Monday, August 18, 2008

AGOSTI 18,2008 KUKUMBATIANA (A HUG)

Leo nimeamua kuandika swala la kukumbatiana:-

Kukumbatiana ni aina ya kugawana furaha na uchungu. Wote tunahitaji kukumbatiana kwa sababu tunajaliana. Kuanzia bibi mpaka yule umpendaye. Kukumbatiana ni kitu cha kustaajabisha (kizuri). Ni njia nzuri ya kuonyesha upendo bila kutumia maneno. Ni ajabu kuona kukumbatiana kunawapa watu furaha. Kukumbatiana kunafaa kila mahali kwa lugha zote. Kukumbatiana hakuhitaji betri. Kwa hiyo sasa inachobidi ni kuendeleza mkumbato na mpe/wape rafiki zako na yule umpendaye. Haya mimi nanza tayari sasa hivi nimesha kukukumbatia. :-)

Sunday, August 17, 2008

AGOSTI 17, 2008 KUMBUKUMBU,KUTOWEKA KWA MAMA YANGU

Mpaka leo ni miaka minne (4) imepita tangu mama yangu mpendwa Alana magnus Ngonyani aiage dunia hii. Ila kwa mimi inaonekana kama ilikuwa jana tu. Napenda kukuombea mama kwa sara hii:-


Salamu, Maria, umejaa neema,
Bwana yu nawe,
umebarikiwakuliko wanawake wote,
Na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
Utuombee sisi wakosefu,
Sasa na saa ya kufa kwetu,
Amina.


Marehemu astarehe kwa amani, Amina.




Saturday, August 16, 2008

video

Kedmon Mapena kanisa la skoghall





Nova Cantica

Agosti 16, 2008 KAMBI ZA AFRIKA KUSINI




Zaidi ya watu 60 waliuawa kutokana na ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini
Maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wameamua kuongeza muda zaidi hadi Jumatatu, kabla ya kutoa amri ya kufungwa kwa kambi sita ambazo ziliwapokea wakimbizi nchini humo, kufuatia ghasia dhidi ya wageni mwezi Mei.
Muda huo utatoa nafasi kwa mahakama ya katiba kupata nafasi zaidi, kabla ya kutoa uamuzi wake, baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kupinga hatua ya kutaka kuzifunga kambi hizo.
Mamlaka ya serikali katika mkoa wa Gauteng inaeleza kwamba ni salama sasa kwa wageni kuweza kurudi katika makazi yao.
Kambi hizo zilianzishwa mwezi Mei, baada ya zaidi ya watu 60 kuawa, na maelfu kupoteza makao yao, kufuatia ghasia dhidi ya wageni.
Mapema wiki hii, jaji mmoja wa mahakama kuu alikataa rufaa kutoka kwa makundi yanayotetea haki za binadamu, ambayo yanasema kwamba kuzifunga kambi hizo ni kuwanyima haki wakimbizi wanaoishi humo.
Awali mahakama ya katiba ilikuwa inatazamiwa kutoa uamuzi Ijumaa.
Ghasia hizo dhidi ya wageni ndizo zilizokuwa mbaya tangu siku za uongozi wa ubaguzi wa rangi uliokomeshwa mwaka 1994.
Zilianza katika mtaa mmoja kaskazini mwa Johannesburg, na kuenea kote nchini.
Walioshambuliwa walilaumiwa kwa kuchangia katika ukosefu wa ajira na kuzidi kwa uhalifu nchini humo.
Raia 21 wa Afrika Kusini ni kati ya wale waliouawa, baada ya kudhaniwa kwamba walikuwa ni wageni.

