefahamika kwa jina la Ska-vunza kwenye karne ya 18. Na ifahamike kuwa Washona ni moja ya kabila ambalo linapatiakna katika kundi hili la Wangoni.
Monday, August 28, 2017
Friday, August 25, 2017
JAMANI MWENZENU BADO NIPO NYASA KWETU NAKULA SAMAKI CHAKULA NIKIPENDACHO KUPITA VYOTE:-)
Thursday, August 24, 2017
Monday, August 21, 2017
HUU NDIYO MLO WETY KAMILI HUKU NYASA
Ugali wa muhogo kwa maharage, dagaa na samaki pia huwa matembele au kisamvu ila leo tumesamehe:-) KARIBUNI TUJUMUIKE. NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA JUMA.
Sunday, August 20, 2017
NAPENDA KUWATAKIENI JUMAPILI NJEMA KWA NENO HILI....
......Yeye ajibuye kabla hajasikia, ni mpumbavu na aibu kwake
MITHALI 18:13
JUMAPILI NJEMA IWE YENYE AMANI, FURAHA NA BARAKA. TUSIKILIZANE KWA MAKINI NA PIA TUPENDANE!
MITHALI 18:13
JUMAPILI NJEMA IWE YENYE AMANI, FURAHA NA BARAKA. TUSIKILIZANE KWA MAKINI NA PIA TUPENDANE!
Friday, August 18, 2017
HAINA KEMEKALI HII...NI BORA ZAIDI KWA AFYA!
POMBE AINA YA KOMONI
NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO WA JUMA MWEMA ILA KUNYWA KIDOGO USIPITILIZE. PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMA LIJALO HAPA HAPA. KAPULYA WENU...
Wednesday, August 16, 2017
Tuesday, August 15, 2017
KAPULYA WENU AMETAMANI MLO HUU LEO
Hakika asiyetamani mlo huu mmmhhh yaani nimeamka leo hii nikiwa na hamu sanaya mlo kama huu .....ngoja nifanye mpango. Au nile kwa macho tu:-)
Saturday, August 12, 2017
Wednesday, August 9, 2017
FANYA KAZI PIA CHUKUA MUDA WA KUPUMZIKA PALE INAPOTAKIWA.....
Hivi kwa nini sisi binadamu daima tunafanya kazi kwa ajili ya keshe, lakini wakati kesho ikija, badala ya kufurahi, lakini bado tutafikiria kesho tena? Hebu tufurahie leo basi !.
Tuesday, August 8, 2017
UJUMBE TOKA KWA KAPULYA KUJA KWA YEYOTE ATAKAYEPITA HAPA
Katika maisha :- Kitu kizuri ni pale unapojisikia /unapojua ya kwamba hapa duniani mtu /watu ana/wana furaha kwa ajili yako wewe
Monday, August 7, 2017
KILIMO CHA BUSTANI KWA MTINDO MPYA ....KAZI YA MIKONO YANGU
HAPA NI NYANYA TENA JANA TUMEANZA KULA
PILIPILI
ZABIBU PIA ZIPO
Niwatakieni mwanza mwema wa juma hili panapo majaliwa tutaonana tena.....Kapulya wenu:-)
Thursday, August 3, 2017
LEO TUANGALIE :- SIFA ZA MTAMA NA VIRUTUBISHO VYAKE!
Sifa za mtama:- Mtama una virutubisho muhimu vinavyotakiwa katika mwili wa binadamu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtama una kiasi cha wanga, nishati, nyuzi nyuzi, na mafuta karibu au sawa na mahindi au nafaka nyingine.
Mtama una madini aina ya chuma na chokaa kwa wingi kuliko mahindi au nafaka nyingine. Una protini kwa wingi kuliko mahindi, mchele au ngano. Mafuta yake hayanarehamu, Una vitamin B complex,vitamin C na vitamin E kwa wingi. Mtama una madini ya zinc, phosphorus, potassium, na manganese kwa wingi kuliko nafaka nyingine.
Mtama una vimelea viitwavyo phenolica mbavyo ni mhimu sana kwa mwili kujikinga na saratani, Mtama hauna gluten hivyo ni salama kutumiwa na watu wenye matatizo au ugonjwa wa Celiac.
Muhimu: Sukari yake huyeyuka taratibu sana mwilini hivyo mtama ni chakula kinachofaa kuliwa na watu wenye magonjwa kama kisukari.
HII NIMETUMIWA NA RAFIKI NIKAONA NI SOMO ZURI KWA WENGI ....AHSANTENI.
Wednesday, August 2, 2017
HIVI NDIVYO VYAKULA AVIPENDAVYO KAPULYA WENU
Ugali wa ulezi na nyama ya kuku, na sio ugali tu ugali na mlima wake juu ukiisha huu ni lazima usingizi mnono utapatikana iwe mchana au usiku:-)
Samaki waliokaangwa kwa ustadi haswaaaa
Au tu chips MIHOGO...nimekula sana mlo huu wakati nipo chuo kwanza naupenda pia ilikuwa bei rahisi na unashibisha . Ukipata na kachumbali yako mmmhhh utajiuma kidole au pia ulimi:-) Haya niwatakieni mlo mwema siku ya leo chochote utakachokula kiwe kitamu.....PANAPO MAJALIWA
Tuesday, August 1, 2017
KAPULYA KATALII KIDOGO
Kasafisha macho kidogo sio mbaya hapa hili jengo ni makumbusho ya vita nchini Norway
Nashanga shangaa tu:-)
Hapa ilikuwa ni mlima kidogo kwa hiyo ikawa kama ule wimbo wa mchakamchaka panda, panda , panda usichoke....WOTE MWAPENDWA...
Subscribe to:
Posts (Atom)




























