Tuesday, July 4, 2017
Monday, July 3, 2017
BUSTANI...NILIMTEMBELEA DADA YANGU MMOJA KWENYE BUSTANI YAKO HII NZURI
MCHICHA NA MAHARAGWE
Jana nilimtembelea dada yangu kwenye bustani yake. Ana bustani nzuri sana niliipenda sana na kumwonea wivu:-) ila kwa upendo wake alinichumia mchicha mwingi tu nilimshukuru sana. Bustani yangu mwaka huu inasuasua....ila sijakata tamaa na hivyo nimeiona ya huyu dada nimepata nguvu zaidi......karibuni mtaona bustani yangu
Friday, June 30, 2017
TUMALIZE WIKI HII NA PICHA HII......IJUMAA NJEMA
Kama hamogopi njoeni ukutane na mawe...:-) duh kaaaazi kweli kweli maana hayo mawe yenyewe yanaonekana makubwa haswaaa likikupata hilo kichwani ...mmmmhhh.....NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA....KAPULYA WENU!
Thursday, June 29, 2017
NYUMBA ZA KALE ZA WANGONI
Leo nimekumbuka kwetu ungonini na nyumba zetu za asili....nyumba aina hii huitaji kiyoyozi safi sana....
Wednesday, June 28, 2017
KUMBUKUMBU : - UNAKUMBUKA HADITHI HII MANDAWA NA MANENGE....
Hapo zamani palikuwa na mtu na mkewe, mtu huyo aliitwa Manenge na mkewe aliitwa Mandawa. Siku hizo chakula kizuri kilikuwa maziwa na nyama.
Lakini vyakula hivi vilipatikana kwa shida shida. Maziwa yaliweza kupatikana tu kama mtu alikuwa na ngòmbe. Na nyama iliweza kupatikana tu kama mtu alipewa zawadi na jamaa yake au alinunua. JE ? UNAIKUMBUKA HADITHI HII?
Lakini vyakula hivi vilipatikana kwa shida shida. Maziwa yaliweza kupatikana tu kama mtu alikuwa na ngòmbe. Na nyama iliweza kupatikana tu kama mtu alipewa zawadi na jamaa yake au alinunua. JE ? UNAIKUMBUKA HADITHI HII?
Tuesday, June 27, 2017
KITENDAWILI........!
Kitendawilii!!!!!!
Ni cheupe kama Barafu,
Na ni cheusi kama giza,
Kuliwa ni haramu na kunywa ni halali kina herufi 5
na kinaanza na herufi ( M ) kinatumiwa na wanaume mara 3 kwa siku,
Na kinatumiwa na wanawake mara 1 kaitka umri wao,
Je?,Ni kitu gan hicho???
TAFADHALI TAFADHALI NI KITU GANI HICHO?
Ni cheupe kama Barafu,
Na ni cheusi kama giza,
Kuliwa ni haramu na kunywa ni halali kina herufi 5
na kinaanza na herufi ( M ) kinatumiwa na wanaume mara 3 kwa siku,
Na kinatumiwa na wanawake mara 1 kaitka umri wao,
Je?,Ni kitu gan hicho???
TAFADHALI TAFADHALI NI KITU GANI HICHO?
Monday, June 26, 2017
KUMBUKUMBU:- KARIBU TUNYWE PAMOJA MTANI
Leo nimekumbuka ubenani au niseme MATETEREKA KWETU kwa babu MBOZA...ULAZI. ILA huyu dada duh! kazi kwelikweli...nawatakieni JUMATATU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA!