Thursday, August 14, 2008

AGOSTI 15, 2008 MAISHA YANGU


Kila nikiwaza sipati jibu, kwani maisha yangu ni tofauti sana na ndugu zangu. Mara nyingine naona kama nimetokea hewani (yaani sina ndungu na pia sina mama wala baba) niliondoka nyumbani mapema. Nikiwa na miaka 16, nilianza kujitegemea mapema sana kuliko ndugu zangu. Sijaishi sana na wazazi wangu na sijawategemea sana. Sijafaidi kuwa mtoto wao kama mwenzangu. Na pia sijawategemea sana kwa jambo la uchumi ila kwa namna nyingine. Yaani kama nilivyokuwa shuleni nilipata pesa za matumizi labda kama 200-500Tsh, na hiyo ilikuwa ni matumizi ya mwezi mzima au zaidi. . Wakati nilikuwa mdogo nilikuwa na kanga upande mmoja, vyupi viwili, magauni mawili moja la kuchezea na moja la jumapili. Nilikuwa narithi magauni ya mama, anapunguza na ananishonea mimi. Viatu nilikuwa nasikia jina tu nikipata ndala (za matairi ya gari) nilikuwa najisikia kweli. Fikiria mwenyewe kwenda mstuni kutafuta kuni bila viatu. Unachomwa na miba, unaweza kukanyaga nyoka n,k. Sio kusema wazazi wangu hawakuwa na uwezo hapana. Ila hawakuona kama ni muhimu watoto kuwa na vitu vingi. Pia nilipokuwa mdogo mambo ya kunywa soda, kula pipi hayakuwa kabisa kichwani mwangu. Kwani hatukuzoeshwa Sio kusema maisha yangu yalikuwa mabaya hapana. Mahitaji muhimu nilipata kama kawaida. Lakini sasa watoto wengi hawaridhiki na gauni/shati au suruali moja. Pia wanataka viatu. Na halafu wanataka kila mtu na chumba chake cha kulala. Mimi nilikuwa nanalala chumba kimoja na kitanda kimoja na kaka yangu . Kila mtu alionyesha kichwa upande wake. (mzungu wa nne) Lakini leo mdogo/ndugu zangu wana karibu kila kitu. Kwa jambo hili mara nyingi najisikia nipo peke yangu hapa duniani.

Maisha yangu kwa ujumla hayajawa rahisi. Kipindi kile nasoma kuwa karani nilipata shida sana mimi, asubuhi nilikuwa naamka kuandaa chai na baadaye kwenda shule kwa mguu labda kama saa moja au dakiki 45 hivi. Mchana nilikuwa nabaki shuleni, kwani mwanzoni nilikuwa narudi na sikupata chakula. (Bali ilikuwa kwenda kuchota maji unajua tena foleni kubwa.) Niliporudi na maji kuanza kuandaa chakula, na baadaye muda wa kurudi shuleni umefika. Basi ni kugeuza tena tu bila kula kwani ningekula basi ningechelewa. Nilikuwa naishi kwa "ndugu" lakini nilikuwa kama MFANYAKAZI (mama wa nyumba alikuwa mkatili mno sio mchezo). Jioni baada ya shule kufika tu bila kula kitu amekwishaandaa mahindi kwenda kusaga na niliporudi tu ni kuchukua ndoo kwenda kuchota maji na pia kuandaa mboga. Usidhani hapakuwa na watoto wao, walikuwepo. Lakini walikuwa wanacheza, kufanya homework au walikaa tu. Kila siku hivyohivyo kwa muda wa miaka 2. Labda ndio maana maisha yangu sio kama ndugu zangu, na ndio maana sikuweza kufanikisha masomo yangu vizuri. Kwa namna nyingine namshukuru (mama wa nyumba) amenifundisha jinsi ya kujitegemea, kuishi peke yangu. Ila jamani tembeeni mwoone mmh maisha ni safari ndefu.

Agosti 14, 2008 MASHAIRI

MAPENZI
Mapenzi, mapenzi, mapenzi,
Ingekuwaje bila mapenzi,
Bila mabusu na kupapasana?
Mimi nakuwaza wewe tu,
Mikono yako wakati unaponigusa,
Macho yako na mikono yako unapotabasamu,
Maisha yanapendeza,
Mpenzi, nikumbatie mimi na sema ya kuwa unanipenda.

WEWE
Wewe mpendwa, wewe ni maisha yangu,
Ambaye nataka kuishi naye,
Katika ndoto zangu, katika ndoto za maisha nakushona na uzi wa dhahabu,
Rohoni mwangu, upo wewe na mimi, tumefungwa katika nyavu.

2008,8,14 UTAJIRI WA LUGHA

Watanzania kwa kweli tuna haki ya kujivunia nchi yetu nzuri yenye amani na utulivu. Halafu sasa kitu kinachonifurahisha ni kwamba Tanzania haina utajiri wa mbuga za wanyama tu na mlima wetu mrefu Kilimanjaro ambavyo watalii huja kuangalia. Hapana, Tanzania ni tajiri wa lugha mnajua hakuna nchi yenye makabila mengi kama TZ. Makabila 129(130) ambayo ni machache tu huwa wanaelewana wanapoongea, kama vile Wangoni na Wamanda, Wabena na wahehe nk. Hii ndiyo maana Hayati baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere aliona ni vema kuwe na lugha moja ambayo watu wote tutaweza kuongea na kuelewana ni lugha ya Taifa KISWAHILI.

Wednesday, August 13, 2008

AGOSTI 13, 2008 MADAWA YA KULEVYA

Duniani wote tunapenda sana kijisikia vizuri. Tunataka kujisikia kuwa na raha, wenye nguvu na sio kuwa na wasiwasi. Hivyo wengi wetu tunaanza kufikiria kuwa dawa za kulevya, pombe na sigara zitatupa raha. Angalia sana! usidanganyike! kutumia vitu hivyo ili kupata furaha bali ni kuhatarisha maisha kwani unaweza kujikuta umeingia ulevini. Kujinasua kwenye hali hiyo itakuwa kasheshe kwelikweli (si lelemama) inahitaji moyo na pia kujizatiti.


Leo nimejisikia kuandika kwa kiswidi pia ili nao wafurahi:

LIVSSTILSHOT
Tobak är gift för kroppen
Rökning är extremt skadlig och ökar risken för cancer, sjukdomar i luftvägarna, hjärt-kärlsjukdomar, typ 2- diabetes, magsår, benskörhet, nedsatt fruktsamhet och dålig sårläkning. Tobaksrök innehåller över 4000 olika ämne, varav många äa giftiga - till exempel koloxid och nikotin - medan en del är tjärämnen och andra partilar som sätter sig i luftvägarna.
Alkohol ger organskador
Alkohol i en mängd överstigande 15ml ren alkohol per dag är skadlig för bukspottkörtel, tarm, lever samt nervcellerna i hjärnan och andra ställen i kroppen. Organskadorna kan leda till dåligt upptag av vitaminer och mineraler, viliket i sig påverkar hälsan negativt. Alkoholens skadeverkningar beror på att det är ett lösningsmedel som irriterar cellerna och belastar leve.

Tuesday, August 12, 2008

AGOSTI 12,2008 RAHA YA KUWA NA MISITU

UYOGA




BLUEBERRY
Raha ya kuwa na misitu leo nimeenda msituni nimachuma uyoga pia blueberry(samahani naomba msaada sijui blueberry ni nini kwa kiswahili.

AGOSTI 12,2008 URAFIKI, MAPENZI NA NDOA

Mara nyingi nimekuwa nimejiuliza:- Hivi maisha yangekuwa vipi kama kusingekuwa na urafiki? Rafiki si mtu tunayecheka na kufurahia naye maisha tu, hapana bali pia tunayekuwa naye katika shida na raha! Marafiki hutusaidi kupata majibu ya maswali mbalimbali yanayotukabili. Katika ndoa, urafiki ni msingi imara kwani wanandoa wanatakiwa kuwa marafiki. Lakini hata hivyo bado sijapata jibu sawa sawa kuwa rafiki wa kweli ni nani? na anatakiwa kuwa na sifa gani?

Monday, August 11, 2008

AGOSTI 11,2008 LUNDO, KUMBUKUMBU

Leo nimekumbuka sana Lundo, eeh jamani ilikuwa kazi kweli. Wale wote waliofika Kijiji cha Lundo Tanzania. Yaani pale Lundo shule ya msingi ya wakimbizi kwa sasa inaitwa Lundo Secondary School.

Mnajua pale shuleni kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali kama vile mapapai, machungwa, malimao, ndizi n.k. Na mimi ilikuwa kazi yangu kila baada ya shule nilirudi tena shuleni, nilikuwa mwizi wa malimao nilikuwa nakula sana malimao kwa siku nilikuwa nakula 10. Mama alikuwa analalamika sana. Kwani nilikuwa nakula na chumvi iliyochanganywa na pilipili. Nilikuwa siibi malimao tu chumvi pia.

Halafu magauni yangu na sketi zilikuwa na matobo sana, sababu nilikuwa nabebea malimao. Mmh! jamani Lundo sitasahau, yaani kujificha kwa kweli nilikuwa mwizi maalufu kwani sikushikwa. Ila sasa siwezi kula malimao zaidi ya nusu limao nimekinai kabisa.