Thursday, June 22, 2017
MLO WA MCHANA WA LEO:- UGALI,TEMBELE NA DAGAA
Kuna watu tembele wanaona kama mboga duni sana, wanakosa uhondo kwa kweli. Ni hivi:- kwanza chambua vizuri, kisha osha tembele lako, mimi huwa naanika kidogo lakini kuna wengine wanapika moja kwa moja baada ya kuosha yaani bila kuanika. Weka sufuria/chungu motoni, weka mafuta ya kutosha, maana tembele linahitaji mafuta la sivyo utalichukia na ndio sababu wengi hulalamika matembele sio mazuri, kumbe mapishi duni. Tia kitunguu geuza geuza kisha tia nyanya zako na chumvi kidogo. Nyanya zikiiva weka tembele lako. Ligeuze hapo mpaka linywee weka maji kidogo sana kisha funika, sio sasa ndo utoke....utaunguza. Watakiwa uwe hapo hapo unalichungulia kama limeiva. Ukiona bado ongeza maji kidogooo usiweke maji menge, ukiona linanywea zaidi hapo mambo tayari/limeiva.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu tayari kwa kula sasa.
Mwisho mwidho kamulia kipande cha ndimu au limau geuza dakika mbili -tatu tayari kwa kula sasa.
UGALI,TEMBELE NIMEONGEZA NA DAGAA
Weka mezani kama hutakipenda hiki chakula, basi nimeshindwa. NATUMAINI UTAJILAMBA VIDOLE:-) MCHANA MWEMA.
Wednesday, June 21, 2017
HISTORIA- TUSIWASAHAU MASHUJAA WETU WA VITA YA MAJIMAJI
Maaskari wa vita ya majimaji
Tuesday, June 20, 2017
UJUMBE KUTOKA KWANGU KAPULYA KUJA KWENU
Sisi binadamu ni wanasheria (mahakimu) wazuri kwa makosa yetu, lakini ni watu wazuri sana kuhusu makosa ya wengine
NAWATAKIENI HII SIKU YA LEO IWE YENYE AMANI NA FURAHA PIA. PANAPO MAJALIWA TUKUTANA PAPA HAPA. KAPULYA
NAWATAKIENI HII SIKU YA LEO IWE YENYE AMANI NA FURAHA PIA. PANAPO MAJALIWA TUKUTANA PAPA HAPA. KAPULYA
Friday, June 16, 2017
NAPENDA KUWATAKIEN MWISHO WA JUMA HILI UWE MWEMA WENYE AMANI NA FURAHA KWA WOTE...
Binafsi bado nina uchovu kidogo wa shughuli za jana...ila nipo sawa..NAWAPENDA WOTE
NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA ...KAPULYA
Thursday, June 15, 2017
PONGEZI: BINTI CAMILLA LEO ANAMALIZA ELIMU YAKE YA SEKONDARI
Hapa yupo katika maandalizi....kisherea hapa huvaa gauni nyeupe na kofia nyeupe...
Hapa ilikuwa juzi katika sherehe ya kuhitimu Sekondari ( GRADUATION) Hapa huanza na sherehe na baadaye ndiyo kupokea cheti cha kuhitimu.
Na hapa alikuwa na msindikizaji wake kaka Philip.
picha zaidi zitakuja ambazo zitakuwa na maelezo zaidi na labdda maakuli na shamrashamra...haya baadaye kidogo
Monday, June 12, 2017
JUMATATU YA LEO TUANGALIE BAADHI YA METHALI/MISEMO ILIYOZOELEKA SANA HASA KWENYE KANGA
1. Penzi la mama haliishi
2. Mchimba kisima huingia mwenyewe
3. Zawadi pokea usahau yalotokea
4. Haraka haraka haina baraka
5. Haba na haba hujaza kibaba
6. Si kusudi ni tabia
7. Usilaumu dunia bali imani na nia.
2. Mchimba kisima huingia mwenyewe
3. Zawadi pokea usahau yalotokea
4. Haraka haraka haina baraka
5. Haba na haba hujaza kibaba
6. Si kusudi ni tabia
7. Usilaumu dunia bali imani na nia.
Friday, June 9, 2017
IJUMAA: MITINDO YA NYWELE, UREMBO KWA UJUMLA NA VAZI LA SKETI ALIPENDALO KAPULYA WENU
Nimependa mtindo huu wa nywele (MABUTU) na jinsi alivyojipamba kwa ujumla yaani ni kiasili haswaaa...SAFI SANA!