LUNDO BAADA YA MIAKA ISHIRINI
Mmhh furaha, hisia pia raha vilinijia siku hii yaani mwaka jana 2007. Fikiria mwenyewe sehemu uliyozaliwa, sehemu ulianza darasa la kwanza halafu umeondoka na baada ya miaka 20 unarudi/tembelea tena.
Ila nilisikitika kidogo kwani sikuweza kujua ni nyumba gani nilizaliwa/ishi kulikuwa na mabadiliko mno. Ila cha kufurahisha zaidi ni kwamba nilionana na mjomba wangu ambaye sikumwona tangu 1985. Siku hii nilikuwa kama mtoto mdogo nilikimbia na kumrukia mjomba kwa jinsi nilivyokuwa na furaha. Mpaka machozi yalinitoka. Kwa vile mjomba anajua mimi napenda nini aliniandalia samaki What a joy. pia nilifurahi zaidi kujua alikumbuka jina langu la utani ambalo hata mwenyewe nilisahau. Mnataka kujua au? Okey ni (KANYANJA) kilugha kiswahili kanyasa. Sasa mnajua .

Sunday, August 10, 2008

AGOSTI 10,2008 KUMBUKUMBU

Angekuwa sweden huyu angaumia kweli na baridi.Kwani hapa wakati wa joto ni kama makambako.

Saturday, August 9, 2008

AGOSTI 9,2008 MIMI YASINTA

Leo, kuna jua kidogo nimeamka nimevaa nguo zangu za mazoezi na kuanza kukimbia baada ya kukimbia kidogo mvua hiyo lakini kwa vile nilishaamua kukimbia basi nimeendelea nimekimbia kilimeta 5. Ila sasa nimerudi na natetemeka kama kifaranga cha kuku. Nataka nifanye mazoezi ili niiwakilishe Nchi yangu Tanzania kwa jinsi ninavyoipenda. Mnajua hii hali ya hewa ya hapa inaniuzi sana kwani kila siku hali nyingine leo jua kesho mvua keshokutwa baridi na hata pengine theruji hakuna msimamo. Kwa hiyo kama hujitosi tu kukimbia au kuwa mstuni labda kutafuta uyoga au matunda basi utabaki ndani ya nyumba siku hadi siku.

Mnajua leo nimekumbuka sana nyumbani kwa hiyo nimeamua kupika ugali na mchicha pia maharage. Nimeukanyaga kweli lakini hata hivyo haitoshi kwa hiyo nimeamua kusikiliza mziki.

Friday, August 8, 2008

8,8 .2008 SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE








Mwenzenu nilisahau kabisa kuwa leo ni sikukuu ya nane nane. Kuna rafiki kanikumbusha asante sana kwani bila wakulima hatungekula.

Thursday, August 7, 2008

AGOSTI 7,2008 THE KONDOA-IRANGI ROCK PAINTING

Hapa ilikuwa zamani za kale kule Kondoa baina ya Singida na Irangi Hills. Ni baina ya miaka 19000 na 30000 iliyopita babu zetu walikuwa wakichoro kwenye mawe safi eeeh.

AGOSTI 7,2008 NYWELE




The Sixties were the era of long hair.As long as the hippies were wearing their hair long and bein' against war and stuff, Black people decided they wanted to do it, too. Hippy hair hung down, Black people's hair went in every direction. This was known as the Afro.
This looked so neat that white people started getting perms so they could have Afros, too. But then Michael Jackson turned white, so Black people decided maybe they'd do corn rows instead.

Wednesday, August 6, 2008

Agosti 6, 2008 KIJIJI CHA IFINGA

Mpunga


Kanisa

Najua wote mtashangaa sawa mnaruhusiwa kushangaa. Kwani mimi leo nimetembelea kijiji kimoja kiitwacho Ifinga, Kijiji hiki ni maalufu sana kwa kilimo cha mpunga. Kwa hiyo ukifika/tembea Ifinga chukua na unga wako usije ukatamani ugali kwani wao wanakula wali kila siku siku wanayokula ugali ni sikuuu au jumapili tu.