Na hii sketi duh! rangi za kitenge ni murwaaa na urefu wa sketi yaaani nikama ugalina samaki wa kuchuma kwenye mkaa!
NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA HILI JUMA
Na hii sketi duh! rangi za kitenge ni murwaaa na urefu wa sketi yaaani nikama ugalina samaki wa kuchuma kwenye mkaa!
NAWATAKIENI MWANZO MWEMA WA MWISHO WA HILI JUMA
Thursday, June 8, 2017
KARIBUNI CHAI NA MBATATA/VIAZI VITAMU...
Nimeona nisiwe mchoyo karibuni tujumuike kwa mlo huu maalumu na mtamu pia mzito. Binafsi napenda zaidi mlo kama huu kuliko CHAI MIKATE (MABOFULA) ambayo ukila tu dakika kadhaa ni bonge la njaa tena. Halafu angalia viazi vilivyopikwa na maganda yake..Mmmmhhh ngoja niache maelezo na wengine waseme:-) PANAPO MAJALIWA!
Wednesday, June 7, 2017
SERIKALI KUIFUNGA HOSPITALI YA KIBENA NJOMBE KWA HUDUMA MBOVU
Hii iliwekwa 14 feb. 2016
Ya kwamba ...Serikali huenda ikaifunga hospitali ya Kibena iliyopo mkoani NJombe kutokana na kutoa huduma zilizo chini ya kiwango
Saturday, June 3, 2017
LEO NI SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KIJANA WETU ERIK..HONGERA
Tuesday, May 30, 2017
MSIBA MKUBWA UMETUPATA UKOO WA AKINA NGONYANI PERAMIHO /LUNDUSI BABA/BABU NA KIONGOZI WETU KATUTANGULIA MBELE ZA MUNGU LEO MAPEMA ASUBUHI
Hii picha ni wakati wa uhai wake hapa ilikuwa 2005 nyumbani kwetu LITUMBANDYOSI yeye ni huyo mwenye miwani yupo pamoja na wdogo zake.
Na hapa yupo na moja wa wajukuu zake ilikuwa mwaka 2016 November. Babu yetu Lotary amekuw akiugua tangu kipindi cha pasaka
Na hapa ni picha yake ya mwisho iliyopigwa 28/12/2016.Wewe Ulikuwa Kiongozi wa ukoo wa akina Ngonyani, babu yetu, baba yetu na pia mshauri mzuri sana pale mtu atakapo ushauri. TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ATUTIE NGUVU KWA KIPINDI HIKI CHA MAOMBELEZO. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIMIWE. UPUMZIKE KWA AMANI BABU YANGU/YETU. AMINA
Na hapa yupo na moja wa wajukuu zake ilikuwa mwaka 2016 November. Babu yetu Lotary amekuw akiugua tangu kipindi cha pasaka
Na hapa ni picha yake ya mwisho iliyopigwa 28/12/2016.Wewe Ulikuwa Kiongozi wa ukoo wa akina Ngonyani, babu yetu, baba yetu na pia mshauri mzuri sana pale mtu atakapo ushauri. TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ATUTIE NGUVU KWA KIPINDI HIKI CHA MAOMBELEZO. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIDIMIWE. UPUMZIKE KWA AMANI BABU YANGU/YETU. AMINA
Sunday, May 28, 2017
TUMALIZE JUMAPILI YA MWEZI HUU WA TANO KIHIVI,,,ASUBUHI NA NAFASI MPYA YA NDOTO ZAKO KUWA DHAHIRI
Asubuhi ni nafasi mpya ya kuzifanya ndoto zako kuwa dhahiri:- Fursa mpya, mipango mipya ...huja katika fikra.
Usifikiri sana kuhusu jana, juzi wala siku yoyote ambayo pengine ulikosa au ulishindwa jambo fulani...anza siku ya leo kwa kukiri kuwa itakuwa siku njema kuliko nyingine zote.
Siku, ni sehemu ndogo katika "MAISHA" ambayo Mungu hutuzawadia. Itumie vizuri, ifanye iwe ya MAANA KWAKO, USIPOTEZE TUMAINI....USIKATE TAMAA MUNGU YUPO PAMOJA NAWE SONGA MBELE DAIMA . Kumbuka "unaweza mambo yote katika yeye (MUNGU) akutiae nguvu" FIL 4:13 NAKUTAKIA ASUBUHI NJEMA, SIKU NA JUMAPILI YENYE BARAKA, AMANI NA FURAHA. AMINA!
Usifikiri sana kuhusu jana, juzi wala siku yoyote ambayo pengine ulikosa au ulishindwa jambo fulani...anza siku ya leo kwa kukiri kuwa itakuwa siku njema kuliko nyingine zote.
Siku, ni sehemu ndogo katika "MAISHA" ambayo Mungu hutuzawadia. Itumie vizuri, ifanye iwe ya MAANA KWAKO, USIPOTEZE TUMAINI....USIKATE TAMAA MUNGU YUPO PAMOJA NAWE SONGA MBELE DAIMA . Kumbuka "unaweza mambo yote katika yeye (MUNGU) akutiae nguvu" FIL 4:13 NAKUTAKIA ASUBUHI NJEMA, SIKU NA JUMAPILI YENYE BARAKA, AMANI NA FURAHA. AMINA!
Saturday, May 27, 2017
Wednesday, May 24, 2017
UJUMBE WA WIKI HII: MAISHA HAYAMTAMBULISHI MTU KWA WATU....
Maisha hayamtambulishi mtu kwa watu atakaokukutana nao. Kuna wakati, maisha yaweza kukukutanisha na watu ambao uliwahitaji/unawahitaji kukutana nao ili wakupe msaada, ili wakuumize, ili wakuongoze, ili wakuache mpweke, ili wakupende na ili wakupe/wakutie nguvu katika hatua ya kukuimarisha ili uwe mtu imara katika maisha yako.....TUPO PAMOJA!
Tuesday, May 23, 2017
Sunday, May 21, 2017
JUMAPILI NJEMA...
Vazi la Jumapili ya leo....nimekumbuka mtindo wa kufunga mkanda zilipendwa mmeona eeeh!
Kama kawaida mbwembwe tu hapa nilikuwa sijui nikiomba?
Kama kawaida mbwembwe tu hapa nilikuwa sijui nikiomba?
Friday, May 19, 2017
NIMETUMIWA ZAWADI YA DAGAA NYASA
Ukiwa na hamu ya vyakula vya nyumbani na marafiki wanakutumia ni raha sana. Leo nimebahatika kutumiwa dagaa nyasa na rafiki yangu mpendwa ....angalao nile kwa macho:-(. IJUMAA NJEMA KWA WOTE.
Thursday, May 18, 2017
MAMA HIVI ULIMPA MUNGU SHILINGI NGAPI?
Baada ya miaka saba ya ndoa bila kupata mtoto, Magreth alimuambia mumewe Benjamin kuwa atafute mwanamke mwingine wa kuzaa naye. Walishahangaika sana kuzunguka mahospitalini na kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio.
Nyumba yao ilikua na amani na Ben alishakubaliana na ile hali, lakini ndugu zake walikua wanasumbua sana, walimtukana mkewe matusi mengi, wakimuambia kula, kulala anawajazia choo, walimnyanyasa sana na Mage hakuwa na raha.
Aliona njia pekee ni kumruhusu mumewe kuoa mwanamke mwingine ili angalau apate mtoto na ndugu zake waache kumsakama. Ben hakuwa tayari kuoa mwanamke mwingine, alikataa katakata lakini mkewe alisisitiza huku akitishia kuondoka kama asingeoa mke mwingine.
Siku moja Ben aliamua kuwaita ndugu zake wote, na wote waliitikaa wito aliwaambia ana kitu kikubwa cha kuwaambia kwani na yeye alishachoka suala la mtoto na alitaka kufanya mamauzi makubwa. Wakiwa na shauku ya kujua ni nini walifika.