Tuesday, August 5, 2008

AGOSTI 5,2008 AFYA

Mwenzenu nahisi kuchanganyikiwa. Labda kwa sababu nina tamaduni/mila na desturi mbili najua mimi ni mtanzania na najua mila na desturi pia utamaduni wangu. Lakini sasa kichwa/akili yangu imevurugika kabisa:-

Ni hivi najua nyumbani TZ ni kawaida au labda niseme safi kama mtu umenenepa/nawili. Nakumbuka mwaka wa kwanza niliporudi TZ kusalimia watu walishtuka/shangaa sana na kuzani nilikuwa na ngoma au. Na baada ya miaka kadhaa nikarudi tena na wote walifurahi na kusema ya kwamba hivi ndiyo inavyotakiwa, wao walisema ya kwamba nilipendeza yaani niliongoza kilo kidogo nilinenepa. Na niliporudi hapa watu walisema eeh? Mbona unanenepa sana si vizuri inabidi upungue. Sasa nadhani mmegundua kwa nini nimesema nimechanganyikiwa. Ngoja niendelee kidogo kiundani au niseme kiafya nakubaliana na "waswidi" wazungu, lakini hali hii inanipa hofu kidogo kwani sasa hata watoto wadogo wanafuata mwenendo wa wazazi na marafiki pia, wanajinyima kula. Na wengine wanakula kama kawaida na baadaye wanatapika makusudi. Mnajua wanasemaje, eti wanataka kuwa wembamba, ndiyo wanapendeza. Lakini ukiwaangalia wanaonekana kama mti hata matako (wowowo) hawana.
Ndiyo najua kunenepa sana sio safi kwani kuna madara yake kama vile mshtuko wa moyo(heart attack) daibetes nk.

kama nilivyosema hapo juu mara nyingi sijui mimi ni nani na nchi gani ni yangu. ndio maana nimesema nimechanganyikiwa. Watanzania (waafrika) wanaona kunenepa ni safi na wazungu wanasema ni hatari, Na najua hakuna anayesema kweli au uongo. Je wasomaji mnasemaje Nisaidieni kidogo!!!!!!!!!

Monday, August 4, 2008

Agosti 4, 2008 SAMER/WAMASAI



Hapa nataka kusema sio wamasai tu wanaishi kwenye nyumba kama hizi manyata kwani hata hapa Sweden kuna watu aina ya wamasai wanaitwa Samer wao ni maalufu sana kwa kufuga (rendeer) kulungu kwani wao wanaishi sehemu ya baridi sanaaaa. Na wamasai wetu wote tunajua maalufu kwa ufugaji wa ngómbe.

Saturday, August 2, 2008

AUGOSTI 2, 2008 HALI YA HEWA NYUMBANI SONGEA

Kama mnataka kuangalia hali ya hewa Songea Bonyeza hapa

AUGOSTI 2, 2008 UTANI

Kuna watu wengi wanapenda sana mambo ya utani kiasi kwamba yule anayempa ule utani anaami ni au anaweza mpaka kuchanganyikiwa. Mimi mwenyewe ni moja wa watu hao, napenda sana utani laki ni sio kwamba nataka kuwatesa au kuwachanganya la hasha. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama ule utani umepita mipaka na unakaribia kuwapoteza marafiki zako wote utafanyaje. Kwani hilo swali nimepata leo kwa rafiki mmoja amemdanganya rafiki yake kwamba wakutane sehemu furani lakini kumbe ni uwongo je afanyeje ili wawaze kuwa marafiki tena. Kwani anajisikia vibaya pia anaona aibu kwa kuwa mwongo. Hataki kumpoteza rafiki yake kwani ni mabest. Pia anasema kwa vile wako mbalimbali kama ingekuwa karibu angejaribu kuongea naye na kuomba radhi. Kwa yeye aliona kama ni mchezo. Wasomaji naomba mnisaidia nimwambieje huyo ili amwambie rafiki yake wa mbali.

Thursday, July 31, 2008

31 JULAI 2008 MJI MKUU AU?

mwenzeni leo nimekuwa bungeni. Nawaona jinsi mnavyoona wivu

JULAI 31,2008 USAFIRI


Mimi sisemi nawaachieni wasomaji

JULAI 31, 2008 KWAYA TENA


Mwenzenu leo nimefurahi sana nimeiimba kwa kiswahili nyimba za kumsifu mungu. Yaani raha kweli nimejikuta nipo nyumbani nimesahau kutamani nyumbani. Mmmm najua wengi mnaona wivu mtajiju.

JULAI 31,2008 KWAYA