Ben aliwapokea vizuri na baada ya chakula Ben alimuambia mkewe akachukue begi liko kitandani. Ndugu zake walitabasmu wakijua mtoto wao kaamka na sasa anamfukuza mkewe ili atafute mke mwingine na kupata mtoto.
Mkewe alienda kitandani, alichukua begi kubwa na kulileta pale. Ndugu walikaa kimya, Ben alilichukua na kulifungua, lilikua limejaa pesa tu, noti za shilingi elfu kumi zimepangwa vizuri.
Kila mtu alishangaa na hata mkewe alishangaa. Ben alianza kuongea. “Ndugu zangu nimewaita hapa kwa kuwa nina tatizo kubwa nyie wote mna watoto Mungu kawabariki hata wewe mdogo wangu hapa ni mjamzito na Mungu akijaalia utajifungua salama.
Lakini mimi na mke wangu Mungu hajatubariki kuwa na watoto” Alitulia kidogo huku akifuta machozi, yaliyotaka kudondoka. “Sasa nimewaita hapa mnisaidie kitu kimoja tu. Nianze na wewe Mama kwani kila siku umekua ukiniambia kuhusu mjukuu.
Aliongea huku akimgeukia Mma yake. “Chochote mwanangu…” Mama yake aliitikia kwa shauku. “Ninachotaka Mama ni kwamba uniambie ulimpa Mungu shilingi ngapi mpaka akakupa watoto…
Maana mimi nimejaribu imeshindikana, hizi ni hela zote nilizonazo benki na kesho nitaongea na Dalali ili tuuze nyumba mimi na mke wangu tukapangishe lakini tupate mtoto.”
Alitulia kidogo, watu wote walimshangaa, lakini aliendelea. “Ndugu zangu nisaidieni, nyie mna watoto mlimpa Mungu shilingi ngapi au nini mlitoa, mlimuona wapi mkampelekea, mimi nipo tayari kutoa kila kitu katika maisha yangu ili tu na mimi niitwe Baba na mke wangu aitwe Mama.
Niambieni tu ni bei gani Mungu anapokea?” Wote walinyamaza kimya, hakuna aliyeongea tena, walimuangalia huku wakiangaliana kwa aibu. Hakuna aliyejaribu kunyanyua mdomo.
“Sasa ndugu zangu kama hamjui kiasi ambacho Mungu anapokea ili kutoa watoto basi sitaki kusikia tena hili suala. Mimi na mke wangu tuna furaha, sitaki mtuingilie, siku mkitaja mtoto mje mniambie anauzwa wapi na bei gani nitanunua!
Kama nyie mlinunua au ni wajanja sana mpaka mkampata nifundisheni huo ujanja….Mama…” Alimgeukia Mama yake. “Nakupenda sana lakini mimi sina uwezo wa kujipa mtoto, kama unajua Mungu anataka kiasi gani basi niambie ila kama na wewe hujui basi sitaki umsumbue mke wangu.
Kila siku mnampigia kelele kuwa hazai hazai hivi mnafikiri yeye hataki mtoto, mnafikiri yeye hataki kuitwa Mama, sasa mimi nimemaliza, hizi pesa narudisha ndani siku mkisikia Mungu anauza watoto basi niambieni nitakuja kununua la sivyo mtuache na ndoa yetu..”
Alimaliza kuongea, wote walitoka kimyakimya bila kuongea chochote. Tangu siku hiyo hakukuwa na maneno tena ya mtoto wala nini. Ben na mkewe bado hawajajaaliwa kupata mtoto, wameamua kuasili mtoto yatima na wanaishi naye kama mtoto wao na wote wanafuraha.
***** Imeandikwa Na. Iddi Makengo
Kabla hujamnyanyasa mtu kwa kitu ambacho hana uwezo nacho hembu jiulize wewe ulimpa nini Mungu mpaka akakupa hicho kitu?
Kwani kuna watu ambao wanadhani kuwa Mungu anawapenda wao zaidi na wao ni bora kuliko wengine.
Subscribe to:
Posts (Atom)


























